Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
JENGA IMANI/UAMINIFU.
Biashara, hivi sasa zinahamia katika digital platforms. Kuna majukwaa mengi ambayo wateja wanakutana na wauzaji na kufanya biashara bila kuonana.
Mifumo hii imeongeza mauzo, na kukuza biashara nyingi, na nguzo kubwa ya mafanikio kwenye majukwaa (platforms) hizi ni uaminifu. Hivyo uaminifu wako ni nguzo kwenye ukuaji wa biashara.
Kuna usemi, unaosema uaminifu hutumia miaka kujenga, sekunde kubomoka/kupotea na unaweza chukua maisha kuurudisha.
Leo tutajifunza namna ya kujenga uaminifu wako na kuutunza.
1. Fanya ulichoahidi. Unaposema utafanya jambo fulani lifanye kama ulivyo ahidi.
Uaminifu hujengwa kwa kutimiza ahadi zako, pale wateja wanapofika kwako na kukubaliana na wewe jambo lolote na kuwaahidi litimize.
Mfano uliwambia watapata bidhaa walizonunua ndani ya siku 2 timiza, kama kuna ofa au zawadi unatoa zitimize. Hii itavuta wengi kwako kwani wanauhakika na usalama wa fedha zao.
2. Usikimbilie kujenga uaminifu kwa haraka, kwa maneno. Zile sentensi za tunatuma kwa uaminifu mkubwa nk.
Hizo zote hazifanyi kazi kwani wengi wanatoa ahadi hizo na hawatimizi hivyo kitakacho kutofautisha nawo ni vitendo.
Jenga uaminifu wako taratibu bila kushawishi sana kwa maneno, kwani uaminifu hutumia muda mrefu kuujenga, usilazimishe watu wakuamini.
3. Jifunze kuwasiliana kwa usahihi (effective communication). Wengi wamevunja uaminifu wao kwa kutoelewana.
Jifunze namna bora ya kuwasiliana na watu wakuelewe unachomaanisha, msipoelewana unaweza poteza imani yako.
4. Ishi na baki kwenye misingi ya biashara yako (business values). Kama misingi ni ubora wa bidhaa, unafuu wa bei, huduma za haraka na rahisi nk.
Jifunze kusimamia misingi hiyo siyo kubadilika mara kwa mara. Kumbuka misingi hiyo ndiyo huleta watu kwako ukibadilika utawapoteza.
5. Wekeza kwenye uhusiano na wateja wako, waanzilishi wengi kwa sasa wana mahusiano ya moja kwa moja na wateja.
Kuwa na mifumo ya kuwasiliana na kupata feedback kutoka kwao, njia hii itakusaidia kuaminika.
6. Jifunze pyramid ya uaminifu, kuza uaminifu taratibu, kutana na watu, jenga interest, deliver na mwisho utaaminika.
7. Kuwa mkweli (Sencere & aunthentic).
Kelvin Kibenje
Mtaalamu wa mauzo na masoko