Unawezaje kulala na mtoto mdogo usiku mama yake akiwa kazini

Unawezaje kulala na mtoto mdogo usiku mama yake akiwa kazini

Hakikisha kwanza kabisa mtoto anakuzoea kwa kupenda kumbeba mara kwa mara na kucheza naye. Yani hata ukimkuta kwa mama yake unambeba, akilia (kabla hajakuzoea) unatoka nae unambembeleza. Na unapocheza nae hakikisha muda mwingi mnatazamana usoni ili aijue sura yako. Akilala wakati uko nae na unataka kumlaza mpeleke chumbani kisha jilaze pamoja nae hata dakika 10. Hii inamfanya alizoee joto lako kwahiyo atakuwa na amani muda wote anapohisi uwepo wako.

Kumbuka mtoto mdogo kabisa humzoea mtu kwa kukariri harufu, joto na sauti mpaka pale atakapokuwa na uwezo wa kuona. Kwahiyo fanya juu chini mtoto aanze kukuzoea mapema sana na akiwa na wewe hawezi kupata hofu muda wowoteatajua yupo mikono salama.

Ni jambo moja kati ya mambo manne tu yanamfanya mtoto alie sana usiku.

1. Upweke 2. Njaa 3. Hofu 4. Kuugua

Ukiweza kudhibiti hayo basi utakuwa umemtuliza
 
Mzoeshe kulala kwenye chumba peke yake,akizidi kulialia sana mpuuzie atanyamaza.Ikishindikana kabisa tengeneza mazingira awe anamlilia mama yake wewe deal na mambo mengine.Wangu alikuwa analia usiku kelele kama AKA47 nabembeleza ananyamaza,nikirudi kulala analianzisha nikaamua kuwa nampuuzia tu akaacha.

Wababa [emoji28][emoji119]
 
Unachotakiwa kujua ni kwamba mtoto akiwa mdgo huwa anapenda kukumbatia au kuwa karibu na mzazi Ili ajisikie yupo salama na hapo anaeza acha kulia ko wee unachotakiwa kufny ni kuhakikiasha unakuw nae karbu na ahisi uwepo wako na joto lako pia na mama ake kabla hajaondk ahakikishe mtoto ameshiba vizuri na kama unaeza mnunulie pacifier Ili imzubaishe pia

Don’t try this

Ukimzoesha joto lako utakua Haufanyi kitu ni kukumbatia mtoto, mpe nafasi ajitegemee hasa muda wa kulala
 
Kinachonishangaza ni kitu kimoja kutoka kwa wanajamii wenzangu jukwaani. Mleta mada ameuliza anachopaswa kufanya wakati wa usiku akiwa amelala na mwanaye. Lakini badala yake anapewa mawaidha ya kumlea mtoto wakati wa mchana ambao hata mamaye anakuwa yupo
 
Ila mtoto mchana anasumbua sana usiku silali bila kupiga maji yangu maana ni shida kweli ndio kwanza ana mwezi mmoja
 
Wanaume mbinu tunatoa wapi? We Ukikuta kalala mchana muamshe msumbue sana yaan jion ikiwezekana toka nae zunguka nae mtaa kwa mtaa hakikisha halali kabla ya saa 5 ukimlaza hapo anakua hoi akishtuka kumekucha unamuachia msala mama yake
Daah wahuni sio watu
 
Habari...

Wale mlio oa wanawake wanao fanya kazi za shift za usiku tuambieni mnawezaje kulala na mtoto mdogo mpaka asubuhi mama yake anapo kua katika shift ya usiku kazini kwa kuzingatia mtoto wako ni yule anayelia sana nyakati za usiku?

Nawasilisha..
Cha muhimu zaidi mtoto ni kushiba na asivimbiwe, maziwa ya chupa yawepo jirani na hakikisha unajua anapenda kulala kwa style gani! Mlaze hivyo anavyotaka ingawa watoto wengi husumbua sana wanapotala kulala yaani ana usingizi halafu bado analia. Hapo muwekee chuchu ya chupa yake huku unatembea tembea ndani usimbembeleze ukiwa umekaaa. Wanataka movement
 
Mzoeshe kulala kwenye chumba peke yake,akizidi kulialia sana mpuuzie atanyamaza.Ikishindikana kabisa tengeneza mazingira awe anamlilia mama yake wewe deal na mambo mengine.Wangu alikuwa analia usiku kelele kama AKA47 nabembeleza ananyamaza,nikirudi kulala analianzisha nikaamua kuwa nampuuzia tu akaacha.
Madhara ya hili utayaona tu baadae mkuu! 😀😀😀jiandae tu kisaikoljia
 
Mtoto ukimzoesha tabia ya kulia hadi anyamaze mwenyewe akikua mkubwa anapata tatizo la Hasira yaani anakuwa short-tempered.
Na ukizoea tabia ya kumbembeleza kila anapolia bila sababu za msingi inakuwaje?
 
Wasikushangae bwana. Ukweli watoto wanapendaga attention na ukiwapa atakayekuja kuumia ni wewe. Mtoto wangu wa kwanza ilikua hivyo akilia kidogo nimeshamkimbilia wakubwa wakanikataza nikaona hawampendi mwanangu.
Alinisumbua sana sana nilikoma. Waliofuata sikurudia kama amekula vizuri, hana homa anajiliza bila sababu alie tu. Na wao na udogo wao wanajua kucheza na saikolojia za wazazi.

Mkubwa wao mpaka leo na ukubwa wake anapenda kulia lia tu
[emoji122]
 
Habari...

Wale mlio oa wanawake wanao fanya kazi za shift za usiku tuambieni mnawezaje kulala na mtoto mdogo mpaka asubuhi mama yake anapo kua katika shift ya usiku kazini kwa kuzingatia mtoto wako ni yule anayelia sana nyakati za usiku?

Nawasilisha..

Kwa kuwa Baba muwajibikaji na sio mbabaishaji, ina maana akiwa analia mkeo akiwepo hauamki kumsaidia? Wanawake wa kiafrica wanaisha maisha magumu sana.
 
Wanaume mbinu tunatoa wapi? We Ukikuta kalala mchana muamshe msumbue sana yaan jion ikiwezekana toka nae zunguka nae mtaa kwa mtaa hakikisha halali kabla ya saa 5 ukimlaza hapo anakua hoi akishtuka kumekucha unamuachia msala mama yake
😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom