Yoda
Kwa sababu umeuliza wacha leo nikuambie visa3 sio vya kuhadisiwa
Kisa cha kwanza ni babu yangu mwenyewe. yeye ni mnyantuzu alienda kwa mganga akafanyiwa yake kisha akaapiwa nakuambiwa nenda baada ya siku kadhaa atakuja mgeni mpokee kwa ku nyunyizia maziwa fresh yaani yale maziwa unayameza mdomoni kisha unayapuliza ukimpulizia huyo mgeni na muda huo hujui mgeni atakuwa aina gani.
Babu akarudi kusubiri mgeni baada ya siku 9 mchana wanamenya mihogo kwa ajiri ya udaga chatu mkubwa wakamuona anakuja nyumbani family ikatahamalaki kwa uoga na wengine kufata fimbo.
Cha ajabu babu akaagiza yafatwe maziwa na kutekeleza kama aliyoambiwa baada ya kumaliza zoezi lile nyoka alienda moja kwa moja hadi sehemu ile ya kuhifadhia nafaka ninyi waswahili mnaita stoo huku kuna majina kama ng'hunguku ama kwenye maruli.
chatu yule alikuwa na tabia ya kwenda na kurudi akirudi mifugo itazaa sana yaani kila kazi ya mwanafamilia atakayofanya
inakuwa na mafanikio tele sio kilimo wala mifugo vyote vilienda vyema.
Kuna jamaa mwingine sitataja uhusiano wake hapa ila ni ndg kabisa. kazi yake ya kuchimba dhahabu huyu jamaa alikopa hela za kutosha bank na akashindwa kurejesha jamaa akawa katika msongo mkubwa wa mawazo.ndipo akaambiwa na jamaa yake wa karibu mchimbaji wa dhdhabu vilevile akampa abc zote na kumhakikisha swala lako ni dogo sana hili iwapo upo tyr twende kwa mtaalamu. kwa sababu ya umaarufu aliokuwa nao pia kufirisiwa anaogopa aliukubali ushauri wa jamaa.
Walipo enda akapewa maelekezo yote kisha akaombwa kijana wake wa kwanza . jama hakusita na dogo akapita kushoto. Basi ukwasi ukazidi mara2 zaidi ya mwanzo tena kwa ghafla mnoo duara zake zikawa za kugusa tu anapata. mfano mwaka 2017 yeye mfuko wa mawe ya duara zake kg50 alikuwa anauza m13 wengine m1au tatu wengini ni laki7 nk.
Nikiwa kama kiongozi wa duara zake tulikuwa tunafanya makubwa sana na tukiwa ofisini kwakwe kuna mambo ya kutisha tulikuwa tunaona watu 3 tu yaani mimi yeye na mtoto wake wengine hawaoni.
mfano siku moja nikiwa mwazwilo machimboni mimi na mtoto wake tulipewa maagizo na jamaa kuwa leo mnaugeni hapa mtafanya kama nilivyo waambia. tukakubali na tukasubiria huo ugeni uje midaa kama ya saa8 mchana tuliona mnyama wa ajabu maarufu sana Tz hii kaambana na chatu mkubwa mno. baada ya kuona tuliingia ndani kufanya yetu mkitoka kule ndani wa nje hawamuoni mtafanya kila kitu lakini kamwe hawatakuona hata awe mchawi hawezi kukuona. Yule mnyama alipofika kambini akiwa na chatu na wanatembea taaratibu tukafanya kama tulivyoambiwa na kuwaruhusu warudi. Na walikuwa wanaenda kupotelea maduarani wanaishia bila kuelewa wameenda wapi.
Kitakachofuata hapo ni duara zitachanganya hadi na ninyi mnachanganyikiwa pia hela nje nje.
Huyo jamaa akao mke wa2 na hapa sasa story ya kumtoa mtoto wake wa kwanza tuliijua yule mke mkubwa alienda akiria kwa mama mkwe wake akisema hadharani "'mama unajua kabisa nilimtoa mwanangu ili tufanikiwe kimaisha na mme wangu leo tumefanikiwa kaoa mwanamke mwingine Nimemoksea nini mimi mwanao?" kama haitoshi hapo nyumbani mtoto mwingine (KE) alikuwa na kichaa na yeye kumbe kashawekwa akianza anguka ama kutoka makamasi na kufanya mambo ya ajabu ajabu.Biashara za jamaa ndo zinapamba moto sana na aliyekuwa anasimamia ni huyu mwanamke wake mkubwa mtama akaumwaga wote ndo kujua kumbe mtoto alikufa kimaajabu ajabu kumbe sababu ilikuwa ni hii.
Mimi baada kutoka machimboni nikiwa na hela kiasi chake yale mambo japo niliya zoea lakini bado yalikuwa yana nisumbua sana kichwani hata nikiwa nimelala mara napiga yowe usiku maana yalikuwa yananijia mara kwa mara.
Nilikaa na wazazi nikaawaambia yote jibu la wazazi lilikuwa ni moja tu kutoka kwa mzee KAMA UNAJUA SISI NDO TULIOKUZAA ACHANA MARA MOJA NA NDG YAKO HUYU NAWEWE ATAKUPELEKA HUKOHUKO MWISHO UTUUE.muda huo mama akilia akisema ungeliwa na yule chatu nani angetuambia?
Ya3 sitaandika zitoshe hizi tu.
Mara zote huwa nasema hapa Iwapo unaamini kabisa haya mambo hayapo yamkini uko sawa kabisa.Na yule asiye amini kuwa yapo yupo sawa vilevile.
NIMESHAOKOKA SAII MSIJE PM. BWANA ASIFIWE SANA.