Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kudumu kwa mahusiano kunategemeana na juhudi za pande zote mbili (mwanamke na mwanaume); na iwapo upande mmoja utalemaa, kuna uwezekano mkubwa kwa mahusiano kuvunjika. Baadhi ya juhudi wanazotumia:-
- Wapo wanaotumia fedha
- Wapo wanaokuwa wapole ili mahusiano yadumu
- Wapo wanaojiongezea mapambo ili waendelee kutamanisha
- Wapo wanaojiweka safi na kujipiga pamba ili kutamanisha
- Wapo wanaotumia nguvu zao za ushauri ili kudumisha mahusiano
- Wapo wanaotumia mitishamba/ndumba/limbwata n.k
- Wapo wanaotumia elimu yao kama kishawishi kwenye mahusiano
- Wapo wanaotumia njia za kuwa karibu karibu ili mwingine asiwahi nafasi
- Wapo wanaotumia ufundi mwingi faragha ili kudumisha uhusiano n.k