Kabisa mkuu ....
Kwanza inaonekana kabisa kulikuwa na tofauti kati ya Waisraeli kwa maana ya Wayahudi na Wayunani,Wayahudi walifanana na Wamisri na ndio maana hata walionekana kama wao,lakini hata Yusuph,mtoto wa Jacob nae pia alikuwa anafanana na Wamisri
Sasa ndio nilikuwa najiuliza huu mtazamo kuwa Wayahudi walikuwa ni weupe unaanzia wapi?
Lakini pia watu wanadai kuwa baba wa watu weusi ni Ham kwasababu tu alikuwa na mtoto alieitwa Kushi,lakini ukitazama Kibiblia utaona kuwa Ibrahimu hakutokana na uzao wa Hamu bali alitokana na Shemu,sasa kama ni hivyo,je ni kweli kwamba Hamu alikuwa mweusi?
Nauliza hivyo kwasababu ushahidi unaonesha Wausraeli [Musa,Yusuph,Paulo n.k] walikuwa weusi,je weusi wao waliutolea wapi kama shemu hakuwa mweusi?
Lakini pia ukisoma kuanzia Mwanzo 9 hadi 20 utaona kwamba hakuna mahali ambapo maandiko yanaelezea wale watoto na uzao wao walikuwa wanatofautiana rangi kabisa,kwa maana hii naweza kusema inawezekana watoto wa Nuhu wote walikuwa weusi na hizi rangi zilikuja kutokea baadae au baba wa watu weusi sio Hamu ni Shemu kutokana na ushahidi hu hapo juu!