Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Ukweli ni kuwa CCM ipo ilipo kwa sababu ya vyombo vya dola. Na endapo leo hii vyombo hivi vikisema hatuiungi mkono tena CCM huo ndio utakuwa mwisho wa CCM kuongoza Tanzania.
Kwa upande wa vyama mbadala ni chama kimoja tu ambacho kwa muda mrefu sasa kimeweza kuonekana kuwa ndo mbadala sahihi wa chama cha mapinduzi. Chama hicho ni CHADEMA.
Kuonekana kwa Chadema kama chama mbadala kwa CCM hakujatokea kwa bahati mbaya ila ni kwa sababu ya consistency yake katika kusimamia ukweli hasa kuwa na hoja mbadala ambazo kwa kipindi kirefu zimeonekana kuwatetea watanzania na kuonekana ndizo zinaweza kuwafikisha katika maendeleo ya kweli.
Pamoja na kuwekewa mizengwe na CCM ikiwemo kutengenezewa mamluki, CHADEMA kimesimama sana kwenye reli yake. Hakijaweza kutetereka kama chama.
Sehemu kubwa zaidi ambayo CHADEMA wanaweza kuiteka mioyo ya Watanzania na kuzishinda kabisa hila za CCM na vyombo vyake ni kwenye uchaguzi huu wa Mwenyekiti wa chama chao.
Hii ni kwa sababu pamoja na kuwa na hoja nzuri kwa Watanzania sehemu ambayo CCM wameweza kuwalaghai Watanzania juu ya ubaya wa CHADEMA ni kuhusu Mwenyekiti wao kuwa wa kudumu na asiye na mbadala. Hoja hii imekuwa ikitumiwa na CCM kuwashawishi Watanzania kuwa CHADEMA sio chama kizuri, ni chama cha ukoo fulani na cha watu fulani.
Endapo CHADEMA itafanikiwa kukamilisha uchaguzi huu kwa TUNDU LISSU kushinda nina uhakika suala hili litabadili fikra potofu waliyoweza kuijengwa CCM kwa Watanzania na hatimaye CHADEMA kujisimika rasmi kuwa chama pekee mbadala kwa Watanzania.
Hongereni Chadema kwa kuonesha kuwa chama chenu kina demokrasia. Fanyeni uchaguzi wenu mkijua kuwa huu ndo wakati pekee mlionao wa kuziteka nyoyo za Watanzania. Jueni tu endapo TUNDU LISSU akishinda uchaguzi huu, hii ndo itakuwa game changer kwenye siasa za Tanzania. Hii ni kwa sababu, mwanasiasa pekee anayeaminika na Watanzania wengi kwa sasa kuanzia wa Serikalini, Sekta binafsi, Vijana na watu wa kawaida kabisa ni TUNDU ANTIPASS LISSU.