Habari za weekend wanajamvi!
Unawezaje kusamehe kirahisi mwanaume aliyecheat tena kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani mnakoishi!! ???!!!
Ni mumeo wa ndoa na mna watoto. Katika harakati za kutafuta pesa ulisafiri kwa muda fulani ndipo alipotumia mwanya huo kufanya aliyofanya.
Uliporudi ukakutana nahizo habari! Na badae mwenyewe kukiri kabisa kufanya kitendo hiko eti hatarudia tena! Inauma sana. Kama wewe utafanyeje hapo!!?? Binafsi sijui hata nifanye nini tangu atubu sijamjibu chochote nipo kimyaa ila naumia sanaaaa!
View attachment 2024934
Pole sana.
Mumeo kafanya makosa mawili ya kiufundi ambayo mwanaume mwenye familia hatakiwi kufanya.
1. Ni kumleta mchepuko nyumbani kwako na hata kumchakata kitandani mwenu. Hii ni dharau ya kiwango cha juu kwa familia na siyo mke pekee.
Sisi wanaume ni wadhaifu sana ikifika kwenye suala la mikia ya wanawake ila, heshima ya familia ni muhimu kuliko utamu wa mchepuko wa masaa machache.
2. Kitendo cha kukiri kumchakata mwanamke mwingine ni dhambi ambayo mwanaume hatakiwi kulifanya. Hata kama ukikutwa kifuani mwa mwanamke mwingine live, hakuna kukiri. Hii ni suala la kisaikolojia kama unavyoona hapa, mumeo alikiri kumchakata mwenzio, japo unajaribu kumsamehe, bado unapata hisia hasi ukivuta picha ya mumeo kitandani na mwanamke mwingine unakuta unapoteza hisia.
Mwisho: wanaume wengi tuna michepuko tena wengi ila inategemea mtu anavyocheza karata zake. Binafsi nilijaribu sana huu mchezo ila baadae nikaona najitesa, nikaamua kuwa na wake wengi badala ya kujidanganya eti nina mke mmoja wakati natumia gharama kubwa ku manage michepuko.
Wanaume na tulio na sifa za kuwa na wake wengi, naomba tujitokeze kwa ujasiri tu, tuache huu ujinga wa kujificha huku tukijua uchakataji unaendelea kimya kimya. Wanawake wapo wengi zaidi ya wanaume, tukisema kila mwanaume abaki na mmoja hatutafika.
Ni hayo tu kwa sasa.
Dada kaa na mumeo myamalize ulinde ndoa. Sisi wanaume ni wapuuzi sana, utamuacha leo ila baada ya miaka kadhaa inawezekana ukajutia uamuzi wako, pia kuna uwezekano ukafanikiwa.
Bila uvumilivu na busara, na misamaha yenu, hakuna familia. Mnalo jukumu la kutuongoza na kutusaidia kuyafikia malengo ya familia.