Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?


Sawa sawa
 
Naweza fanya order kila weekend kama upo Dar!!!
 
Tumia maji ya Moto kukanda, Maji yakiwa ya Moto weka mafuta ya kupikia kwenye hayo maji then weka sukari/Chumvi then weka unga Kanda. Chapati zinatoka lainii
 
Nikiona mada za chapati namkumbuka dada yangu Carleen
Binafsi mbinu zote nimemaliza lakini tokeo la mwisho ni lile lile either kaukau ama ugumu...nimeamua kukubali kushindwa
Kweny kuchanganya unga wako kabla hujakanda jaribu kutia sukari kidogo inafanya unga kua laini.
 
Kwenye chapati, maua wapewe wanawake wa Zenji...chapati ya nazi na siagi...noma sana!
 
Chapati za Tanga [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mimi nina Aunt yangu mmoja anaishi tanga aisee yaani akipika chapati zake wallahi utaenjoy zinakuwa laini mno ukila mpaka raha yaaan..sasa nina manzi yangu siku moja ananiambia babe leo nakupikia chapati maini nami nikajibu hayaaaa twende kazi..ahahahah jamani chapati ngumu kuliko maisha yangu.nilicheka mpaka akasusa kula.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…