Unawajua wauza chakula almaarufu "mama ntilie"?

Unawajua wauza chakula almaarufu "mama ntilie"?

strong star

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
36
Reaction score
42
Hili ni kundi la watu muhim sana katika jamii kwani ukamilisha maitaji ya wafanya kazi wengi wawapo kazini bila kwenda majumbani kwao kwa kuwapatia chakula, maji na maitaji mengine kisha kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Swali ni kwamba je unawajua watu hawa muhim sana katika ujenzi wa taifa , yafaham yafuatayo kutoka kwao na tujifunze :

Uvumilivu na juhudi .
Ukitaka kufanya kazi hii kwanza lazima uwe mvumilivu tena mwenye kujitoa kwa juhudi na maarifa yote kwani kazi yao uitaji vitu hivyo vyoye ili usonge mbele na udumu katika nafasi hiyo,itakupasa uamke mapema na uchelewe kulala ,ushughulike mchana kutwa bila kupumzika ,nakadhalika.

Kujitoa na kujituma.
watu hawa ujitoa sana katika maisha yao ya kila siku ili kufikia malengo ,iwe katika kutafuta wateja wapya , kuwapelekea wateja wao huduma,na ata pia kubuni vitu mbali mbali vitakavyo zidi kuwa vutia wateja wao.

Uchangamfu na ucheshi .
Pale anaposogea mteja eneo lao basi watu hawa ubadilika na kuwa wachangamfu zaidi na wacheshi zaidi ili kumvutia zaidi mteja na kumkalibisha kwa furaha na bashasha ata kama kuna jambo linawasumbua na kuwatesa kabla ila ubadilika kabisa na kuwa watu tofauti.

Uzalendo na jitihada.
Watu hawa imani yao kubwa ni uzalendo wao na jitihada zao katika nguvu na mda wao mwingi wanaoutoa kwenye kulijenga taifa na kutumikia wananchi walio wengi kwani hawana ubaguzi kwa mteja,wanahakikisha wanatoa huduma staiki kwa kila mteja,juhudi na jitihada zao zipo katika kazi ya mikono yao.

Pamoja na hayo yote watu hawa wazalendo na wasio kata tamaa kila hisi wanapitia changamoto nyingi kama vile :

Lugha zisizo faa ( matusi na uzalilishaji ) kutoka kwa wateja .
Wateja wao wengi ni vijana ambao wanajishughulisha na shughuli mbali mbali mtaaani hivyo mama ntilie ujikuta wakiambulia matusi na lugha zingine zisizo faa wakati mwingine ata za kuwazalilisha kabisa kutoka kwa wateja wao hasa pale wamapodai pesa za chakula na vinywaji,au wanapotoa huduma.

Wizi na dhuluma mbali mbali.
Bado mama ntilie katika kujitoa kwao kote juu ya kazi yao hii wapo baadhi ya wateja wao wengine uamuwa kuwaibia na kuwadhulum pesa zao za chakula na wengine uenda mbali zaidi ata kuwapiga kabisa .

Mfumuko wa bei za vyakula na viungo mbali mbali .
Kutokanana na bidhaa kuwa adim na ghali hivyo uwalazim mama ntilie kupambana na hali hiyo kwa kuongeza bei za chakula au kupunguza kipimo na kujikuta wakikosa wateja kwani maisha yanakuwa magum zaidi.

Kusumbuliwa na kuhalibiwa .
Watu hawa bado ukumbana na usumbufu kutoka kwa wateja, bwana na bibi afya, polisi na ata pia wanajamii juu ya biashara zao za chakula ,hivyo basi wengi wao ukwama kabisa na kukata tamaa ,mwisho kujikuta ni wamama wa nyumbani tu.

Upungufu wa mitaji na uwezeshwaji .
Wengi wao hutamani kujiendeleza zaidi katika kuuinua mitaji yao na kuifanya mighahawa yao kuwa ya adhi ya kati na zaidi ila kutokanana na upungufu wa mitaji uwezeshaji kiuchumi unawakwamisha kabisa na kuwa ndoto na kiu yao.

Pamoja na yote ayo wapo mama ntilie wanaosomesha watoto wao na kukidhi maisha yao vizuri uku wakiendeleza juhudi zao katika kulijenga taifa letu na kutimiza ndoto zao .
 
Ahsante kwa kutambua uwepo wetu,. wengine TOZ😏 imetufanya turudi wenyewe masokoni,awali tulikuwa tunaletewa eneo husika bidhaa tunalipa kwa njia ya simu,na mengineyo..,😔
ahsante sana ndugu ,MNA mchango mkubwa sana katika maendeleo ya kila siku !
 
Kweli watu wengi tunapita apo !
Pongezi za dhati kabisa kwa hawa mama ntilie, wanatusaidia saana sisi mabachela wavivu wa kujipikia na kiosha vyombo..

Ukijiongeza kidogo (mbinu za kivita) ukawa ni lemubebez wako unajikuta unakula pishi na mpishi kiulaini.. Unapata special treatment, msosi wa nguuvu.. We kazi yako mtaji ukipungua unamuongezea. [emoji23]
 
🤪🤪Sio wachoyo ukila chakula cha kwanza wanakupa na chakula kingine kitamu zaidi🏃🏃🏃
 
Big up kwa mama Kashinje pale five doors Kakola Kahama 1999...💪
 
Pongezi za dhati kabisa kwa hawa mama ntilie, wanatusaidia saana sisi mabachela wavivu wa kujipikia na kiosha vyombo..

Ukijiongeza kidogo (mbinu za kivita) ukawa ni lemubebez wako unajikuta unakula pishi na mpishi kiulaini.. Unapata special treatment, msosi wa nguuvu.. We kazi yako mtaji ukipungua unamuongezea.
emoji23.png
Duuuuh hatari
mama lishe ndio jina sahihi la kiswahili
Wengine ata hawatupi lishe wanatupa makapi tu ,! Wanakaanga sana .
 
Ili kuonesha support Leo breakfast mpaka dinner ni huko.

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu walinde kina mama wote.
 
Wanalogana hao mama lishe aswa ukanda huu wa tabora, shinyanga, mpanda na kigoma Kama hauko fiti utajikuta unauza sahani 1 ktk sahani 100
 
Back
Top Bottom