Unawezaje kutumia VPN kwenye simu ya Android? Nini faida zake?

Unawezaje kutumia VPN kwenye simu ya Android? Nini faida zake?

Ivi unawezaje kutumia VPN app kutumia social network hata kama TCRA wamezima mitambo yao kwa muda kama walinvyozimiwaga uganda kipindi cha uchaguzi
Jibu la swali lako ni ndio, unaweza tumia social net ambayo itafungiwa bongo kwa sever za nchi nyingine.
 
Jibu la swali lako ni ndio, unaweza tumia social net ambayo itafungiwa bongo kwa sever za nchi nyingine.
Na jinsi ya kuunga bundle utakuwa unaungaje mkuu wakati hapa tz watakuwa wamefunga mkuu ebu tuelezee kwa mapana kidogo mkuu kama hutojari
 
Wakuu habarini za weekend!

Napenda kufahamu namna ya kutumia hii VPN kwenye simu ya Android maana naona kwenye setting za network ipo.

Pia nini faida zake kama nikiamua kuwa naitumia na inaweza kutumika kwenye WiFi au hata hizi internet za Halotel na Voda?
nsaidie hiyo app
 
Kuitumia ni rahisi hasa kwa kupitia simu, kila VPN host huwa anatoa IP address za nchi tofauti tofauti.
Utakapo install hii app na kuanza kuitumia utakuwa tayari umejiunganisha na host server na ndan utakutana na option ya kuchagua nchi uitakayo na utabonyeza kitufe cha connect ili kuanza kupokea huduma. Kutakuwa na alama ya ufunguo sehemu ya status bar ya simu yako kuonesha upo protected.
Haina process nyingi za kukuchosha.
Kwa hiyoo unatumiaa ukiwa unatumiaa net ya kawaida au wife?
 
Mi ninayo VPN master app, niliipakua google.

Ili kuweka urahisi wa kuelewa kuanza tujue hii misamiati .

IP address -
Ni namba pekee inayotambulisha kila kifaa cha mawasiliano katika mtandao, iwe ni simu,kompyuta,tablet.IP address huwa ni kitambulisho cha kifaa kimoja tu na huwa haijirudi kwa kifaa kingine. Ni sawa kabisa na alama za vidole zilivyo kwa binadamu! Ipo katika mfumo huu 23.651.98.201

VPN- Ni network server itumikayo ili kuongeza usalama na usiri pindi utumiapo mitandao ya jumuia.
Faida yake kubwa ni kukuficha ukiwa mtandaoni. Kinachofanyika ni kwamba VPN app inakusajili katika mtandao kutumia IP address tofauti kabisa na ile ambayo ndio halisi ya kifaa chako cha mawasiliano. Itaongopa IP address yako na nyingi huonesha kwamba unaingilia mtandao toka mahala tofauti kabisa na ulipo kihalisia.

Mfano:- Upo Mbeya Mwanjelwa, IP address yako halisi ni 23.651.98.201 utakapo install VPN master ukaanza kuitumia itakuwezesha kutumia IP address 45.802.10.150 ambayo ni tofauti na ile halisi na unaweza kuonekana unaingia katika mtandao toka Marekani, Norway,Mexico ama sehemu yoyote ya ulimwengu amabayo huduma hii inapatikana.

Faida za VPN:- Ukiwa unaitumia hii unajiachia utakavyo ukiwa mtandaoni maana usalama wako ni wa uhakika, unaweza hata kumuita yule diki uchwara killazer na hakutakuwa na ushahidi wa kuwezesha waungwana wa TCRA kukutia hatiani. Wakifanya tracing wataishia kupoteana maana taarifa zitakuwa hazikamiliki na watakuwa hawawezi kukugundua exactly muhusika ni nani maana sikuhizi servers za mitandao hutumia utaratibu wa Dynamic Host Control Protocol (DHCP) yani
Kila session utakayoingia mtandaoni utapewa IP address tofauti.
Asante kwa maelekezo, naomba kujua namna ya kuitumia, je ni pale unapoifungua tu automatic inaanza kufanya kazi?
Kuna moja inaitwa PSIPHON PRO. Jamaa alinieleza hata kama ukienda nchi waliozuia mitandao ya kijamii kama China waweza ku run app hiyo na kupata acces.
Tatizo sijapata maelekezo ya kutosha namna ya kuitumia. Naomba maelekezo pls.
 
Hio psiphon pro ushaidownload?
 
Hio psiphon pro ushaidownload?
mkuu nimeshainstall VPN MASTER, kwahyo nikishaifungua ndio tayari inafanya kazi automatiki au???

maana nimeopen nikaweka sever ya France, so naweza fungua whatsapp au operamini kupitia hyo VPN master??

swali; Kama Tcra wamezima internet yaan aaccess vip sasa au nikishaifungua tu na server ikiwa France tayari inanipa internet??
 
Na jinsi ya kuunga bundle utakuwa unaungaje mkuu wakati hapa tz watakuwa wamefunga mkuu ebu tuelezee kwa mapana kidogo mkuu kama hutojari
Kujiunga bundle ni jambo moja na kufungua internet ni jambo jingine.
Mfano tcra wakifungia fb haimaanishi jf haitifanya kazi.
Hivyo basi ili kuweza kutumia fb ikiwa imefungiwa hapo sasa inakubidi utumia sever za kukuonesha upo nchi fulani ambapo huko fb haijafungiwa.
 
mkuu nimeshainstall VPN MASTER, kwahyo nikishaifungua ndio tayari inafanya kazi automatiki au???

maana nimeopen nikaweka sever ya France, so naweza fungua whatsapp au operamini kupitia hyo VPN master??

swali; Kama Tcra wamezima internet yaan aaccess vip sasa au nikishaifungua tu na server ikiwa France tayari inanipa internet??
Vpn Master haikufanyi utumie internet bure mkuu bali. Ina kuficha ktk nchi uliyo chagua yani ukifanya jambo lolote kwenye mtandao tcra wakisema wakufuatilie wataona upo france wakati upo tz.
 
Ivi unawezaje kutumia VPN app kutumia social network hata kama TCRA wamezima mitambo yao kwa muda kama walinvyozimiwaga uganda kipindi cha uchaguzi
Now you've hit the nail,nilijua tu lengo ni hili.
 
mkuu nimeshainstall VPN MASTER, kwahyo nikishaifungua ndio tayari inafanya kazi automatiki au???

maana nimeopen nikaweka sever ya France, so naweza fungua whatsapp au operamini kupitia hyo VPN master??

swali; Kama Tcra wamezima internet yaan aaccess vip sasa au nikishaifungua tu na server ikiwa France tayari inanipa internet??
Zamani kwenye hili jukwaa 2013 kushuka chini VPN ilikuwa inatumika kwa ajili ya free unlimited internet pale ambapo open ports zinajuwepo kwenye mitandao husika, kwa sasa tricks nyingi haziwekwi wazi tena, kwa hiyo VPN inakusaidia tu kuficha IP yako na kukupa IP nyingine hivyo kifaa chako kinaonekana kipo kwenye nchi nyingine. Kwa mfano kuna baadhi ya website wanaonyesha drama za wakorea huwa wanalimit bAadhi ya nchi hivyo ukiwa na VPN ukaweka server za nchi ambazo na hiyo huduma ipo basis na wewe utaweza kuwa na access na hiyo huduma.[/QUOTE]
 
Naombeni hiyo nembo ya VPN master, nazicheki zipo nyingi hapa zinanichanganya
 
Zamani kwenye hili jukwaa 2013 kushuka chini VPN ilikuwa inatumika kwa ajili ya free unlimited internet pale ambapo open ports zinajuwepo kwenye mitandao husika, kwa sasa tricks nyingi haziwekwi wazi tena, kwa hiyo VPN inakusaidia tu kuficha IP yako na kukupa IP nyingine hivyo kifaa chako kinaonekana kipo kwenye nchi nyingine. Kwa mfano kuna baadhi ya website wanaonyesha drama za wakorea huwa wanalimit bAadhi ya nchi hivyo ukiwa na VPN ukaweka server za nchi ambazo na hiyo huduma ipo basis na wewe utaweza kuwa na access na hiyo huduma.
[/QUOTE]
Asante mkuu hapa nimekuelewa vizuri sana
 
Back
Top Bottom