Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Dunia hii imejaa mambo mengi sana, ukiachana na watumishi ambao wanalipwa mshahara kwa mfanyabiashara yoyote unaweza kutoboa na biashara ikawa kubwa bila kuroga? Au kusali sana?
Vijana wengi naona hatutoboi maana haturogi Wala hatusali spiritual tuko naked sana, nimeenda kukodi shamba huku kigoma story za watu zimeninyong'onyesha sana, nimeambiwa bila kuroga sitoboi nikijiangalia kwa mganga Sijawahi kwenda, kanisani naenda Imani kwa Mungu hipo, Lakini madhambi pia nafanya.
Watu wanaroga Kila sehemu iwe biashara kubwa (kariakoo) au wauza vitunguu (ilala)...tena kama wafanyabiashara sokoni ndio usiseme, niliwahi kupeleka gunia langu la dagaa wa bukoba Hapo mabibo likabadilika rangi na kua jekundu nikatamani nikimbiie niliache, wateja hawaonekani. Nikaanza kuuza vitunguu vikaanza kunyauka na kuoza wakati mwenzangu anamaliza kwa siku moja, nikaviacha.
Tuambizane ukweli Kuna mtu humu amefanikiwa kukuza biashara bila kua na power yoyote ile? Kwa Mungu au kwa shetani?