Unawafundishaje Watoto wako kuhusu Athari za Unyanyasaji wa Kijinsia?

Unawafundishaje Watoto wako kuhusu Athari za Unyanyasaji wa Kijinsia?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Onyango Otieno, mwanaharakati mwenye umri wa miaka 35 kutoka Kenya, anasema kwamba wanaume wameshawishika na jamii kuamini kuwa nafasi yao ni juu ya wanawake, lakini kuongezeka kwa ufeministi kumewaacha wanaume wengi wakihisi wamedhoofika au nafasi yao kuchukuliwa na wanawake.

Anaeleza “Wanaume wengi hawakufundishwa wala kuelimishwa jinsi ya kuishi pamoja na wanawake wakiwa binadamu kama sawa,”

"Dunia imebadilika kwa njia nyingi sana. Wanaume hawajabadilika,"

Malezi kwenye Familia yako yalikufanya uone Ukatili dhidi ya Wanawake ni jambo la kawaida au yalikusaidia Mtetezi wa Haki za Wanawake na Wasichana?
 
1. Sikulelewa kuwa mtetezi wa wanawake na wasichana.

2. Nimelelewa kutoa haki kwa kila mtu bila kujali umri wake, jinsia yake, Elimu yake, rangi yake, dini yake, n.k.

3. Binadamu wote ni sawa. Kila aliye kwenye mwamvuli wangu ana uhakika wa kutendewa kwa haki bila kubaguliwa.
 
Malezi kwenye Familia yako yalikufanya uone Ukatili dhidi ya Wanawake ni jambo la kawaida au yalikusaidia Mtetezi wa Haki za Wanawake na Wasichana?
Tuachane na hii kasumba ya kutilia mkazo jinsia moja tu. Tuwalinde na unyanyasaji watoto wa jinsia zote mbili
 
Hii ni kutokana na mfumo dume ambao umeshamiri Barani Afrika.Ambapo ukiangalia makabila mengi haswa Kanda ya Maziwa makuu yanamuona Mwanamke ni kiumbe dhaifu ambaye hafai hata kushirikishwa kwenye kutoa maamuzi juu ya wanaume.Hivyo jamii nyingi humchukulia Mwanamke Kama kiumbe dhaifu ambacho hakiruhusiwi kuchangia chochote mbele ya mwanaume.Kwa mfano Nchini Tanzania,haswa jamii ya kabila la wasukuma na Wakurya Kanda ya Ziwa Mwanamke Hana hata haki ya kuchagua ampandaye kwenye suala zima la ndoa.Hata mzee Umri wa Babayako au Babuyako anakuoa chamsingi tu Wazazi wako ama Walezi wako wamekubaliana Mahali ya kutosha.
 
Jinsia ya kiume ilindwe maana ndio inabeba mbegu za kuendeleza kizazi cha wana wa adamu.

Mungu aliangamiza Mji wa Gomorrah na Sodoma kwasababu walikuwa wanataka kuangamiza jinsia ya kiume na kuuharibu ulimwengu. Bila ya wanaume huu ulimwengu ni bure
 
hivi izo haki Sawa pale kwenye katiba yetu ipi mtu kanyimwa hasa jinsia ya kike

nilimsikiliza mwanasaikolojia mmoja anasema
kizazi cha sasa hivi tunaishi Kati ya wanaume wenye misuli na wanawake ambao wamefunzwa kwamba kuna haki wamekosa ndomana ukatili siku hizi umeongozeka kusikia mtu kala kisu kisa mapenzi imekuwa kawaida
 
Suala la ukatili wa kijinsia naona kama linazidi kukita mizizi katika jamii yetu, licha ya kuwa baadhi ya familia huwafundisha watoto usawa wa jinsia zote lakini katika hili jamii za kanda ya ziwa zimebaki nyuma katika hili.

Ukatili wa kijinsia piah unachangiwa na mfumo wa nchi yetu katika wizara husika kwamfano wizara ya jinsia kila ikisimama inazungumzia suala la jinsia ya kike tu, hii inapelekea jinsia ya kiume kujiona yenye nguvu, lakini suala hili piah limepelekea jinsia ya kike kuona inalindwa sana na hivyo mda mwingine kuwa na kiburi jambo ambalo linapelekea ugomvi mkubwa katika jamii kwa jinsia hizi ambapo matokeo ya ugomvi huu hutafsiriwa kama ukatili wa kijinsia pale mmoja anaposhindwa
 
Back
Top Bottom