Unawezaje kuishi na mwanaume ambaye anakunyamazia bila sababu?

Unawezaje kuishi na mwanaume ambaye anakunyamazia bila sababu?

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
3,278
Reaction score
5,212
Nafikiri mwaka ukiisha mnipe tuzo ya watesekaji bora wa mahusiano JF.

Nipo na huyu kijana mwezi wa pili sasa lakini naona kama mapichapicha japo since tunaanza niliona ni mtu wa hivyo ila nikasema nimpe muda.

Huyu jamaa yangu kwenye upande wa mawasiliano ni kipengele, anaweza kujitahidi siku mbili mkawasiliana vizuri hizo siku zinazobaki sasa utasema ana mashetani! Halafu hayuko romantic, yaani yeye hata kuita majina ya kimahaba hola naitwaga (mamtu), sawa haina tatizo maana nishazoea.

Ila hii tabia yake ya kuwa kimya bila sababu ya msingi inaniumiza. Kuna kipindi ilipita siku 2 hatuwasiliani nikamtafuta kwa kutuma ujumbe na kupiga simu hakunijibu, na mimi nikakausha akaja kunitafuta tena yeye.

Sasa mimi inaniumiza, nawaza au kwasababu jobless maana maandamano yamefanya nipoteze kazi nipo home tu labda ningekuwa na kazi ningekuwa bize. Maana unakuta unatamani kuongea na mpenzi wako ila haoneshi ule utayari ama ushirikiano, inanifanya nakata tamaa.

Ningeweza kumuacha lakini nimeona nijaribu kumvumilia, mwisho wa siku naweza kujikuta nabadilisha mahusiano kila wakati. Ni kijana mwenzangu, kanizidi mwaka 1 (26/27).

Nimeona naweza kutengeneza naye maisha maana wote ni vijana ila sijajua kwa upande wake kama ananihitaji!

Naombeni njia za namna ya kuishi na mwanaume wa namna hiyo, ambaye anaweza kukunyamazia tu bila sababu! Na kama hanifai pia mnaweza mkanambia.
 
Tukiwa tuandelea kujiandaa na tarehe 9 kuelekea uhuru wa Tanganyika nimeona nilete swali kama hoja pamoja na maswahibu yangu

Nafikiri mwaka ukiisha mnipe tuzo ya watesekaji bora wa mahusiano jf

Nipo na huyu Kijana mwezi wa pili sasa lakini Naona kama mapichapicha japo since tunaanza niliona ni mtu wa hivyo ila nikasema nimpe muda..

Huyu jamaa angu kwenye upande wa mawasiliano ni kipengele.. anaweza kujitahidi siku mbili mkawasiliana vizuri hizo siku zinazobaki sasa utasema ana mashetani.. halafu hayuko romantic yaani yeye hata kuita majina ya kimahaba hola naitwaga (mamtu) sawa haina tatizo maana nishazoea

Ila hii tabia yake ya kuwa kimya bila sababu ya msingi inaniumiza.. kuna kipindi ilipita siku 2 hatuwasiliani nikamtafuta kwa kutuma na kupiga simu hakunijibu.. na mimi nikakausha akaja kunitafuta tena yeye..

Sasa mimi inaniumiza nawaza au kwasababu jobless maana maandamano yamefanya nipoteze kazi nipo home tu labda ningekuwa na kazi ningekuwa bize.. maana unakuta unatamani kuongea na mpenzi wako ila haoneshi ule utayari ama ushirikiano inanifanya nakata tamaa

Ningeweza kumuacha lakini nimeona nijaribu kumvumilia mwisho wa siku naweza kujikuta nabadilisha mahusiano kila wakati.. ni kijana mwenzangu kanizidi mwaka 1 26/27
Nimeona naweza kutengeneza nae maisha maana wote ni vijana ila sijajua kwa upande wake kama ananihitaji

Naombeni njia za namna ya kuishi na mwanaume wa namna hiyo.. ambae anaweza kukunyamazia tu bila sababu..
Na kama hanifai pia mnaweza mkanambia
Njoo tujenge mahusiano achana nae huyo hakupendi
 
Back
Top Bottom