Hongera kwa ubunifu. Wakuu naona hamjamwelewa yeye anazungumzia kilo ambazo unatakiwa uwe nazo in relation to your height ingawa amekosea kusema pima bila kutumia mzani, kwa jinsi ninavyofahamu uzito in relation to your height inakumpa kitu kiitwacho MBI yaani body mass index. BMI= W/H2 . H= height square should be in metre. BMI 18.5 - 24.5 normal, < 18.5 underweight, 25-33 over weight and > 33 obesity. Sasa ukichukua formulae ya mshikaji hapo ni kwamba ukipima urefu wako nafikiri ni applicable kwa adult, mfano mimi urefu wangu ni 156cm ukitoa 100 inabaki 56cm. Sasa inamaana uzito wangu kwa kawaida inatakiwa niwe na kg 56. Ukitafuta BMI kwa kg 56 na urefu 156cm BMI inakuwa 23 ambayo ni normal. Lakini sasa mimi nina kg 67 kwa urefu huo huo yaani 156cm ambapo unapata BMI ya 27.5 ambayo ni over weight. Hivyo natakiwa nipunguze kg 11 ili niwe na BMI 23: sasa basi inamaana ukijua urefu wako na uzito wako itakurahisishia kujua zimezidi kilo ngapi. Naamini mtanielewa kama hujaelewa uliza swali.