Hahaaaaa, umenifanya nichangie fasta hii thread maana juzi nilikua nawafundisha wanafunzi wangu mahali fulani nikawaambia kuwa hawajui kuandika essay kwasababu wao siku hizi wanategemea sms ambazo zimefupishwa kiasi kwamba huwezi jua hata maana yake. Enzi hizo nipo pale Magamba Boys now ( SeKUCo- Sebastian Kolowa University College-Lushoto) ndio nilikua nafanya dili za kuwaandikia washkaji barua halafu wananilipa....serious nilikua bingwa wa kuandika hizo barua hasa kwa lugha ya kigeni maana zilikua zinaenda Mazinde Juu ( St.Mary's) au Kifungilo Girls' ambako ndio by then kulikua na watoto wakali kinoma na ngeli inapanda sana, sasa ukiaka uwapate lazima uandike barua kwa kiingereza.
Nilikua naenda kununua karatasi maalum za kuandikia barua za mapenzi halafu nawauzia jamaa, kisha kama nitaandika Mimi hio barua inabidi uongeze dau! Ndio maisha yangu yalivyokuwa, huwezi kwenda kununua kadi bila kupata ushauri wangu.....next time nitawaeleza kisa nilichokifanya kwa mshkaji aliekua anataka nikamnunulie Card amtumie Demu wake pale Mazinde Juu.
Barua zilisaidia sana kuweza kuandika essay zenye maana na kanuni za uandishi zilizingatiwa......Umenikumbusha mbali saaaaana