Unaweza kudhibiti hasira mtu akifanya usichopenda?

Unaweza kudhibiti hasira mtu akifanya usichopenda?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Salaam!

Nakumbuka kuna msemo unasema usifanye au chukua maamuzi katika hali 3. Hasira, furaha na huzuni. Juzi ilinitokea moja ya tukio ambalo limenifanya niwe na hasira hadi hivi leo. Naomba nijue unawezaje kufanya maamuzi ukiwa katika furaha au huzuni? Unaweza kujizuia?
 
MSAMAHA maana tafsiri sahihi ya hasira ni kosa analokufanyia MTU Mwingine ila Adhabu unajipa wewe

So Upatapo hisia za hasira anza na kuachilia MSAMAHA na kushukuru ukifanya hivyo utaendelea kuishi Maisha Furaha amani na upendo na hii ndo siri
ahsante ila naamini inatk muda zaidi.
 
Ntaanza kwa mfano wa fire triangle.

1698223196206.png

Ili moto uwake, kunahitajika vitu vitatu; oksijeni, mafuta na joto. Moto ukiwa unawaka, ukiondo kimoja wapo katika hivyo vitatu moto utazima.

Sasa, kwenye hasira, kuna aliyekuudhi, mazingira uliyopo na wewe uliyeudhika. Kikiondoka chochote katika hayo, hasira zako hazitakufanya ufanye maamuzi ya ajabu, hivyo basi njia mojawapo ya kudhibiti hasira zako ni kuondoka eneo ulilopatia hasira au muondoe aliyekuudhi. Time heals. Unapokuwa mbali na mazingira yale au na mtu yule aliyekuudhi, huwazi uliyokuwa unataka kuyafanya kwa wakati ule kwa namna ile.
 
Inashauriwa usifanye maamuzi makubwa wakati unapokuwa katika hali ya furaha, huzuni, au hasira kwa sababu hisia hizo zinaweza kusababisha upendeleo na kutokuwa na utulivu katika maamuzi yako.

Furaha inaweza kukufanya uchague chaguo lenye hatari bila kufikiria vizuri, huzuni inaweza kusababisha maamuzi ya kukosa matumaini, na hasira inaweza kufanya uchukue hatua isiyo na busara.

Ni muhimu kupumzika na kutulia ili kufikiria kwa kina na kufanya maamuzi sahihi.
Fanya maauzi yako ukiwa katika hali yako ya kawaida maana.
 
Hiyo ni kanuni inaitwa the power of Gratitude kuwa mtu wa kushukuru ur life will change completely tumia hiyo mbinu utaona hata maadui zako wanaelekeza silaha zao katika kukulinda badala ya kukudhuru
dah ngumu sna.
 
Inashauriwa usifanye maamuzi makubwa wakati unapokuwa katika hali ya furaha, huzuni, au hasira kwa sababu hisia hizo zinaweza kusababisha upendeleo na kutokuwa na utulivu katika maamuzi yako.

Furaha inaweza kukufanya uchague chaguo lenye hatari bila kufikiria vizuri, huzuni inaweza kusababisha maamuzi ya kukosa matumaini, na hasira inaweza kufanya uchukue hatua isiyo na busara.

Ni muhimu kupumzika na kutulia ili kufikiria kwa kina na kufanya maamuzi sahihi.
Fanya maauzi yako ukiwa katika hali yako ya kawaida maana.
Kwenye case amby maamuzi yote ni mabaya je?
 
IKitokea case ambpo maamuzi yote unayochukua ni mabaya?
Tuliza akili. Hakuna maamuzi mabaya. Sema maamuzi uliyoyachukua yanaweza yasilete matokeo uliyoyategemea kwa wakati ule. Na maamuzi mengi mabovu yanafanywa katika hali hizo zilizokatazwa.
Muhimu ni kutuliza akili wakati wa maamuzi na usifanye mhemko.
 
MSAMAHA maana tafsiri sahihi ya hasira ni kosa analokufanyia MTU Mwingine ila Adhabu unajipa wewe

So Upatapo hisia za hasira anza na kuachilia MSAMAHA na kushukuru ukifanya hivyo utaendelea kuishi Maisha Furaha amani na upendo na hii ndo siri
Sio kila anaekasirika ana kinyongo,au hawezi kusamehe,hasira ni hisia inayokuja auotomatically baada ya kuudhiwa kitu ambacho huwezi kujizuia, cha muhimu hapa ni kuto kukaa na hiyo hasira kwa muda mrefu, kwani mwisho wa siku itakusababisha uwe na chuki amabayo itakayokufanya sasa uwe na kinyongo,na hapa sasa ndio utahitajika kusamehe, maana kumuweka moyoni mtu aliyekuudhi kwa muda mrefu itakuletea madhara ya kimwili na kiroho.
 
Back
Top Bottom