CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Katika biashara kuna mambo mengi sana ya kufanya ili uweze kufanikiwa na kufika sehemu ukaona faida ya biashara,Katika mambo mengi kuna moja ambalo wafanyabiashara wengi hawalitambui na wachache sana wanaolifhamu na kwa uchache wao wanafaidika na kukaa kimya.
Mimi kazi yangu kila siku nikuwafungulia watu code ambazo walikua hawazifahamu ili kila mtu afurahie biashara yake na kuipenda.
Umeshawahi kukaa katika story na wenzako mkawa mnasimuliana namna Vitu vya pale M/city vilivyo ghali na gharama? unaona namna mnavyosapotiana na kukubali kweli mlimani kunauzwa vitu expensive na wengi wanunuaji wa pale ni watu expensive pia...!!
Sasa leo acha nikwambie,hivi hauna watu unaowajua wakawaida kabisa hanunui kitu chake chochote cha electronic nnje ya m/city? unahisi ana hela sana eeeh? Jibu ni HAPANA...
TV unayouziwa wewe 650,000 inch 32, mwenzako anauziwa TV hiyo hiyo kwa 450,000 na hata ukiingia hilo duka utakuta tv imebandikwa 650,000 price lakini mwenzako ananunua kwa 450k or lower zaidi...
KWANINI?
Wafanyabiashara wengi (wakubwa) humthamini mteja wa mara kwa mara yani yule mteja wa kila siku kuliko yule mteja mpita njia,kwasababu akimuuzia kitu leo baada ya wiki atarudi kununua kitu kingine na kingine na kingine kwa hiyo huyu mteja ameshajulikana hivyo bei ya vitu vyote kwenye duka husika ananunua kwa bei ndogo sana sana wakati mwingine hadi n kukopeshwa juu.
Wewe ukienda pale mlimani leo SURA mpya,umeenda kwasababu unataka TV hauna kawaida ya kwenda ukifika pale utatandikwa bei na watu wako serious,ukinunua sawa usiponunua sawa! WHY! sio kwamba hawakujali ila wanakujua wewe ni mpita njia, hivyo wateja "wapita njia" wapya ndio hutufanya tuishi hapa mjini,kwasababu bidhaa ya 100 nitamuuzia 200 najua hatorudi,incase akirudi nikimkumbuka nitamuuzia bidhaa ile ile kwa 150, akirudi na tena nitamuuzia 130 ikitokea akarudi tena Basi atakua automaticaly kaingia kwenye kundi la "wateja wangu" hivyo atapata bidhaaa kwa sh 100 bei ninayowauzia wateja wenyeji.
Tunawapenda wateja wazawa/wenyeji kwasababu hutufanya biashara zetu zisife zisonge mbele siku zote tuwe kwenye CHAT kwasababu ni mteja wa mara kwa mara.
Tunawahitaji wateja wapya/wageni/wapita njia sana kwasababu wao ndio hutupa jeuri ya kuishi mjini maana bei ninayomuuzia mpita njia Friji la 250,000 nitamuuzia 500,000 nitapata faida mara dufu pesa itanipa jeuri ya kufanya mabadiliko katika maisha yangu. Tofauti na mteja mwenyeji Friji nitamuuzia ile ile bei elekezi 250k nitapata faida kdgo sana tofauti na mteja mpita njia.
Kwahiyo katika Biashara yako hakikisha sana unamjua mteja wako (wa kila siku) na kuwatambua Wageni (wapita njia) maana usipofanikisha hili Biashara utafanya lakini hautofanikiwa kwa kiwango cha wenzako.
Biashara yoyote ili ikutoe ni lazima ujue kuchuja wateja,ujue wateja wa kukuimarisha biashara yako ni wapi, na wateja wakukupa pesa ya kutamba Mjini ni wapi.
Kariakoo ukienda kuna maduka ukiingia anakutajia bei kubwa wakat ulielekezwa na mtu uende duka hilo hilo,lakini kwasababu HUJULIKANI (wewe ni mpita njia) unatandikwa bei, sio kosa lao hiyo ndio PRINCIPLE ya biashara.
Ukikaa duka hilo hilo ukampigia simu aliekuelekeza ukamwambia mbona wamenitajia bei tofauti nauliyoniambia,atakwambia Mpe simu uliemkuta DUKANI ukishatoa simu kwa mtu wa dukani,wakishaongea Utashangaa unapewa bidhaa ilele uliyotajiwa bei kubwa mara 3 ila utapewa kwa bei ndogo kama rafiki yako alivyokuelekeza.
Kumbe tunaona biashara yeyote ili ufanikiwe ni lazima ujue kuwachuja wateja ujue ni wapi wa kuwashikilia na wapi wa kukupa pesa za wewe ku move na kwnda mbali zaidi.
Usikubali kufanya biashara ukawa na bei sawa kwa wateja wote,hutokaa ufanikiwe wala uifurahie biashara yako ng'o, Ukitaka kuona utamu wa biashara siku nunua kitu kwa 5000 kiuze kwa 20,000 hapo ndio utajua kumbe Bashara inalipa kiasi hiki.
Fanya hivyo ili ufurahie biashara yako,wateja wapo wengi lakini kuna namna yakupata hela kutoka kwa hao hao wateja Upo katika biashara Discount and Equality kwa wateja wako haitokufikisha mbali utacheza dance dance mwisho useme biashara mbaya,kumbe unakosea mwenyewe.
Hapo Mjini Jamuhuri ya Kariakoo Kuna watu wapo Dukani wanahitaji Mteja mmoja tu (mpita njia) anyooshwe Afunge hesabu akisubiri wateja wake wa "palilia mtaji", Pita pale china Plaza wanapouza mafriji,pita maduka ya simu uone utavyokua unaitwa kama vile wanakujua.
Kumbe wanachohitaji ni mteja mmoja tu,maana mteja huyo ndie ataetoa hela ya yeye kula,hela ya kodi ya siku,hela ya matumizi ya umeme,nk halafu wale wateja "wenyeji" wale hela yao ni ya kurudshia mtaji usiyumbe, maana wao faida yao huwa ni ndogo mnooo,ila tunai hitaji sana faida yao ndogo maana ni ya mara kwa mara.
Natamani niandike zaidi lakini kama mtu haelewi ni haelewi ila kama ni wa kuelewa nadhani mpka hapa inatosha,Usifanye biashara kimazoea Hakkisha biashara yako inakulipa.
Watambue Wateja wako,Usiwalegezee kamba wapita njia "ndio maisha yako hao"...
CONTROLA 2023