Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Unatumia utaalamu gani kufanya chapati zako za kusukuma ziwe laini?

Pole bas tumia mafuta
Juz nilijaribu kukanda na mafuta kidogo nikachanganya na prestige na wakati wa kuzipaka mafuta na kuzikunja nikatumia prestige nikazichoma Kwa mafuta zilikuwa tamu sana na laini zikabaki nikazisahau nikashtuka siku ya pili jion Bado zilikuwa laini sana

Sawa sawa
 
Habari Wakuu,

Chapati za kusukuma ni pishi ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi, mtu anajitahidi alkini mwisho wa siku anatoa chapati ngumu na imesimama kama sinia😂🤣.

Mbinu ninayotumia mimi kufanya chapati iwe ni laini, ni kukanda unga na kuhakikisha umekuwa laini kabisa. Tumia hata muda mrefu kama huna nguvu sana mikononi ila hakikisha donge lako linakuwa laini kabisa. Na kipindi unakunja mwanzo fanya iwe nyembamba sana kama karatsi, muda wa kusukuma ili uchome iwe wastani, isiwe nene sana haitaiva na isiwe nyembamba sana itakua kaukau.

Pia wakati wa kuchoma, kama umeweka chapati kwenye kikaango na haifuri jua kuna kitu umekosea, inaweza kuwa hujakanda unga vizuri au umeweka nene.

Lete maujuzi yako mpishi, unatumia njia gani kufanya chapati yako inakuwa laini?
Naweza fanya order kila weekend kama upo Dar!!!
 
Tumia maji ya Moto kukanda, Maji yakiwa ya Moto weka mafuta ya kupikia kwenye hayo maji then weka sukari/Chumvi then weka unga Kanda. Chapati zinatoka lainii
 
Nikiona mada za chapati namkumbuka dada yangu Carleen
Binafsi mbinu zote nimemaliza lakini tokeo la mwisho ni lile lile either kaukau ama ugumu...nimeamua kukubali kushindwa
Kweny kuchanganya unga wako kabla hujakanda jaribu kutia sukari kidogo inafanya unga kua laini.
 
Kwenye chapati, maua wapewe wanawake wa Zenji...chapati ya nazi na siagi...noma sana!
 
Chapati za Tanga [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mimi nina Aunt yangu mmoja anaishi tanga aisee yaani akipika chapati zake wallahi utaenjoy zinakuwa laini mno ukila mpaka raha yaaan..sasa nina manzi yangu siku moja ananiambia babe leo nakupikia chapati maini nami nikajibu hayaaaa twende kazi..ahahahah jamani chapati ngumu kuliko maisha yangu.nilicheka mpaka akasusa kula.
 
😂😂😂
 
Back
Top Bottom