Unaweza ukakisia ni sherehe ngapi za harusi zinafanyika Tanzania kwa wiki

Unaweza ukakisia ni sherehe ngapi za harusi zinafanyika Tanzania kwa wiki

Freelancer

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
2,965
Reaction score
2,147
Hili swali litaonekana la kizushi kwa baadhi ya watu. Ila nataka kujua more details kuhusu hii makitu maana imeshakuwa ni industry sasa. Kuna watu wanatengeza hela kwenye vyakula, kuna watu wanangeneza hela kwa kumiliki ukumbi, na kuna watu wanatengeneza hela kwa kukodisha magari. Nataka ku approximate hii industry ina worth kiasi gani? najua kuna watu waliokosa akili watakuja hapa na kuuliza ili iweje? Naomba tuwe wastaarabu. Kama huna jibu la kunipa ni mara kumi ukakaa kimya maana sijaanzisha hii post kwa ajili ya watu wenye mizaha au akili ndogo. Kama mtu anajua ukumbi fulani anaweza akataja huo ukumbi na ku approximate sherehe ngapi zinafanyika in a week. Mi nitaangalia namba ya kumbi zilizotajwa na namba ya sherehe kwa ujumla. unaweza taja kwenye mkoa unaoishii tu si lazima Tanzania nzima. Asanteni.
 
ni billions ya TZS!, mi sina matatizo na kufunga harusi ya kifahari, tatizo langu ni KULAZIMISHANA KUCHANGA MICHANGO, MIJITU MIZIMA na IMESOMA MPAKA UNIVERSITY, ANAAMUA KUWA ADUI NA HATA KUVUNJA URAFIKI, kwa sababu tu haukuweza kumchangia harusi!
 
Kuna mtu mmoja anaheshimika sana ktk nji hii, kwa kuwa huwa ni mchambuzi mzuri wa issue za uchumi na siasa katika Runinga (tulisoma wote kwenye zile shule za wilaya/mkoa). Ameamua kuwa adui yangu, nikimpigia simu hapokei kwa kuwa sikumchangia harusi yake! he was the best of my best friends, ningeweza kumchangia lakini sikuwa na feza hata ya kujikimu mimi mwenyewe.
 
ni billions ya TZS!, mi sina matatizo na kufunga harusi ya kifahari, tatizo langu ni KULAZIMISHANA KUCHANGA MICHANGO, MIJITU MIZIMA na IMESOMA MPAKA UNIVERSITY, ANAAMUA KUWA ADUI NA HATA KUVUNJA URAFIKI, kwa sababu tu haukuweza kumchangia harusi!
Naomba nitajie kumbi unazozifahamu vizuri na how many weddings zinafanyika zinafanyika katika hizo kumbi. Zile ambazo upo na uhakika zaidi. Labda ni karibu na maeneo unayoishi. Mambo ya michango yataisha tu. Ila industry itaendelea kuwepo.
 
Mkuu mi nakaa kijijini, huku hakuna kumbi, ila watu wa mjini wakiwa na namba yako ya simu inatosha kukuharasi na michango yao, wanakutaarifu eti umeteuliwa kuwa ktk kamati ya maandalizi, kikao cha kwanza wanakupigia cm huku wameweka loud speaker ili ufanye pledge kila mtu asikie.
 
Back
Top Bottom