Diamond kakariri kwamba mashabiki wa sasa wanataka nyimbo za kuchezeka sawa hatukatai lakini sasa ziwe za kueleweka jamani mbona Kina Davido na Wizkid wamestick kwenye namna yao ileile ya uimbaji???...ukisikiliza Wizkid Essence na huu utopolo ndio utaona tofauti kati ya mchele na chuya..Mtu Yupo chini Warner Music basi imba nyimbo ambazo hata hao Warner hawatosita kukupromote kwenye billboards HUTAKI napata picha kwanini alivunja mkataba wake na Universal mwenyewe akauita wa kinyonyaji wakati zaidi ya asilimia 75 ya wasanii Marekani wapo chini ya Universal huenda kuwa Universal walivunja mkataba na yeye baada ya kuona hana ishu ukweli ni kwamba tangu 2019 Diamond platinumz anatoa nyimbo nyepesi mno ambazo hawezi kutumia kama CV kuomba collabo kwa watu kama Kina Wiz khalifa anaopiga nao picha,Drake,Ty Dolla sign na wengjneo kama wenzio kina Wizkid wanavyofanya..Wizkid sasahivi amekuwa ni lulu wasanii wakubwa kina Justin Bieber,Kranium n.k wanaomba wenyewe washirikishwe kwenye nyimbo zake