Unawezaje kufanikiwa bila nguvu ya ziada nyuma yako?

engijape

Senior Member
Joined
Nov 8, 2014
Posts
178
Reaction score
97
Ndugu zangu nimekuwa natafakari sana kuhusu nguvu nyingine nje ya Mungu inayoweza kumpa mtu mafanikio bila kumtegemea Mungu ambaye mimi namtumikia kama mkristo. Hii nguvu ikoje, kuna mtu sio mkristo, siyo Muislam, ni mpagani na asiyeenda kwa yale miungu mingine, anafanikiwa ama hafanikiwi. Na je siwezi kuamini mimi mwenyewe na nikafanikiwa bila hiyo nguvu? unaweza ukawaza kwanini nimemtenga Mungu. Ni kwa sababu namwogopa sana huyu Mungu ambao wakati nasoma Philosophy walimwita supernatural power. Ina nguvu kuliko kitu chochote kile.

Sasa basi kama siwezi kumjadili Mungu kama mkristo, naomba usipate shida wewe jadili ninachotak kufahamu kuhusu nguvu ya mafanio bila kutegemea chochote.

Asante.
 
Tusaidiane hapooo
 
ukweli ambao wengi hawapendi tuujue ni.

Mungu hapatani na utajiri,maana asili yake ni uchoyo na ubinafsi.kwahiyo unapoomba kwake utajiri yafaa ujue unaomba kitu asichotaka uwe nacho.

chunguza mkuu,watu wanasali,wanakesha wakiomba mafanikio ya kipesa na mali ila chaliii,wakiacha na kwenda kwa wataalamu wa kimila wanapewa codes,ndani ya mwaka tu mambo ni fire

kwenye mali na utajiri ndiko huko yupo shetani na nduguze,wewe wa Mungu utaambulia makwenzi ya haja.
 
Naomba unifafanulie pale shetani alipomuonesha na kumwambia Yesu '' Mali na Fahari zote duniani nimepewa mimi, nitakupa hivi vyote ukinisujudia ", je Mungu amempa utajiri shetani ?, maana yake Kuwa upande wa Mungu ni kuutafuta umasikini ?. Je wachungaji wanatudanganya ya kwamba dhahabu na fedha ni za Mungu ?.
 
Mimi sikubali uwepo wa Mungu.

Lakini pia sikubali katika dhana ya kufanikiwa bila msaada wa wengine.

Ili ufanikiwe bila nguvu yoyote nyuma yako, jambo la kwanza kabisa utakalohitaji ni kujizaa mwenyewe.

Maana ukishazaliwa na wazazi tu, tayari mtu mwingine kashachangia katika mafanikio yako kwa namna moja ama nyingine.
 
shetani hajapewa utajiri pekee bali fahari zote za duniani.

unaona shetani anahitaji kusujudiwa si na Yesu pekee,bali hata kiumbe yeyote wa Mungu anakupa mali unazotaka.

kwa upande wa Mungu si kuutafuta umasikini,maana mali na umasikini havikuwa mpango wake toka mwanzo,bali watu tuishi tu kwa usawa.halikuwa jukumu letu kujua kesho tutakula nini au kuvaa nini,ila tukayatafuta huko eden na kuyapata ya kuyapata.

wachungaji wanatukamata maana tumemezwa na dhiki,tunapenda aina flani tu za mafundisho,nayo ni yale ya mafanikio ya kipesa na kiuchumi,Mungu aliumba dhahabu hata almasi,lakini hazikuwa kwa ajiri ya mtu mmoja mmoja.ndio maana wahuni kwa mpango wa shetani,wakazipandisha thamani ili watu fulani wasimudu kuwa nazo.
 
Hapo naona unasema ili ufanikiwe lazima kuwe na nguvu ya ziada nyuma yako...
 
Hapo naona unasema ili ufanikiwe lazima kuwe na nguvu ya ziada nyuma yako...
Angalau ya kukuzaa tu.

Maana kufanikiwa bila msaada wa mwingine, kwanza unahitaji kujizaa mwenyewe.
 
Ujuzi wa shughuli unayofanya, nidhamu ya kuthamini shughuli yako na uendeshaji wake, itakayowezesha iwe ya hali ya juu, mawasiliano mazuri kati yako na wadau wengine (hasa) wateja, na juhudi/ maarifa za kuyaboresha yote niliyoyataja.
 
Labda nikuulize kitu kama kweli umesoma philosophy, je unaamini unaishi bila kutegemea nguvu yeyote??
 
Mkuu,mbona Ibrahim,Daud na Suleman walikuwa matajiri wakubwa na walimtegemea Mungu?
 
Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.

1 Samweli 2:7
 
Kama unaamini kuhusu Mungu kwenye biblia kuna sehemu anasema
(na tumfanye mtu kwa mfano wetu ).
Unaona Mungu mwenyewe aliamua kushirikisha nguvu nyingine ili kutimiza uumbaji wake,sasa kwanini wewe utake kufanya pasi na kushirikisha nguvu/watu wengine ?

Hii dunia inavyokwenda ipo kama ina sheria yake ya asili tupo kwa kutegemeana nafikiri ni vyema ukiiacha hiyo sheria ya asili ikuongoze utafanikiwa kwa wepesi kama unavyotaka.
Kama ilivyo usiku na mchana,mwanamke na mwanaume,mvua na jua basi ndivyo ilivyo hata kwenye mafanikio lazima mtegemeane.
 
Hata shetani mwenyewe ni mali ya Mungu, wachungaji ni waongo sana wanachotaka ni kujipatia pesa huku wakiishi maisha ya anasa, changamoto ni kuwa Mungu anataka aabudiwe kwa sababu ni Mungu na sio kwa sababu amekupa kitu fulani, katika mazingira yyte yale, utajiri, umaskini, maradhi, Fadhaa, Tabu, Raha. Na hata kifo , sasa anachotaka imani yako kwake iwe costant katika mazingira hayo yote ndo anakupa utajir,....

Swala linakuja kuwa Utajiri ni sehemu alipojibanza shetani, una changamoto sana za kiimani, mtu akiwa tajiri automaticaly anakuwa subjected na majaribu makali kabisa, ambayo ni vigumu kuyakwepa mara nyingi matajiri huwa wanaturnout kumwabudu Mungu, kitu ambacho Mungu hataki kabisa, na kumbuka mission kubwa ya Mungu ni kukutoa kwenye Ulimwengu huu mana kiuhalisia hakuna raha yoyte na maisha ni unpredictable...na ndio maana fahari kuu ya mkristo ni uzima wa milele na sio kitu kingine, Zaidi ya hapo ni surplus

Sasa ili Mungu akupe utajir unahitajika uonyeshe imani isiyoyumba katika nyakat zote za maisha, za amani na shida, Yusuph baada ya kuonyesha imani dhabiti wakati wa taabu na raha mwisho aliruhusiwa kuwa wazir mkuu wa nchi kubwa zaidi kipind hicho, Ayubu baada ya kuonyesha imani kubwa wakati wa taabu na wakati wa raha arihusiwa kuwa na ukwasi wa hatari. Daniel baada ya kuhustle kuisimamia imani aliruhusiwa kuwa kiongozi wa juu wa mataifa makubwa dunian by that time,
Shida kubwa mtu anataka utajiri ili afanye mambo kinyume na Mungu, awe mzinzi, mlevi, majivuno n.k...kwa mazingira hayo lazima uende kwa mganga tuuu,
Mkuu biblia yenyewe inajitosheleza kukupa Mwongozo achana na wachungaji hao ni wahuni tu na wavivu wa kufanya kazi, wangekuwa watu wa Mungu kwa nini hawapatani
 

Mtu alifanya kazi kwa bidii asipofanya dhambi, dhuluma au unaya wowote, Hana dini ila hakufuru Mungu anafuata mambo yake na Hana ushirikina, HUYO naye Mungu anampenda na atampa riziki yake na watoto wake!!

Mi ni Mkristo ninaamini sana katika kuwezeshwa na Mungu, ila Mungu sio mkatili au mbaguzi Kama tunabyofikiri, hapana, hata kidogo...... anawapenda hata wale ambapo sio wake.....

Soma Marko 11:23..... inaanza na yeyote haijasema mkristo au mcha Mungu au anayelala Kanisa, Huu Upendo wa Ki Mungu ndiyo unaofanya watu waache dhambi....
 
Kudanganya ni mzigo.
 
Mafanikio sio ajali. Ipo misingi ya mafanikio ukizingatia na kuthubutu kutafuta unachotaka unafanikiwa bila shida.

Dunia inatoa kila kitu, tatzo ni mimi na wewe.
 
l
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…