Fighter101
Member
- Jan 8, 2022
- 46
- 64
umeongea jambo la maana sana ambalo naona watu wengi hawalichukulii maanani. ila blacks ndio tunaoongoza kwa nyama uzembe.Watu wenye unene uliopitiliza wanaongezeka kwa idadi duniani. Tunapanda nao madaladala na wanachukua nafasi ya watu wawili wakati wanalipikia kiti kimoja. Hata ile sehemu ya kusimama, ukigeuka hivi umekutana na tumbo mara mgongo. Ulisombe ukae dirishani na yeye awe jirani yako atakubana wewe.
Kwakweli wanga uliochanganywa na mafuta una ladha tamu sana. Kuanzia keki mpaka pilau iliyokolea mafuta. Nyama ya kidari ina ladha ya pekeee. Binafsi huwa ninaikaanga mpaka inakua hudhurungi ndipo nina ipika kwa moto mdogo nikichanganya na mboga mboga.
Huko tunakokwenda mashirika ya ndege yatalazimika kuweka viti ya obese na kuwawekea bei yao, sasa uzito wa kilo 98-100+ unashindwa kupanda business class! Huku economy class tuachiwe tunaokula ugali na papa ya kulumangia.
watu wengi wanakula ovyo ovyo huku hawataki hata kufanya mazoezi, "YOUR BODY SIZE REFLECTS YOUR LIFE STYLE AND WHAT YOU EAT".