Under value food crops ambazo zinaweza kuwa ni biashara kubwa sana

Under value food crops ambazo zinaweza kuwa ni biashara kubwa sana

Nimewahi andika maoni humu kwenye maboga.
Tunaweza kutumia mazao yasio ya gharama kama viazi vitamu kulisha mifugo. Kwa hio pesa utaipata kwa kuuza mifugo si zao lenyewe .

Maboga kwa sasa ni dili hasa mbegu zake.
Nyama ya boga lisha mfugo ile mbegu
sindika kauze au kamua mafuta.
Wataalamu watusaidie aina ya maboga yanayotoa mbegu nyingi na mafuta mengi.
🙏🙏🙏
 
Watanzania wengi still na still tunalima au kufanya vitu kwa kuigana tu. Hii hupelekea mazao menhine kuwa na wakulima.wachache sana.

Nani mfano analima mazao haya comercialy?

1. Viazi vitamu
2.Magimbi
3.Maboga

Mazao tajwa hapo juu yana demandi kubwa sana na inalekea productions yake ni ile traditional ya kujilimia kijisehemu tu. Ila ukweli ni kwamba hayo mazao yanaweza limwa kibiashara na.yakafanya vyema kabisa.

Magimbi yana bei kubwa sana na pamoja na kuwa na bei kubwa.ila bado production yake iko chini sana.watu tunalima Magimbi traditional. Kuna mdada mmoja yuko Songea nazani kuna.siku alinipigia simu akasema anataka kulima hekari 10 za Magimbi kwa kuanzia ila target yake ni hekari 50.Magimbi bado ni chakula cha wenye vipato kiasi make kwa sisi choka mbaya hatuwezani na bei yake, sasa kwa nini tusiongeze supply?

Nitamtafuta nijue kafikia wapi now make ni kitambo.

Viazi the same, wanai chonswa na mikate, vitumbua na mandazi ni wengi kwa sasa na na hawa wanataka vitu kama viazi na magimbi.

Maboga yana demand sana na yana soko pia zuri kwa foregners, Super Market kubwa hazina watu wa kuwa supplier Maboga through the year. Maboga nayo ni yanalimwa traditionaly sana.

Hayo mazao tajwa hapo yanaweza fanywa kibiashara na ikibidi kufanya umwagiliaji wa kuweza kuvuna mwaka mzima.
🙏
 
Nashukuru kwa maoni ni kweli unayoyasema mkuu , Kwa mimi sio kwamba ndo naanza kuingia kwenye kilimo ni mzoefu ! Ni idea tu nilitamani tu kuifanyia kazi kwa sababu uendeshaji wake na gharama ni wa kawaida sana ! Maana mashamba ni ya kwangu sikodishi na yako karibu na mito kwa hiyo ishu ya kumwagilia sio tatizo !! Ndo maana nikaonelea niifanye pia Rossela zinatunzika zikishakauka vizuri haina shida !! Hata kama itatokea bei ziko chini sio shida!!

Kupata hasara inawezekana na faida inawezekana ! Hata huyo aliyelima mchai chai alikosa lakini angejiongeza mchai chai unauzwa kwa design nyingi kukaushwa na kusagwa inawezekana ! Na pia mchai chai ni wa muda wote mradi upate maji ya kutosha labda kama huyo jamaa kama hakujipanga kipindi cha kiangazi sio kama karoti au vitunguu kwamba ukichuma ndo mkataba umeisha !!
Una akili sana, na mtu asiniulize kwa nini nimesema hivyo! ☑️👏👏👏🙏🙏
 
wachana na mihemko kuna mzee aliwahi kuitwa mchaichai kisa hii mihemko ya kijinga kacheki sokoni mchaichae bei juu akaenda kulima heka la mchaichai uliza kilichomkuta sasa
NIni kilimkuta?

Mchaichai unaweza kukausha ukapack au ukasaga iwe unga..
Nadhani hakujipanga vizuri.
 
Ndio ndugu. Hata wasukuma wanakausha wanauta mapalage kama sijakosea. Viazi vinaweza kuhifadhiwa vyema.
Mapalage au michembe, Pia vingine wanavipika halafu wanakausha (matobolwa)
 
Back
Top Bottom