Mnyakyusa5000
Member
- Sep 21, 2021
- 83
- 136
Kumezuka makundi ya watu wanaoshabikia mabadiriko ya mtaala wa elimu Tanzania wakidai kuwa mtaala huu ni mbovu kwani hauendi na wakati na haumwezeshi mwanafunzi kutatua changamoto halisi za maisha zinazomkabili. Hofu yangu ni kuwa watu wengi hawaufahamu mtaala wa elimu Tanzania. Wamejiingiza kwenye wimbi la mabadiriko bila hata kufanya utafiti wa kutosha.
Nathubutu kusema tena kwa ujasili kuwa mtaala wa elimu Tanzania bado ni bora na unaweza kutumika hata kwa nusu karne ijayo. Hoja ya mabadiriko ya mtaala ni ya kisiasa na propaganda yenye lengo la kuficha udhaifu mkubwa uliopo katika utekelezaji wa mtaala uliopo. Tutabadili mitaala ya elimu hata mara elfu kumi lakini kama hatutaweka nguvu katika utekelezaji wa mitaala hiyo basi kila mtaala utaonekana kuwa mbovu.
Ndani ya makala hii nitaelezea kwa lugha rahisi sana juu ya nini hasa maana ya mtaala wa elimu, mambo muhimu yanayofanya mtaala uliopo sasa uwe bora na mwisho ni jinsi gani utekelezaji wa mtaala huu ungeweza kuipa nchi yetu matunda tunayoyatarajia katika mtaala mpya wa elimu.
Mtaala wa elimu ni nini?
Mtaala wa elimu ni mwongozo wa ujumla wa nini kifundishwe na kusomwa katika ngazi zote za elimu ndani ya jamii fulani mahususi. Mtaala wa elimu huhusisha pia muda wa kufundisha au kujifunza kitu hicho na namna kinavyotakiwa kufundishwa.
Katika nchi yetu (Tanzania) mtaala uliopo unatoa mwongozo juu ya shughuli zote za kielimu zinazopaswa kufanyika katika ngazi zote za elimu yaani ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Katika makala hii nitazungumzia kwa ukubwa na kutoa mifano mingi katika ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari ingawa kiukweli maelezo nitakayotoa hayabagui ngazi nyingine za elimu ambazo nitazigusia kwa uchache.
Mambo yanayofanya mtaala wa sasa kuwa bora
Mtaala wa elimu Tanzania unatoa mwongozo wa shughuli za aina mbili katika taasisi zote za kielimu. Shughuli hizo tunaweza kuziita hivi:
(I) Shughuli za darasani na
(Ii) Shughuli za nje ya darasa
Kila shughuli ya kielimu kati ya hizo mbili ina malengo yake na imepewa namna inavyopaswa kutekeleza. Hebu tuangalie shughuli hizo kwa undani kidogo.
-Shughuli za darasani
Shughuli hizi zinahusisha mambo yote ambayo hukuza taaluma ya mwanafunzi. Tunaposema taaluma ya mwanafunzi tunazungumzia mafunzo yanayokuza uwezo wa kiakili kwa mwanafunzi. Uwezo wa kiakili hupimwa katika viwango tofauti kama vile: uwezo wa mwanafunzi kuchambua mambo, uwezo wa mwanafunzi kujielezea, uwezo wa mwanafunzi kutunza kumbukumbu, uwezo wa mwanafunzi kutatua changamoto kinadhalia n.k
Lengo kuu la shughuli hizi limebainishwa katika kila muhtasari wa masomo ambayo mwanafunzi anatakiwa kuyasoma. Kupitia shughuli hizi ndio nchi yetu inaweza kutengeneza wataalamu wa kada mbalimbali kama vile: Madaktari, waalimu, waanasheria, wahasibu na kadhalikia.
-Shughuli za nje ya darasa.
Mtaala wa elimu ya Tanzania unatoa mwongozo wa shughuli zote za kielimu zinazopaswa kufanywa nje ya darasa. Shughuli hizi huhusisha mafunzo na kazi ambazo humwezesha mwanafunzi kukuza vipaji vyake, kuongeza uwezo wa kuzalisha, kukuza ushirikiano wa wenzake, kuweka stadi alizojifunza kwa ndharia ndani ya darasa katika vitendo na kupambana na changamoto za kimaisha.
Kila tasisi ya elimu katika ngazi zote za elimu Tanzania ina ratiba ya shughuli zote zinazopaswa kufanyika katika siku zote za masomo. Katika ratiba hizo, mtaala unaweka msisitizo wa kuwepo kwa shughuli za nje ya darasa kwa saa angalau mbili na shughuli za ndani ya darasa angalau nne.
Katika shughuli za nje ya darasa mtaala unaelekeza kuwa mwanafunzi ajifunze kwa vitendo mambo kama vile:- michezo, sanaa, kilimo, mapishi, ujasiliamali, jinsia, stadi za maisha na mambo mtambuka yaani current issues.
Jinsi utekelezaji wa mtaala huu ungeweza kuleta matunda kwa nchi yetu
Ukiacha shughuli za darasani ambazo mara nyingi ndizo zinazotiliwa mkazo na wasimamizi wa mtaala(serikali) na watekelezaji wa mtaala (Shule) kuna mapungufu makubwa katika usimamizi na utekelezaji wa mtaala katika shughuli za nje ya darasa.
Bado hata katika shughuli za ndani ya darasa tunashudia changamoto nyingi za kiutekekezaji ikiwepo ya upungufu wa waalimu na vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji.
Katika ngazi mbalimbali za elimu hasa awali na msingi kuna changamoto ya waalimu kwenye sifa za kiwango cha juu cha utaalamu wa ufunzaji. Pia mapungufu katika vitendea kazi. Jambo hili limeleta changamoto katika kuvuna matunda ya mtaala wa sasa kwa shughuli za ndani ya darasa na hivyo kuleta mapungufu katika ubora wa wahitimu katika shughuli za ndani ya darasa
Katika shughuli za nje ya darasa ndio kuna usimamizi na utekelezaji hafifu kabisa. Taasisi za elimu zimekosa wataalamu wa shughuli hizo. Shule hazina wataalamu wa mahususi wa michezo na sanaa, ujasiliamali, kilimo na mambo mtambuka.
Kama utekelezaji wa mtaala wa sasa ungewezekana hata kwa asikimia sabini na tano basi nchi yetu ingepiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko ilivyo sasa. Hii ni kwa sababu shughuli zote zinazoelekezwa na mtaala huu zinalenga kutatua karibia changamoto zote ambazo watu wanasema kuwa hazitatuliwi na mtaala wa sasa.
Shida sio mtaala wa elimu Tanzania, shida ni utekelezaji wake.
TUCHUKUE HATUA

Upvote
3