Unaweza kuoa/ kuolewa ama kuwa na mahusiano na ex wa rafiki yako?

Unaweza kuoa/ kuolewa ama kuwa na mahusiano na ex wa rafiki yako?

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
1,889
Reaction score
3,059
Nauliza kama hili linawezekana nijilipue naona usingle utanifanya maisha niyaone magumu zaidi with ziro sms, call zaidi ya huduma kwa wateja

Ni hivi wakati nasoma miaka hiyo nipo kidato cha pili kuna kijana alihamia shuleni kwetu tukazoeana alikuwa kabila moja na mama yangu hivyo nikamchukulia kama ndugu,, yeye ni mkubwa kwangu kwa miaka 3 so now yupo na 28

Sasa yule kaka alinitongoza kipindi hicho hata sielewi mambo ya dunia kiufupi nikamkataa so akabaki rafiki tu..Tumeenda mpk kidato cha 3 kuna binti akahamia tukawa marafiki basi huyo kijana tumwite G akamtongoza rafiki yangu akaja kuniambia nikamwambia tu amkubali maana alishawahi kunitongoza ila nilimkataa basi wakakubaliana wakaanza mahusiano, tulipoingia kidato cha 4 wakaachana kila mtu akawa na mahusiano yake mengine

Sasa ni miaka 8 imepita huyo kijana G tumekutana tena kwa namna tofauti kila mtu ana maisha yake,, alienda moja kwa moja kuwa ananihitaji ikiwezekana tuanzishe famillia[emoji846]

Nawaza hapa inawezekana kweli maana alidate na rafiki yangu ( japo hawakukulana hii alinambia rafiki yangu mwenyewe zamani na hata G mwenyewe nilimuuliza akasema hakuwai kulala nae maana ulikuwa ni utoto tu sina uhakika na hili)

Huyu rafiki yangu navowaambia ni mabest mpk sasa tumesoma wote shule zote mpk chuo tumemaliza chuo kimoja, kwa sasa yeye alishazalishwa na mwanaume mwingine ndio yupo nae

Ni rafiki yangu tunaambiana mambo mengi japo kwa sasa mawasiliano sio sana kwa vile tumeshakuwa na maisha tofauti yeye ana mtoto mimi sina kwaiyo sio kama zamani tukiwa wote bilabila

Vipi kama atagundua nina mahusiano na ex wake haitoleta chuki kweli??

Je kuna ubaya wowote nikifanya maamuzi ya kuwa na G

Naomba ushauri kwa wale waliowahi kuwa na mahusiano
Na ex za rafiki zao na wengineo
 
Binafsi sioni kama Kuna shida kwa sababu ni ex wake, ingekuwa ni boy friends wake au mzazi mwenzake isingefaa
Lakini ni ex wake kama mmeridhiana na mnapendana fanyeni tu maamuzi sahihi
Maadamu humkosei mungu Wala kuvunja Sheria
Rafiki yangu hatonimind na kuvunja urafiki
Maana ni rafiki yangu pete na kidole anajua mambo yangu mengi na yake nayajua haitoleta shida
 
Binafsi sioni kama Kuna shida kwa sababu ni ex wake, ingekuwa ni boy friends wake au mzazi mwenzake isingefaa
Lakini ni ex wake kama mmeridhiana na mnapendana fanyeni tu maamuzi sahihi
Maadamu humkosei mungu Wala kuvunja Sheria

[emoji846] sawa best
 
Kifupi mtapitiwa wote na kuolewa mtakusikia tu. Anataka kukutumia ww km chambo kumrusha ex wake Roho Shtuka

Miaka 8 imeshapita ndugu sio kwamba wameachana juzi.. and so hawakudate muda mrefu na hiyo kidato cha 3 so almost miaka9 sasa hapo anamrusha ex wale roho kivipi ndugu yangu

Na ex wake ana mtoto kazaa na mtu mwingine ambae walikutana chuoni
 
Kuna rafiki yangu mmoja wa karibu nili gundua ana mtongoza alie kua X wangu, Nili shangaa sana like WTF dude
 
Kuna rafiki yangu mmoja wa karibu nili gundua ana mtongoza alie kua X wangu, Nili shangaa sana like WTF dude

Ex wako wa muda gani utotoni au ukubwani?

Na mliachana kwa kipindi cha muda gani mpk rafiki yako kumtaka ?

Je ulijisikiaje baada ya kujua?

Vipi kuna ubaya wowote ikiwa wewe umesha move on labda umeoa tayari una familia yako na rafiki yako akataka kumuoa huyo ex ?
 
Namuonea huruma huyo kijana. Inaonesha unataka kuolewa kisa tu umechoka kua single na unaona muda unaenda ila sio kwamba umempenda kwa dhati huyo kijana.
 
Namuonea huruma huyo kijana. Inaonesha unataka kuolewa kisa tu umechoka kua single na unaona muda unaenda ila sio kwamba umempenda kwa dhati huyo kijana.

Sasa kwani wanawake tunapenda basi… inachukua muda mrefu kumpenda mtu, Kaka mapenzi sio ya siku moja ni mlolongo mpk nikubali kuwa nae nina uhakika atanifanya nimpende hapo baadae
 
Back
Top Bottom