Unayo akiba ya Tsh 150,000 kila mwezi na hutaki kufa Masikini, Kataa Ubinafsi, Soma Hapa

Lakini hata watu wakija inbox au kwenye kamwaliko (kikao) wakaona huo mpango wako bado kama hawana nia nzuri wataondoka na wazo lako tu. Ndio maana kuna wadau wamesema humu kwamba wazo nzuri kama hilo huanzishwa na wachache na wanofahamiana vizuri kiuaminfu na hata kiutendaji. Mkishafanya kitu kikasimama ndio sasa mnaweza kualika wengine kwa njia ya hisa na itakuwa ni rahisi kuwashawishi kama tunavyoona makampuni mengine yakiuza hisa. Vinginevyo itakuwa ngumu sana kumobilize watu 50+ kuanzisha hiyo kitu wengi ni matomaso mpaka waone kitu kimesimama ndiyo wanasogea karibu kunusu harufu nzuri itokayo huko! (SIJASEMA HAIWEZEKANI BALI LITAKUWA JAMBO GUMU KUTEKELEZEKA)
 
Mkuu hakuna kitu kigumu duniani kama UBUNIFU na KUFIKIRI.

- Wazo hilo ukiliweka hapa kesho tu mtu anachukua pesa zake anafanya, unabaki huna chako. Ishtoshe ni wazo ambalo nimehangaika nalo mwenyewe mpaka kutengeneza roadmap tangu 2013
mkuu kwa hiyo unataka watu wachange tu pesa bila kujua biashara yenyewe ikoje?...Ukishaeleza kwa kirefu na kina kuhusu hiyo biashara hata wakikuiga hawatakuwa na weledi kama wewe founder!...Weka wazo lako mezani tuone kama linafaa tuanze kujiorganize fasta
 
Hiyo ndio shida yetu tu, vinginevyo ni wazo zuri tu!
Ni kweli kabisa wazo zuri sana ila nikiangaliaga mawazo ya washkaji kwenye magroup ya Watsap!
Huwa naona ni ngumu sana kufanya dili kubwa coz mtaishia kulostishana tu.
 
Mkuu hebu jaribu kuona hawa wachina FOSUN INTERNATIONAL walianza watu wangapi ?
Brother usijilinganishe na wachina na wazungu katika haya mambo wenzetu wana exposure kubwa na muda mrefu kuliko sisi na hata culture zao kiutendaji, uaminifu n.k ni tofauti sana na sisi wabongo! Huo ndio ukweli! Inawezekana hili jambo kufanyika lakini tusicopy na kupaste tuliangalie katika mtazamo wa kibongo utekelezaji wake!
 
bro sio kumobilize ishu ni kwamba je mnaweza simama katika nia moja kwakutojali profit kwa kipindi fulani hili kuweza kufanya biashara iweze kusimama na kwenda mbele.....unajua leo hii mtu unaweza sema kwakua tumeingia kiasi fulani inabidi tuweke kitu fulani kwa faida ya biashara lakn kuna watu kwakua mna hisa sawa watakaa
 
Mkuu ya wezekana ukawa na Mawazo yenye dhamira nzuri sana " na unahitaji " kuona vijana tukijikomboa kwenye Giza LA dhiki "".. lakini changamoto iliyopo ni kwamba vijana wengi wa taifa hili ni wahanga wa utapeli "...vijana wengi waliokuja na Mawazo kama yako yanayohusu maedeleo " wameshindwa kuwa waaminifu na kusababisha kuwaachia makovu ya utapeli "" tokana na tamaa zao walizonazo " hali hii imepelekea watu waliotapeliwa ambao ndio wengi kutokuwa na imani " hata pale anapojitokeza MTU Mwenye wazo chanya " lisilo na mlengo wa kitapeli ''na kijana huyo kutoweza kuaminika
 
Ni kweli kabisa wazo zuri sana ila nikiangaliaga mawazo ya washkaji kwenye magroup ya Watsap!
Huwa naona ni ngumu sana kufanya dili kubwa coz mtaishia kulostishana tu.
Hakika dunia sio mbaya bali walimwengu ndio wabaya
 
Count me in. Ila ni vizuri ukaweka info zako ile uaminifu uongezekee
 
Lakini Mkuu ni suala la kuamua tu, wenzetu hata mfumo wa hisa wakati mwingine siyo lazima. Mtu anatoa mchango tu wa kuraise Start up fulani bila hata kuwemo.

Ona hawa hawa www.mvmtwatches.com walipata funds kuraise tu hapa www.indiegogo.com na wakaanza leo wako mbali. Yaani sisi labda mwaka 3,000 huko !
 
Amina mungu ajaalie kwa hilo, ila ujuwe tu umaskini wako hutokutesa pekeyako na watoto pia watateseka
 
Nilishalizwa mambo ya biashara za ubia... haya mambo tatizo uaminifu zero
Ulilizwa kwasababu ulifanya partnership, ungefanya ubia kwa mfumo wa LIMITED COMPANY Mtaji wako ungekuwa salama !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…