Unaweza kuoa mke mwenye sura Personal na akakupasua kichwa tuu!

Ubaya am uzuri wa kimuonekano kwa upande wako unaupima kwa vigezo gani?

Uzuri kigezo chake kikuu ni mvuto wa macho, kusikia na kunusa. Mtu mwenye mwonekano wa kuvutia huhusishwa na uzuri.

Wapo Watu na viumbe wanaovutia zaidi(Wazuri) kwa kuwatazama, kusikia sauti zao au harufu zao. Huo ndio uzuri.

Mengine ni faraja tuu
 
Inawezekana mkuu , ila kwa sasa mwanamke mzuri ni anae leta wazo la ugali unafikaje mezani mkuu , Figo zikishafeli ata uzuri wa sura huta uona mkuu.

Huo ni uzuri wa kimawazo Mkuu.
Mimi nazungumzia uzuri wa maumbile na mwonekano.

Ugonjwa ni matatizo na haiwezi kuwa excuse ya uzuri.

Ni sawa na useme Mwenye nguvu za kimaumbile na asiye na nguvu. Hizo ni sifa lazima tuwe na tabia ya kukubali ukweli na uhalisia
 
Uzuri kigezo chake kikuu ni mvuto wa macho, kusikia na kunusa. Mtu mwenye mwonekano wa kuvutia huhusishwa na uzuri.

Wapo Watu na viumbe wanaovutia zaidi(Wazuri) kwa kuwatazama, kusikia sauti zao au harufu zao. Huo ndio uzuri.

Mengine ni faraja tuu
Sawa.huo ni mtazamo wako na upande wako.una hakika unachokiita kibaya kinaweza kuwa kibaya kwa mwingine?
Acha hii mitazamo ya kitoto.kila mtu ameumbwa katika namna yake njema.huyu yuko hivi,huyu yuko vile.kila kitu ni chema hakuna ubaya.

Nyie ndo wale hata kichanga kikizaliwa mnakiita kibaya.

Kua na uachie huu upuuzi watoto
 
Tatzo kila mtu ana jicho lake mkuu sidhani kama kuna uzuri wa General.
 

Hatuzungumzii mtazamo tunazungumzia uhalisia.

Unachojaribu kukieleza hapo ndio upuuzi kwa sababu unaukataa ukweli.
Mungu kila kitu kikiwa chema kulingana na matumizi yake. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa katika hivyo vitu vyema kuna vizuri na vîbaya.

Ukishasema kuna kitu kizuri basi elewa umetamka kuwa kuna kitu kibaya. Ukishasema kuna Watu wazuri wa sura basi elewa kuwa umetamka kuna wabaya wa sura.

Ukishasema kuna Watu wenye tabia mbaya elewa automatically umesema kuna wenye tabia nzuri.

Lakini vyote ni vyema kwa sababu vina matumizi.

Ninyi ndio mnaotaka kuleta Unafiki kwa kuukataa Ukweli.

Uache utoto wa kujidanganya, na kuukimbia ukweli.

Wazuri wapo na wabaya wapo. Ila wote ni muhimu kwa sababu kila mmoja anamatumizi yake.
 
Tatzo kila mtu ana jicho lake mkuu sidhani kama kuna uzuri wa General.

Unajaribu kusema hakuna uzuri wala ubaya.

Kitu kizuri ni kizuri tuu.
Na kitu kibaya ni kibaya. Hapa tunazungumzia mvuto.
Wewe unazungumzia kupenda.

Upendo ndio unaweza ukakufanya ukaona kitu kibaya ni kizuri. Na chuki inaweza kukufanya ukaona kitu kizuri ni kibaya.

Ila Akili itakufanya uone kitu kizuri ni kizuri na kibaya ni kibaya.
 
Taikon vipi? Mbona umechafukwa sana leo? Shemeji amekutenda? Pole, na asante kwa nondo.

Mwanaume ni kujiamini. Huwa ninashangaa wanaume wanapoomba samahani kwa wake zao. Eti baby samahani sitachepuka tena. Ilikuwa bahati mbaya. Basi mkewe anavimba kichwa na kufunga begi.

Mara unaenda kwa washenga kuomba msaada wa upatanisho. Hivi wewe ni mwanaume au bwege?

Pamoja Taikon

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 

Mimi nashangaa jambo moja. Kuna Watu wanakiri kuwa kuna Watu wazuri alafu muda huohuo wanakataa hakuna Watu Wabaya.

Wanashindwa kuelewa kuwa mpaka useme uzuri ujue umeutofautisha na ubaya
 
Ni kwel kabisa mkuu , naunga hoja yako 💯%
 
Ni kwel kabisa mkuu , naunga hoja yako 💯%

Ukiambiwa utaje ndege wazuri sio ajabu Watu wengi duniani wakamtaja Tausi na njiwa.
Lakini ni nadra sana kusikia mtu akikutajia bundi.

Haya tukirudi kwenye jamii moja. Kwa mfano kwenye Kuku.
Yapo majogoo mazuri ukiyatazama hivi unasema hili jogoo ni zuri sana.

Lakini ukija kwa binadamu Watu wanaogopa kusema ukweli kwa sababu fulanifulani, ikiwemo kutokuumiza hisia za wale wenye muonekano usiovutia(ambapo maana yake ni wabaya).

Ni kweli kila kitu ni chema kwa sababu kinamatumizi yake.

Mfano Watu wenye sura za kazi Wana role zao hasa role za mamlaka, jeshini, utawala, kutisha na kutiisha jambo.

Lakini huwezi kumleta mtu mwenye sura ya kazi ati awe mshehereshaji au shughuli za fasheni, huo ni uongo.
 
Hii ni kwel kabisa mkuu, kutokuumiza hisia za mwengne ata kama kuna ukweli ni hekima kubwa sana.
 
Hii ni kwel kabisa mkuu, kutokuumiza hisia za mwengne ata kama kuna ukweli ni hekima kubwa sana.

Na hakuna hiyo sababu.
Ila ni vizuri kila mtu kujitambua na kujikubali jinsi alivyo.
Unaweza usiwe mzuri kwenye mvuto wa kimapenzi na kingono lakini ukawa nzuri kwenye sekta zingine kama utafutaji wa mali na biashara.
 
Na hakuna hiyo sababu.
Ila ni vizuri kila mtu kujitambua na kujikubali jinsi alivyo.
Unaweza usiwe mzuri kwenye mvuto wa kimapenzi na kingono lakini ukawa nzuri kwenye sekta zingine kama utafutaji wa mali na biashara.
Sure mkuu.
 
Katika macho yangu haya ya nyama bado sijafanikiwa kuona mwanamke mbaya wa sura , ukiona nimesema wapo wabaya ni
kufuata mkumbo tu .

HAYA MAMBO YAPO KIMTINDO SANA UNAWEZA KUONA UNA MWANAMKE MZURI ILA MBELE YA MACHO YA MWINGNE NI WAKAWAIDA SANA.
Beauty falls in the eyes of the beholder
 
Mkuu huu Uzi ungenoga zaidi Kama ungeambatanisha na kapicha,ila bado hakujaharibika Jambo.
 
Hahahaaaaaa..Yaan tuna tabia za kufanana..Nakukubali sana kaka angu..Big u..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…