Unawezaje kutumia VPN kwenye simu ya Android? Nini faida zake?

Unawezaje kutumia VPN kwenye simu ya Android? Nini faida zake?

Mi nilitumia ila WhatsApp na Facebook call hazikubali, na pia JF app (sio web) haisomi mpaka niondoe ufunguo wa pale juu....nini tatizo?
Kumbe hai-access jf, vp unapotumia unatakiwa kuwa na account mpya?
 
Kutokana na ugumu wa maisha leo siku ya pili nipo mtandaoni natafuta njia za kupita kwenye ganda la ndizi aka kula kitola.
Nimeona VPN imehusishwa kwenye kupata intaneti ya bure, ingawa sina hakika kama inawezekana kwa nchi yetu.
Bado naendelea kuchimbua chimbua ili niachane na kuunga vifurushi.
ingia playstore downlod apk inaitwa your freedom vpn af ntakpa maekekezo jins ya ktumia
 
Mi nilitumia ila WhatsApp na Facebook call hazikubali, na pia JF app (sio web) haisomi mpaka niondoe ufunguo wa pale juu....nini tatizo?
Hii app inategemea na version ya android unayotumia. Ilikuwa released kwa android 4+ ila kuna baadhi ya functions haikuwekewa support mfano hotspot tethering huwa haikubaligi ukiwa on VPN. Hio case yako pia inakuwa miongoni mwa walakini wa hii app.
 
Kwahiyo ukishaweka vpn inabidi ufungue na account nyingine za mitandao? Je vpn inaweza inafanya kazi kwenye browser tu au hata app kama hii ya jf? Vipi kuhusu free VPN nzuri na ubora wake, na unawezaje kuwa na uhakika kwamba uko safe baada ya kuinstall VPN?
Cc: CHIEF MKWAWA, Mwl. Rct, Njunwa wa mavoko.
Huna haja ya account nyengine. Matumizi hasa ni ya kwenye browser ya simu hivyo facebook salama ni ya kupitia browser n.k!
 
Mtandao dhahania wa
kibinafsi
Mtandao dhahania wa kibinafsi (VPN) ni
mtandao wa kompyuta ambao baadhi ya
viungo katikati mwa vitengo hubebwa kwa
unganisho lililowazi au mzungusho wa
dhahania katika baadhi ya mitandao mikubwa
(kwa mfano, wavuti) badala ya nyaya halisi.
Itifaki za tabaka la kiungo cha data cha
mtandao dhahania zinasemekana kupitishwa
kwa mtandao mkubwa zikiwa katika mandhari
haya. Mojawapo ya utendaji ni mawasiliano
yaliyo salama kupitia kwa mtandao wa umma,
lakini hamna haja VPN kuwa na vipengele vya
usalama , kama vile uthibitishaji au usimbaji
fiche wa maudhui. VPN, kwa mfano, inaweza
kutumika kutofautisha mfuatano wa watumiaji
wa jamii tofauti juu ya msingi wa mtandao na
vipengele vya usalama.

VPN yaweza kuwa na utendaji wa juhudi-bora,
au yaweza kuwa na kiwango maalumu cha
huduma cha mkataba wa (SLA) kati ya mteja
wa VPN na mtoa huduma wa VPN. Kwa jumla,
VPN ina topolojia kubwa zaidi kuliko ncha-
kwa-ncha.

VPN inaruhusu watumiaji wa kompyuta
kuonekana kuhakiki kutoka kwa eneo la
anwani ya IP mbali na ile halisi
waliounganishwa nayo kwa mtandao.

CC wikimedia
 
Mi ninayo VPN master app, niliipakua google.

Ili kuweka urahisi wa kuelewa kuanza tujue hii misamiati .

IP address -
Ni namba pekee inayotambulisha kila kifaa cha mawasiliano katika mtandao, iwe ni simu,kompyuta,tablet.IP address huwa ni kitambulisho cha kifaa kimoja tu na huwa haijirudi kwa kifaa kingine. Ni sawa kabisa na alama za vidole zilivyo kwa binadamu! Ipo katika mfumo huu 23.651.98.201

VPN- Ni network server itumikayo ili kuongeza usalama na usiri pindi utumiapo mitandao ya jumuia.
Faida yake kubwa ni kukuficha ukiwa mtandaoni. Kinachofanyika ni kwamba VPN app inakusajili katika mtandao kutumia IP address tofauti kabisa na ile ambayo ndio halisi ya kifaa chako cha mawasiliano. Itaongopa IP address yako na nyingi huonesha kwamba unaingilia mtandao toka mahala tofauti kabisa na ulipo kihalisia.

Mfano:- Upo Mbeya Mwanjelwa, IP address yako halisi ni 23.651.98.201 utakapo install VPN master ukaanza kuitumia itakuwezesha kutumia IP address 45.802.10.150 ambayo ni tofauti na ile halisi na unaweza kuonekana unaingia katika mtandao toka Marekani, Norway,Mexico ama sehemu yoyote ya ulimwengu amabayo huduma hii inapatikana.

Faida za VPN:- Ukiwa unaitumia hii unajiachia utakavyo ukiwa mtandaoni maana usalama wako ni wa uhakika, unaweza hata kumuita yule diki uchwara killazer na hakutakuwa na ushahidi wa kuwezesha waungwana wa TCRA kukutia hatiani. Wakifanya tracing wataishia kupoteana maana taarifa zitakuwa hazikamiliki na watakuwa hawawezi kukugundua exactly muhusika ni nani maana sikuhizi servers za mitandao hutumia utaratibu wa Dynamic Host Control Protocol (DHCP) yani
Kila session utakayoingia mtandaoni utapewa IP address tofauti.
Aaaah hongera mkuu uko vizuri
 
Nahisi ungetumia english ndio ningekuelewa.....kweli kiswahili sikijui
 
Wakuu habarini za weekend!

Napenda kufahamu namna ya kutumia hii VPN kwenye simu ya Android maana naona kwenye setting za network ipo.

Pia nini faida zake kama nikiamua kuwa naitumia na inaweza kutumika kwenye WiFi au hata hizi internet za Halotel na Voda?
Inakusaidia kutumia network unayotaka pale unapokuwa mfano nje ya nchi,VPN. Itakusaidia kua access ntwk ya nyumbani hata kama upon marekani
 
Downloads hii MK ANDROID VPN then install piga 0717545762 upewe user name na password.Tumia line ya zantel au TTCL .kuna malipo 13,000 per month,ni unlimited.
 
Downloads hii MK ANDROID VPN then install piga 0717545762 upewe user name na password.Tumia line ya zantel au TTCL .kuna malipo 13,000 per month,ni unlimited.
Tayari umeshaharibu
 
Mi ninayo VPN master app, niliipakua google.

Ili kuweka urahisi wa kuelewa kuanza tujue hii misamiati .

IP address -
Ni namba pekee inayotambulisha kila kifaa cha mawasiliano katika mtandao, iwe ni simu,kompyuta,tablet.IP address huwa ni kitambulisho cha kifaa kimoja tu na huwa haijirudi kwa kifaa kingine. Ni sawa kabisa na alama za vidole zilivyo kwa binadamu! Ipo katika mfumo huu 23.651.98.201

VPN- Ni network server itumikayo ili kuongeza usalama na usiri pindi utumiapo mitandao ya jumuia.
Faida yake kubwa ni kukuficha ukiwa mtandaoni. Kinachofanyika ni kwamba VPN app inakusajili katika mtandao kutumia IP address tofauti kabisa na ile ambayo ndio halisi ya kifaa chako cha mawasiliano. Itaongopa IP address yako na nyingi huonesha kwamba unaingilia mtandao toka mahala tofauti kabisa na ulipo kihalisia.

Mfano:- Upo Mbeya Mwanjelwa, IP address yako halisi ni 23.651.98.201 utakapo install VPN master ukaanza kuitumia itakuwezesha kutumia IP address 45.802.10.150 ambayo ni tofauti na ile halisi na unaweza kuonekana unaingia katika mtandao toka Marekani, Norway,Mexico ama sehemu yoyote ya ulimwengu amabayo huduma hii inapatikana.

Faida za VPN:- Ukiwa unaitumia hii unajiachia utakavyo ukiwa mtandaoni maana usalama wako ni wa uhakika, unaweza hata kumuita yule diki uchwara killazer na hakutakuwa na ushahidi wa kuwezesha waungwana wa TCRA kukutia hatiani. Wakifanya tracing wataishia kupoteana maana taarifa zitakuwa hazikamiliki na watakuwa hawawezi kukugundua exactly muhusika ni nani maana sikuhizi servers za mitandao hutumia utaratibu wa Dynamic Host Control Protocol (DHCP) yani
Kila session utakayoingia mtandaoni utapewa IP address tofauti.

Umesomeka
 
Back
Top Bottom