Mi ninayo VPN master app, niliipakua google.
Ili kuweka urahisi wa kuelewa kuanza tujue hii misamiati .
IP address - Ni namba pekee inayotambulisha kila kifaa cha mawasiliano katika mtandao, iwe ni simu,kompyuta,tablet.IP address huwa ni kitambulisho cha kifaa kimoja tu na huwa haijirudi kwa kifaa kingine. Ni sawa kabisa na alama za vidole zilivyo kwa binadamu! Ipo katika mfumo huu 23.651.98.201
VPN- Ni network server itumikayo ili kuongeza usalama na usiri pindi utumiapo mitandao ya jumuia.
Faida yake kubwa ni kukuficha ukiwa mtandaoni. Kinachofanyika ni kwamba VPN app inakusajili katika mtandao kutumia IP address tofauti kabisa na ile ambayo ndio halisi ya kifaa chako cha mawasiliano. Itaongopa IP address yako na nyingi huonesha kwamba unaingilia mtandao toka mahala tofauti kabisa na ulipo kihalisia.
Mfano:- Upo Mbeya Mwanjelwa, IP address yako halisi ni 23.651.98.201 utakapo install VPN master ukaanza kuitumia itakuwezesha kutumia IP address 45.802.10.150 ambayo ni tofauti na ile halisi na unaweza kuonekana unaingia katika mtandao toka Marekani, Norway,Mexico ama sehemu yoyote ya ulimwengu amabayo huduma hii inapatikana.
Faida za VPN:- Ukiwa unaitumia hii unajiachia utakavyo ukiwa mtandaoni maana usalama wako ni wa uhakika, unaweza hata kumuita yule diki uchwara killazer na hakutakuwa na ushahidi wa kuwezesha waungwana wa TCRA kukutia hatiani. Wakifanya tracing wataishia kupoteana maana taarifa zitakuwa hazikamiliki na watakuwa hawawezi kukugundua exactly muhusika ni nani maana sikuhizi servers za mitandao hutumia utaratibu wa Dynamic Host Control Protocol (DHCP) yani
Kila session utakayoingia mtandaoni utapewa IP address tofauti.