Naomba unifafanulie pale shetani alipomuonesha na kumwambia Yesu '' Mali na Fahari zote duniani nimepewa mimi, nitakupa hivi vyote ukinisujudia ", je Mungu amempa utajiri shetani ?, maana yake Kuwa upande wa Mungu ni kuutafuta umasikini ?. Je wachungaji wanatudanganya ya kwamba dhahabu na fedha ni za Mungu ?.
Hata shetani mwenyewe ni mali ya Mungu, wachungaji ni waongo sana wanachotaka ni kujipatia pesa huku wakiishi maisha ya anasa, changamoto ni kuwa Mungu anataka aabudiwe kwa sababu ni Mungu na sio kwa sababu amekupa kitu fulani, katika mazingira yyte yale, utajiri, umaskini, maradhi, Fadhaa, Tabu, Raha. Na hata kifo , sasa anachotaka imani yako kwake iwe costant katika mazingira hayo yote ndo anakupa utajir,....
Swala linakuja kuwa Utajiri ni sehemu alipojibanza shetani, una changamoto sana za kiimani, mtu akiwa tajiri automaticaly anakuwa subjected na majaribu makali kabisa, ambayo ni vigumu kuyakwepa mara nyingi matajiri huwa wanaturnout kumwabudu Mungu, kitu ambacho Mungu hataki kabisa, na kumbuka mission kubwa ya Mungu ni kukutoa kwenye Ulimwengu huu mana kiuhalisia hakuna raha yoyte na maisha ni unpredictable...na ndio maana fahari kuu ya mkristo ni uzima wa milele na sio kitu kingine, Zaidi ya hapo ni surplus
Sasa ili Mungu akupe utajir unahitajika uonyeshe imani isiyoyumba katika nyakat zote za maisha, za amani na shida, Yusuph baada ya kuonyesha imani dhabiti wakati wa taabu na raha mwisho aliruhusiwa kuwa wazir mkuu wa nchi kubwa zaidi kipind hicho, Ayubu baada ya kuonyesha imani kubwa wakati wa taabu na wakati wa raha arihusiwa kuwa na ukwasi wa hatari. Daniel baada ya kuhustle kuisimamia imani aliruhusiwa kuwa kiongozi wa juu wa mataifa makubwa dunian by that time,
Shida kubwa mtu anataka utajiri ili afanye mambo kinyume na Mungu, awe mzinzi, mlevi, majivuno n.k...kwa mazingira hayo lazima uende kwa mganga tuuu,
Mkuu biblia yenyewe inajitosheleza kukupa Mwongozo achana na wachungaji hao ni wahuni tu na wavivu wa kufanya kazi, wangekuwa watu wa Mungu kwa nini hawapatani