Unatumia vigezo gani kujua mpenzi uliyenaye ni sahihi?

Asante kwa swali zuri na la msingi sana.
Hakuna kigezo kimoja mtu anachoweza kutumia kujidhihirishia kuwa aliyemchagua ni mwenza sahihi. Aidha vigezo huweza kutofautiana kulingana na matakwa au matarajio ya mtu binafsi. Hapa nitataja baadhi ya vigezo kwa mtazamo wangu.

1. Aina ya vitu anavyopendelea. Mfano anapenda muziki (je wa aina gani), anapendelea movie za aina gani kama ndio. Vitu anavyopendelea vinaonesha ni mtu wa aina gani.

Kama anapendelea kwenda kwenye kilabu cha pombe probably ni mlevi. Anaenda gym, viwanja, shisha, kote andako zingatia sifa zake.

2. Hobies zake βœ“ vitu anavyopendelea vinaniongoza kujua ni mtu ambaye tunaendana au lah!

3. Nature ya marafiki zake (watu anaopendelea kuishi nao kwa mara nyingi)

4. Nature ya mavazi yake. Lazima nipime consistency yake nijiridhishe. Anavyovaa kanisani, darasani, sokoni, libray maybe, kwenye jamii. Especially kwenye maeneo ambayo yupo free kujiamulia life style yake. (Napenda awe anavaa mavazi yenye stara. Kama yeye hawezi kujistiri, ataweza kunistiri mimi na wengine?).

5. Uwajibikaji. Anavyowajibika kwa watu wanaomzunguka, ndugu zake, wazazi, jamii, na kwa Mungu pia. Lakini pia anavyowajibika kwake mwenyewe. Anatambua wajibu wake na mipaka yake?

* Zaidi awe mtu real, awe natural. Sio anayeishi kwa mkumbo. Mtu anayeishi kwa mkumbo ni mtu anayelazimika kufanya mambo hata ambayo hayamfuraishi, hayamunufaishi, na wala hayana tija. Ila ni kwa vile tu anaonaga wengine wanafanya.

βœ“ Awe anajielewa na kujitambua, mwenye mipaka na malengo. Mwenye kujiheshimu na kujipenda.

βœ“ Awe msafi.
βœ“ Hasiwe mshirikina πŸ˜‚, hasiwe na makandokando yanayovunja uadilifu.
βœ“ Nazingadia pia matumizi ya lugha. Anavyoandika sms, anavyoongea na watu wa rika tofautitofauti. Binafsi napendelea mtu anayetumia lugha rasimi, sio lugha za kihuni. Japo natambua masuala ya misimu, na rejesta.

Nazingatia pia masuala ya afya, na uthabiti wa kihisia. Anaweza kudhibiti huruka, mihemko, hasira, huzuni, upweke?

Ana mipaka?
 
Awe anahudumiwa na mwanaume mwingine huku akiwa na wewe πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… hata kujitolea kazini ni miezi mitatu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…