Unawajua watu weusi (waafrica) ndani ya bible?

Unawajua watu weusi (waafrica) ndani ya bible?

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,841
Reaction score
1,843
Kumekuwepo na mitazamo kwamba biblia inazungumzia wazungu na sisi waafrica we had nothing to do with the bible na wokovu wa wanadamu (for believers), wala bible haitutaji.

Leo nakuletea watu weusi ( waafrica) wanaotajwa ndani ya bible, na walioshiriki kujenga historia ya Israel, ukristo na umuhimu wao

1. Cush- huyu ndo chimbuko hasa la waafrica, ni mtoto wa ham, na mjukuu wa noah. Inaaminika huyu ndo babaya waafrica wote. Ethiopia wanaamini kuwa wao ni direct descendant wa cush. (Genesis 10:8; 1 Chr. 1:10)

2. Zipporah, huyu alikuwa mke wa moses,ikumbukwe kuwa baada ya moses kumuoa watu walilalamika sana mpaka Mungu akataka kuwaadhibu, kisa tu alikuwa mwafrica. Moses wote tunajua umuhimu wake katika historiaya dunia hii. (Numbers12:1)

3. Shulammite, huyu alikuwa mke wa solomoni, na inaaminika wimbo ulio bora aliandikiwa yeye. Anasifika kwa uzuri wake na ngozi yeke nyeusi nyororo. Binti huyu katuwakilisha vizuri sana waafrika mpaka kaandikiwa wimbo mzuri namna ile. (Song of Solomon 1:5),

4. Queen of sheba, huyu ni malkia aliyemtembelea Solomon ili kuhakiki hekima yake. Malkia huyu alikuwa tajiri na mwenye ukwasi wa ajabu. Katika safari yake alibeba mabag ya manukato,dhahabu, uvumba, na vito mbalimbali. Hii inatudhihirishia kuwa Africa tulikuwa vizuri kitambo sana mafisadi tu ndo wametulostisha. Ukoo wa haile selasie wanaamini kuwa wao ni wajukuu wa mfalme solomoni baada ya kuzaa na bibi yaoqueen of sheba(1 Kings 10:1)

5. Ethiopian eunuch Acts8:37, huyu alikuwa ni mlinzi wa malkia wa Ethiopia ambaye ametajwa kuwa maraika walimtuma filipo amtokee jangwani ili amfafanulie kitabu cha isaya alichokuwa akisoma wakati akisafiri kutoka Israel. Hii inatwambia kuwa kumbe hata kabla ya wamisionary maandiko yalikuwepo Africa na tulikuwa tukiyasoma vizuri tu

6. Simeon a.k.a Niger ( Acts13:1), huyu alikuwa mwafrika tena mweusi kiasi cha watu kuacha kumuita simon tu ila wakampa a.k.a ya simon "niger". Kwa wanaofahamu simeon ni kati ya watu wa kwanza kabisa kusambaza injili kwa mataifa na kuwa mkuu wa makanisa baada ya Yesu kufa. Kumbe hata sisi waafrica ni kati ya watu walioeneza wakovu sambamba na kina Paulo,silas, na wengineo.
Historia haijatuacha nyuma waafrica, tulikuwepo toka enzi za noah na tutaendelea kuwepo. Na dunia hii tumeshiriki katika kila hatua ya ujenzi na ubomozi. VIVA Afrika.
 
Hivi Waisraeli pamoja na mitume na manabii wa kwenye Biblia ni Wazungu?

asili ya watu yaweza tofautiana katika mitazamo ya jamii tofauti kutokana na nadharia inayotumiwa na jamii hiyo. Nadharia ya neno "wazungu" imetumika "kimtizamo" zaidi, iki reflect rangi na si tabaka la kigiografia.

ndo maana nimeanza na neno "kumekuwa na mtizamo".
 
sasa baba yake na huyo mkushi naye alikuwa wa ngozi nyeusi? Au ham naye alikuwa Mwafrika? Ufafanuzi kidogo tafadhali. Itakua vizuri pia tukielewa maana/tofauti ya neno chimbuko na asili. Natanguliza shukrani SONGOKA NA MAGWIJI WENGINE WA JUKWAA HILI.
 
Last edited by a moderator:
asili ya watu yaweza tofautiana katika mitazamo ya jamii tofauti kutokana na nadharia inayotumiwa na jamii hiyo. Nadharia ya neno "wazungu" imetumika "kimtizamo" zaidi, iki reflect rangi na si tabaka la kigiografia.

ndo maana nimeanza na neno "kumekuwa na mtizamo".

I love this! #Great thinker!
 
Babylon unaweza pata majibu ya hoja yako ukipita hapa
 
Last edited by a moderator:
Tutajie basi na waliopo kwenye agano jipya (new testament)
 
Hivi Waisraeli pamoja na mitume na manabii wa kwenye Biblia ni Wazungu?

Ukisoma vizuri chimbuko la hao baadhi ya hao Waisrael (Wayahudi) unapata picha kuwa kuna uwezekano baadhi yao walikuwa na muonekano wa Kiafrika haswa wa watu wa Misri (sio hawa waarabu wa kimisri ya sasa)...

Mathalani katika Biblia kuna nyakati ambapo Nabii Musa, Mtume Paulo wamefananishwa na Wamisri pamoja na kuwa wao walikuwa ni Wayahudi kwa baba na mama.
Hii inaweza kukupa ujumbe kuwa kuna uwezekano baadhi ya Wayahudi walikuwa wanafanana na Wamisri kuanzia utosini hadi unyayoni.
 
6. Simeon a.k.a Niger ( Acts13:1), huyu alikuwa mwafrika tena mweusi kiasi cha watu kuacha kumuita simon tu ila wakampa a.k.a ya simon "niger". Kwa wanaofahamu simeon ni kati ya watu wa kwanza kabisa kusambaza injili kwa mataifa na kuwa mkuu wa makanisa baada ya Yesu kufa. Kumbe hata sisi waafrica ni kati ya watu walioeneza wakovu sambamba na kina Paulo,silas, na wengineo.
Historia haijatuacha nyuma waafrica, tulikuwepo toka enzi za noah na tutaendelea kuwepo. Na dunia hii tumeshiriki katika kila hatua ya ujenzi na ubomozi. VIVA Afrika.

Je, huyu Simeoni anayetajwa hapa ndiye yule aliyeshurutishwa kumsaidia Yesu kuubeba msalaba? [Mathayo 27:32; Marko 15: 21; Luka 23:26] Tafadhali naomba ufafanuzi mkuu.
 
Good to know that you are currently undertaking a kind of medication. you thought growing a beard is wisdom and knowledge, and if so, even a goat is at once Plato
You were proven wrong in your attempt to criticize my logic after I exposed your critically flawed logic. You cannot demonstrate any problems whatsoever. You don't even attempt to after being proven wrong. You just make empty claims posturing for the audience hoping they won't notice. How cheesy.
 
Ukisoma vizuri chimbuko la hao baadhi ya hao Waisrael (Wayahudi) unapata picha kuwa kuna uwezekano baadhi yao walikuwa na muonekano wa Kiafrika haswa wa watu wa Misri (sio hawa waarabu wa kimisri ya sasa)...

Mathalani katika Biblia kuna nyakati ambapo Nabii Musa, Mtume Paulo wamefananishwa na Wamisri pamoja na kuwa wao walikuwa ni Wayahudi kwa baba na mama.
Hii inaweza kukupa ujumbe kuwa kuna uwezekano baadhi ya Wayahudi walikuwa wanafanana na Wamisri kuanzia utosini hadi unyayoni.

Vilevile angalia lugha walioongea wa yahudi.Lugha hii iko kwenye kundi la Semitic languages.Chanzo cha Semitic languages ni Ethiopia.kwa hiyo wayahudi wamwanzoni walikuwa waafrika.
 
Halafu angalia kwenye biblia linganisha Afrika imetajwa mara ngapi na linganisha ulaya nayo mara ngapi.
 
I did not give you the example, I gave you the impeccable exhibit. It can't be better than that, unless you are here to argue like non theists.

your bluffing again, I find no lucrative reasons to pursue this argument as you have chosen to restrict yourself within limited sphere of your mind. Encouraging your floating perspectives to be a concrete source for universal knowledge
 
Vilevile angalia lugha walioongea wa yahudi.Lugha hii iko kwenye kundi la Semitic languages.Chanzo cha Semitic languages ni Ethiopia.kwa hiyo wayahudi wamwanzoni walikuwa waafrika.

Sawa mchungaji, mbona yahudi weusi mkienda kwao jamaa wanawabagua sana kuzidi hata waarabu? Ina maana wamesahau kama na nyinyi ni black Jews?
 
Kitu kikubwa cha kufahamu hapa ni kuwa ukirsto ulio ingia kwetu ni ukirsto wa kizungu na umeletwa na ukoloni pamoja. Huu sio ukristo halisi na wa asili wa kiafrika

- Ukristo wa asili wa kiafirka upo kwenye nchi kama Ethiopia tangu karne nyingi kwenda nyuma hadi Enzi ya nabii Solomon na mafunzo yao si ya kumdhalilisha muafrika kama ukiristo wa kizungu ambao unatukuza wazungu na kuwaponda waafrika au watu weusi.
 
Back
Top Bottom