Unawezaje kulala na mtoto mdogo usiku mama yake akiwa kazini

Unawezaje kulala na mtoto mdogo usiku mama yake akiwa kazini

Na unajisifia kabisa huoni hta aibu
Hivi unaanzaje kumpuuzia mtoto akiwa analia??? Kuna muda analia kwa uchungu mpk wewe mtu mzima unahisi maumivu rohoni
Ndo ivo unaeza ukajiona mjanja ukamwacha Alie kumbe mtoto anaumwa au kina kitu hakipo saw ndo mana analia mwishowe uje kumpoteza mtoto kisa uzembe na ujinga tu,[emoji35]
 
Unachotakiwa kujua ni kwamba mtoto akiwa mdgo huwa anapenda kukumbatia au kuwa karibu na mzazi Ili ajisikie yupo salama na hapo anaeza acha kulia ko wee unachotakiwa kufny ni kuhakikiasha unakuw nae karbu na ahisi uwepo wako na joto lako pia na mama ake kabla hajaondk ahakikishe mtoto ameshiba vizuri na kama unaeza mnunulie pacifier Ili imzubaishe pia
 
Msiwazuie watoto kulia
Kuwa na thermometer mpime joto, angalia ukavu alipolala au alichovaa
Hakikisha ameshiba

Akiendelea lia mtie kofi za miguu atanyamaza
 
Wanaume mbinu tunatoa wapi? We Ukikuta kalala mchana muamshe msumbue sana yaan jion ikiwezekana toka nae zunguka nae mtaa kwa mtaa hakikisha halali kabla ya saa 5 ukimlaza hapo anakua hoi akishtuka kumekucha unamuachia msala mama yake
Hii mbinu angalau itasaidia.
 
Wanaume mbinu tunatoa wapi? We Ukikuta kalala mchana muamshe msumbue sana yaan jion ikiwezekana toka nae zunguka nae mtaa kwa mtaa hakikisha halali kabla ya saa 5 ukimlaza hapo anakua hoi akishtuka kumekucha unamuachia msala mama yake
Kumbe mtoto ni msala...😳
 
Habari...

Wale mlio oa wanawake wanao fanya kazi za shift za usiku tuambieni mnawezaje kulala na mtoto mdogo mpaka asubuhi mama yake anapo kua katika shift ya usiku kazini kwa kuzingatia mtoto wako ni yule anayelia sana nyakati za usiku?

Nawasilisha..
Kwa mtazamo angu mimi, kosa la kwanza ni kuoa mke anae fanya kazi night shift.
Jambo la pili, ni kama wewe ni mzazi hauwezi ukashindwa kulala na mwanao na kumhudumia wakati wa usiku ikiwa amesha anza kula tofauti na kunyonya maziwa ya mama
 
Na utajuaje kama mtoto ameshiba?
Katika hatua za ukuaji, kila mtoto wa umri flani anatakiwa ale chakula kwa kipimo cha milligrams kahdaa.
Hii kwa wale wazazi wenzangu wanafahami (na ndio maana hata chupa za kunyonyeshea watoto huwekewa alama maalum kwaajili ya kutambua ujazo)
 
Mzoeshe kulala kwenye chumba peke yake,akizidi kulialia sana mpuuzie atanyamaza.Ikishindikana kabisa tengeneza mazingira awe anamlilia mama yake wewe deal na mambo mengine.Wangu alikuwa analia usiku kelele kama AKA47 nabembeleza ananyamaza,nikirudi kulala analianzisha nikaamua kuwa nampuuzia tu akaacha.
Itoshe tu kusema kwamba... unajua kuzaa lakini haujui kulea...😊
 
Mzoeshe kulala kwenye chumba peke yake,akizidi kulialia sana mpuuzie atanyamaza.Ikishindikana kabisa tengeneza mazingira awe anamlilia mama yake wewe deal na mambo mengine.Wangu alikuwa analia usiku kelele kama AKA47 nabembeleza ananyamaza,nikirudi kulala analianzisha nikaamua kuwa nampuuzia tu akaacha.
🙄🙄 Daaah nimeamin wanaume siyo walezi,na sio wa kumwachia mtoto.
 
🙄🙄 Daaah nimeamin wanaume siyo walezi,na sio wa kumwachia mtoto.
........umeona eenh, Kwa mujibu wa komenti sisi wanaume wengi sio wa wakutuachia watoto wadogo, 😊 kuna mwamba anasema mtoto asumbuliwe tu hadi saa Tano usiku ili alale hoi, mwingine anadai mtoto akilia achana nae fanya mambo yako, so finally mwingine atasema akilia usiku kata makofi!!......
 
Kuna uncle wangu nilikua namuona ni bingwa wa kulea ila nae alisanda beki tatu wake alivosepa.

Mke kaenda kazina yeye yupo off nyumbani na ndo abaki na mtoto, mishe kitaa hazisongi dogo ni kilio tu.

Ni wachache sana wanaoweza mkuu.
 
🙄🙄 Daaah nimeamin wanaume siyo walezi,na sio wa kumwachia mtoto.
Tatizo mnaongozwa na hisia ni kama mtoto kulia ni kitu cha ajabu sana.Mtoto anatakiwa awe na kitanda chake azoeee hata alie azoee kitanda au chumba chake,akizoea mikono sana au attention ni vigumu sana hata kwa msichana wa kazi kudeal naye.
 
Back
Top Bottom