Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Walokole wengi ni makapuku, makabwela, mafukara, Apeche Alolo, Hohehae, Pangu pakavu tia mchuzi.
Sio walokole tu , ni wote wanaojiita wafia dini,.....wanafunga maduka saa saba mchana kwenda kwenye ibada kila siku,...🄲
 
Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo

Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.

Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
Akuja kuangukia pua na meno wee mfuatilie tu.
 
Story zake zinatisha, utaweza?šŸ¤’šŸ¤’
Ntaweza si nazama ndani ya handaki nakuta bonge la nyoka limezunguka sanduku lenye mali?? Naweza mkuu utajiri unahitaji mtu jasiri kama mimi 😹
 
Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo

Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.

Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
Kuna watu wanaikimbilia dunia kwa kudhulumu watu, kuuwa n.k, kana kwamba wataishi milele

ayat 20 from Surah Al-Hadid
ļ“æŲ§Ų¹Ł’Ł„ŁŽŁ…ŁŁˆŲ§ Ų£ŁŽŁ†Ł‘ŁŽŁ…ŁŽŲ§ Ų§Ł„Ł’Ų­ŁŽŁŠŁŽŲ§Ų©Ł Ų§Ł„ŲÆŁ‘ŁŁ†Ł’ŁŠŁŽŲ§ Ł„ŁŽŲ¹ŁŲØŁŒ ŁˆŁŽŁ„ŁŽŁ‡Ł’ŁˆŁŒ ŁˆŁŽŲ²ŁŁŠŁ†ŁŽŲ©ŁŒ ŁˆŁŽŲŖŁŽŁŁŽŲ§Ų®ŁŲ±ŁŒ ŲØŁŽŁŠŁ’Ł†ŁŽŁƒŁŁ…Ł’ ŁˆŁŽŲŖŁŽŁƒŁŽŲ§Ų«ŁŲ±ŁŒ فِي Ų§Ł„Ł’Ų£ŁŽŁ…Ł’ŁˆŁŽŲ§Ł„Ł ŁˆŁŽŲ§Ł„Ł’Ų£ŁŽŁˆŁ’Ł„ŁŽŲ§ŲÆŁ Ū– ŁƒŁŽŁ…ŁŽŲ«ŁŽŁ„Ł ŲŗŁŽŁŠŁ’Ų«Ł Ų£ŁŽŲ¹Ł’Ų¬ŁŽŲØŁŽ Ų§Ł„Ł’ŁƒŁŁŁ‘ŁŽŲ§Ų±ŁŽ Ł†ŁŽŲØŁŽŲ§ŲŖŁŁ‡Ł Ų«ŁŁ…Ł‘ŁŽ ŁŠŁŽŁ‡ŁŁŠŲ¬Ł ŁŁŽŲŖŁŽŲ±ŁŽŲ§Ł‡Ł Ł…ŁŲµŁ’ŁŁŽŲ±Ł‘Ł‹Ų§ Ų«ŁŁ…Ł‘ŁŽ ŁŠŁŽŁƒŁŁˆŁ†Ł Ų­ŁŲ·ŁŽŲ§Ł…Ł‹Ų§ Ū– ŁˆŁŽŁŁŁŠ Ų§Ł„Ł’Ų¢Ų®ŁŲ±ŁŽŲ©Ł Ų¹ŁŽŲ°ŁŽŲ§ŲØŁŒ Ų“ŁŽŲÆŁŁŠŲÆŁŒ ŁˆŁŽŁ…ŁŽŲŗŁ’ŁŁŲ±ŁŽŲ©ŁŒ Ł…Ł‘ŁŁ†ŁŽ Ų§Ł„Ł„Ł‘ŁŽŁ‡Ł ŁˆŁŽŲ±ŁŲ¶Ł’ŁˆŁŽŲ§Ł†ŁŒ ۚ ŁˆŁŽŁ…ŁŽŲ§ Ų§Ł„Ł’Ų­ŁŽŁŠŁŽŲ§Ų©Ł Ų§Ł„ŲÆŁ‘ŁŁ†Ł’ŁŠŁŽŲ§ Ų„ŁŁ„Ł‘ŁŽŲ§ Ł…ŁŽŲŖŁŽŲ§Ų¹Ł Ų§Ł„Ł’ŲŗŁŲ±ŁŁˆŲ±Łļ“¾
[ Ų§Ł„Ų­ŲÆŁŠŲÆ: 20]

Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.​

Ukiwa tajiri Africa hakikisha ndugu zako, HAWAUMWI, HAWAFI, pia WANAFANIKIWA,....vinginevyo utaambiwa UNAWAROGA, UNAWATOA KAFARA na KUWAIBIA NYOTA,....shity mindset 🚮🚮🚮
Nina wasiwasi na huu uandishi wa herufi kubwa, isijekuwa jiwe lililorushwa gizani limekupata.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Nina wasiwasi na huu uandishi wa herufi kubwa, isijekuwa jiwe lililorushwa gizani limekupata.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
natumia herufi kubwa kama mkazo tu,...zaidi ya hapo una uhuru na haki ya kutafsiri utakavyo
 
Yoda

Kwa sababu umeuliza wacha leo nikuambie visa3 sio vya kuhadisiwa

Kisa cha kwanza ni babu yangu mwenyewe. yeye ni mnyantuzu alienda kwa mganga akafanyiwa yake kisha akaapiwa nakuambiwa nenda baada ya siku kadhaa atakuja mgeni mpokee kwa ku nyunyizia maziwa fresh yaani yale maziwa unayameza mdomoni kisha unayapuliza ukimpulizia huyo mgeni na muda huo hujui mgeni atakuwa aina gani.

Babu akarudi kusubiri mgeni baada ya siku 9 mchana wanamenya mihogo kwa ajiri ya udaga chatu mkubwa wakamuona anakuja nyumbani family ikatahamalaki kwa uoga na wengine kufata fimbo.

Cha ajabu babu akaagiza yafatwe maziwa na kutekeleza kama aliyoambiwa baada ya kumaliza zoezi lile nyoka alienda moja kwa moja hadi sehemu ile ya kuhifadhia nafaka ninyi waswahili mnaita stoo huku kuna majina kama ng'hunguku ama kwenye maruli.

chatu yule alikuwa na tabia ya kwenda na kurudi akirudi mifugo itazaa sana yaani kila kazi ya mwanafamilia atakayofanya
inakuwa na mafanikio tele sio kilimo wala mifugo vyote vilienda vyema.

Kuna jamaa mwingine sitataja uhusiano wake hapa ila ni ndg kabisa. kazi yake ya kuchimba dhahabu huyu jamaa alikopa hela za kutosha bank na akashindwa kurejesha jamaa akawa katika msongo mkubwa wa mawazo.ndipo akaambiwa na jamaa yake wa karibu mchimbaji wa dhdhabu vilevile akampa abc zote na kumhakikisha swala lako ni dogo sana hili iwapo upo tyr twende kwa mtaalamu. kwa sababu ya umaarufu aliokuwa nao pia kufirisiwa anaogopa aliukubali ushauri wa jamaa.

Walipo enda akapewa maelekezo yote kisha akaombwa kijana wake wa kwanza . jama hakusita na dogo akapita kushoto. Basi ukwasi ukazidi mara2 zaidi ya mwanzo tena kwa ghafla mnoo duara zake zikawa za kugusa tu anapata. mfano mwaka 2017 yeye mfuko wa mawe ya duara zake kg50 alikuwa anauza m13 wengine m1au tatu wengini ni laki7 nk.

Nikiwa kama kiongozi wa duara zake tulikuwa tunafanya makubwa sana na tukiwa ofisini kwakwe kuna mambo ya kutisha tulikuwa tunaona watu 3 tu yaani mimi yeye na mtoto wake wengine hawaoni.

mfano siku moja nikiwa mwazwilo machimboni mimi na mtoto wake tulipewa maagizo na jamaa kuwa leo mnaugeni hapa mtafanya kama nilivyo waambia. tukakubali na tukasubiria huo ugeni uje midaa kama ya saa8 mchana tuliona mnyama wa ajabu maarufu sana Tz hii kaambana na chatu mkubwa mno. baada ya kuona tuliingia ndani kufanya yetu mkitoka kule ndani wa nje hawamuoni mtafanya kila kitu lakini kamwe hawatakuona hata awe mchawi hawezi kukuona. Yule mnyama alipofika kambini akiwa na chatu na wanatembea taaratibu tukafanya kama tulivyoambiwa na kuwaruhusu warudi. Na walikuwa wanaenda kupotelea maduarani wanaishia bila kuelewa wameenda wapi.

Kitakachofuata hapo ni duara zitachanganya hadi na ninyi mnachanganyikiwa pia hela nje nje.

Huyo jamaa akao mke wa2 na hapa sasa story ya kumtoa mtoto wake wa kwanza tuliijua yule mke mkubwa alienda akiria kwa mama mkwe wake akisema hadharani "'mama unajua kabisa nilimtoa mwanangu ili tufanikiwe kimaisha na mme wangu leo tumefanikiwa kaoa mwanamke mwingine Nimemoksea nini mimi mwanao?" kama haitoshi hapo nyumbani mtoto mwingine (KE) alikuwa na kichaa na yeye kumbe kashawekwa akianza anguka ama kutoka makamasi na kufanya mambo ya ajabu ajabu.Biashara za jamaa ndo zinapamba moto sana na aliyekuwa anasimamia ni huyu mwanamke wake mkubwa mtama akaumwaga wote ndo kujua kumbe mtoto alikufa kimaajabu ajabu kumbe sababu ilikuwa ni hii.

Mimi baada kutoka machimboni nikiwa na hela kiasi chake yale mambo japo niliya zoea lakini bado yalikuwa yana nisumbua sana kichwani hata nikiwa nimelala mara napiga yowe usiku maana yalikuwa yananijia mara kwa mara.

Nilikaa na wazazi nikaawaambia yote jibu la wazazi lilikuwa ni moja tu kutoka kwa mzee KAMA UNAJUA SISI NDO TULIOKUZAA ACHANA MARA MOJA NA NDG YAKO HUYU NAWEWE ATAKUPELEKA HUKOHUKO MWISHO UTUUE.muda huo mama akilia akisema ungeliwa na yule chatu nani angetuambia?

Ya3 sitaandika zitoshe hizi tu.

Mara zote huwa nasema hapa Iwapo unaamini kabisa haya mambo hayapo yamkini uko sawa kabisa.Na yule asiye amini kuwa yapo yupo sawa vilevile.

NIMESHAOKOKA SAII MSIJE PM. BWANA ASIFIWE SANA.
 
Ujinga mtupu!

Hakuna utajiri wa mambo ya kishirikina.

Tanzania ni nchi yenye watu wajinga na wapumbavu wengi sana.

Si ajabu Tanzania nzima kwa sasa ambao tunayakataa hayo mambo kuwa yapo, hatufiki hata watano.
 
Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo

Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.

Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
Kwahiyo ephen_ kama mama ako angekubali enzi hizo inawezekana ungeshakuwa umetolewa kafara wewe..?!šŸ¤”
 
Ujinga mtupu!

Hakuna utajiri wa mambo ya kishirikina.

Tanzania ni nchi yenye watu wajinga na wapumbavu wengi sana.

Si ajabu Tanzania nzima kwa sasa ambao tunayakataa hayo mambo kuwa yapo, hatufiki hata watano.
Umeshawahi kaa ukatulia ukajiuliza kwanini ndg zetu wenye uarobino wana uliwa na viungo kuchukuliwa?
Au huwa wanaenda kunywewa supu? ile ya kagera ambapo muhusika mmoja wapo ni padre ndo alikuwa coordinator hujapata kitu hadi sasa? Any way uko sawa julingana na imani yako. Mimi imani yangu inaniambia siku ya mwisho kwa wenye dhambi watachomwa moto wa milele na nina amini hivi wengine wanapinga siyo kweli moto haupo nao wapo sawa kama wewe.
 
Hakuna utajiri wa mambo ya kishirikina kwa sababu hayo mambo kiuhalisia, hayapo. Ni uzushi.

Haiwezekani utajiri wa hivyo uwepo halafu nchi nzima watu wake ni maskini wa kutupwa.

Sitoshangaa kabisa kama average IQ ya Watanzania ni 2.5 🤣.

Yes, single digit IQ.
 
Back
Top Bottom