Undani wa point pendwa ya Sarajevo assassination.

Jamaa history ulipiga fresh coz unashusha nondo kama ilivyo na watu tunakuelewa big up.
Yap advance nilisomaga HGL mkuu.kwa hiyo haya mambo tulikuwa tunachezacheza nayo sana.Mia mkuu
 
Haya mauaji yaliwapa wababe sababu ya kutangaza vita ila watu walishajiandaa kitambo.Ferdnand alitumwa makusudi aende Bosnia na Mazayuni hayo hayo yakawa tuma wale vijana wamuue ili vita itokee
 
Mkuu labda umeelewa tofaut hii sarajevo assasination ni point maarufu ya causes of first world war.waliosoma history form four wanaijuavizuri

Ndo msingi wa title
Achana naye hajasoma hisotory huyo,labda alikomaa na machemikoo tu.Hatuachie sisi wazee wa mafuvu tufurahie huondo.Asante sana mkuu umenikumbusha enzi hizo.
 
Achana naye hajasoma hisotory huyo,labda alikomaa na machemikoo tu.Hatuachie sisi wazee wa mafuvu tufurahie huondo.Asante sana mkuu umenikumbusha enzi hizo.
Hahahaaa huyo atakuwa mzee wa makemiko kweliii
 
Kama ulitakiwa kujibu suali kuhusu vyanzo vya vita kuu ya kwanza, basi huwezi kukwepa hii ya mauaji ya Archduke Franz Ferdinand.

Waserbia pia walichukizwa sana na kitendo cha Austria-Hungary kuifanya Sarajevo kuwa sehemu yake mwaka 1908.

Pili, ilikuwa ni dhahiri kwamba Archduke Franz Ferdinand angekuja kuwa mfamle wa Austria-Hungary jambo lililowaudhi zaidi waSerbia.

Halafu pia kuna sababu zingine za nyongeza kuhusiana na mauaji hayo.

1. Wakati Archduke Franz Ferdinand na mkewe Sophie wakikagua vikosi vya jeshi huko Sarajevo pia walikuwa walisherehekea miaka michache ya ndoa yao.

Baba yake Franz mfalme wa Austria Franz Joseph alikuwa amemkataza mwanae kutoonekana nje kwenye shughuli za umati wa watu kwasababu Sophie alikuwa ni "commoner" yaani mtu asiye na cheo ndani ya ukoo wa kifalme yaani alikuwa ametoka katika familia ya kawaida.

2. June 28 mwaka 1914 ilikuwa ni siku ya taifa ya Serbia.

3. Baada ya kumpiga risasi Franz Ferdinand muuaji Pricip akajaribu kumpiga risasi gavana wa Sarajevo alieitwa Potiorek ambae alikuwa ni muAustria aliekuwa amekaa kwenye kiti cha mbele kwenye gari na katika purukushani ndiyo akapiga risasi Sophie.

4. Black hand kilikuwa ni kikundi cha kigaidi.
 
Umeelezea vzur sana,ongera sana
 
Mtoa post hii uliyoeleza sio point iliyosababisha vita, umetoa tu historia ya kifo cha mtu tu. Hujaeleza jinsi gani kuuawa kwake kumeleta vita.
 
Mtoa post hii uliyoeleza sio point iliyosababisha vita, umetoa tu historia ya kifo cha mtu tu. Hujaeleza jinsi gani kuuawa kwake kumeleta vita.
Yaa,alutakiwa aonesha na Altimatum ya Austeo Hungary kwa Serbia.
 
Yaa,alutakiwa aonesha na Altimatum ya Austeo Hungary kwa Serbia.
Lengo langu nilikuwa najaribu ku trace back background mpaka Archiduke Ferdinand anapigwa risasi.Maana wengi wanajua tu alipigwa risasi ila hawajui yaliyokua yanaendelea.

Kosa nililokosea ni ku assume watu wanajua relationship ya hili tukio na kuanza kwa vita vya dunia ndo maana sikuieezea.Japo nimetoa mwanga kwenye comment no 30
 
Mmh . Sioni point hapo yaani wewe umuue adui halafu na wewe ujiue? Unafaidika nini sasa?
Ni kiapo cha uzalendo alichotoka nacho kwao. Hata Wajapan, walikua na mbinu ya Kamikaze, unajiua katikati ya naadui huku ukiwadhuru wao kwa wingi. Ni kama wafanyavyo magaidi wanajilipua Iraki, Afghanistani na Syria
 
Mwandishi asante kwa andiko lako japo hujasema ni kwa nini vita ya dunia ianze kwa sababu ya kifo cha huyo jamaa na mkewe. Washirika wa hiyo vita wanahusiana vipi na marehemu Franz?
Kwa kukusaidia, mgogoro ambao ungepelekea vita ulikuepo na ulikua unafukuta tayari chini kwa chini kama mwandishi alivyoandika. Haya mauaji yaliharakisha tu mwanzo wa vita.
 
Mkuu kwanini ziitwe vita ya dunia wakati zimepiganwa na wazungu peke yao??? Huko america ya kusini hta haikurushwa risasi au ndio wazungu wanatuburuza
Sababu kuu ni kwamba vita hivi vilibeba wanajeshi na rasilimali zingine kutoka almost mabara yote ambayo yalitawaliwa na Waingereza, Wajerumani, Wareno, Wafaransa nk. Makaburi ya wanajeshi walioshiriki vita hizi kwa Dar yapo pale Upanga, opposite na Redcross kama unatoka city centre kuelekea Selander.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…