musicarlito
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 368
- 556
Wengi mpaka hapa tulipo leo kwenye maofisi yaliyo kwenye floor ya ngapi sijui nini tower...kuna watu a tulishirikiana au walitusaidia kama si fedha basi hata ule mchango wa mawazo lakini na kampani kiaina kuwa na amani
Wengine ilivyompendeza Mungu ni tumewaacha vijijini...wengine bado wamepigika mtaani ...je! huwa tukikutana nao tuna wa-avoid/kimbia au tunahisi ni watu wa kututia aibu?
Wengine hutusogelea karibu hata kutoka safari za mbali kutoka vijijini kuja kutusalimia...ndio ..bado wanauthamini muda wa thamani tuliokua nao ambao haukuwekewa madaraja ya elimu kama digrii au dini na ustaarabu wa kigeni...lakini wakitukaribia ama maofisini au majumbani kwetu hudhani wamefuata pesa au fahari zetu...kwa ujinga huwa hatuwapi muda huo...si ajabu ukasikia mtu anampeleka ndugu yake toka kijijini au anamtafutia kampani ya kiduka cha jirani kuwa akihitaji chochote kwa maana ya kinywaji au pesa achukue hapo...na yeye kuzuga kuwa yuko busy na shughuli za kiofisi au kibiashara ...hali anamsema vibaya huyo ndugu au mshikaji kwenye vijiwe anavyodhani kuwa ni levo yako
Ustaarabu ni kuthamini Utu...madaraja kama elimu,madaraka au hadhi fulani ni mpango wa Mungu tuu kuratibisha ulimwengu wetu na kuufanya uwe mahali petu pazuri pa kuishi...lakini kiukweli hayamaanishi chochote katika kuwako madaraja ya Utu...binadamu wote ni sawa.