Freelancer
JF-Expert Member
- Sep 22, 2008
- 2,965
- 2,147
Hili swali litaonekana la kizushi kwa baadhi ya watu. Ila nataka kujua more details kuhusu hii makitu maana imeshakuwa ni industry sasa. Kuna watu wanatengeza hela kwenye vyakula, kuna watu wanangeneza hela kwa kumiliki ukumbi, na kuna watu wanatengeneza hela kwa kukodisha magari. Nataka ku approximate hii industry ina worth kiasi gani? najua kuna watu waliokosa akili watakuja hapa na kuuliza ili iweje? Naomba tuwe wastaarabu. Kama huna jibu la kunipa ni mara kumi ukakaa kimya maana sijaanzisha hii post kwa ajili ya watu wenye mizaha au akili ndogo. Kama mtu anajua ukumbi fulani anaweza akataja huo ukumbi na ku approximate sherehe ngapi zinafanyika in a week. Mi nitaangalia namba ya kumbi zilizotajwa na namba ya sherehe kwa ujumla. unaweza taja kwenye mkoa unaoishii tu si lazima Tanzania nzima. Asanteni.