Unene wa mke wangu unamuweka matatani

Unene wa mke wangu unamuweka matatani

We unastahili ban,unaleta story zako za kijingajinga ukfikiri humu ndai kuna mataahira,umetoka kuanzisha thread hukai na mwanamke now unatuletea huu upuuzi.
Hahahahah! Amesha sahau kama amedumu na bonge kwa miaka 10.
 
Umejiita ze big kwa sababu ya unene wa mkeo??..unajifananisha na mkeo??..safi sana
 
Uckute ww ndo uyo mnene mwenye kg 110 af unajfanya mkeo ndo mana hudum na dem kwa zaid ya cku 4...
 
duuuh huyo mkeo kiboko ana kula kama kiboko kilo mbil za mdudu dadek sio mchezo ana tumbo pakacha????
 
umeumbukaaaaa duuh kwahiyo ulizan sie mataahira leta thread nyingne hadithi zako tamuuu naona unazo nyingi
 
Sasa stress si angekonda stress gani ananenepa
Kuna aina mbili ya matendo wanayofanya watu wakiwa na stress
1. Kuna baadhi wanakula sana kwa maana wanapunguza msongo wa mawazo kwa kufanya kitu kinachofawariji bila kujizuia.
2. Kuna baadhi wanashindwa kula kwa sababu ya msongo wa mawazo.

Probably huyu mke wa mdau hapa ana msongo wa mawazo ambao umepelekea kushindwa tena kujizuia baada ya kujenga tabia ya kula kupita kiasi, na huu ukali unaokuja ukigusia mazoezi unaweza uka-justify kilichopo kwenye kichwa chake.
 
Kuna aina mbili ya matendo wanayofanya watu wakiwa na stress
1. Kuna baadhi wanakula sana kwa maana wanapunguza msongo wa mawazo kwa kufanya kitu kinachofawariji bila kujizuia.
2. Kuna baadhi wanashindwa kula kwa sababu ya msongo wa mawazo.

Probably huyu mke wa mdau hapa ana msongo wa mawazo ambao umepelekea kushindwa tena kujizuia baada ya kujenga tabia ya kula kupita kiasi, na huu ukali unaokuja ukigusia mazoezi unaweza uka-justify kilichopo kwenye kichwa chake.
Aasante sana mheshimiwa umenisaidia sana naomba nijue nifanyeje sasa
 
Umeshafanya yote unayoweza kufanya, cha mwisho mueleze tena madhara ya unene, na hatari zitakazo tokea kama anapata diabetes, hypertension, stroke ect. Mwisho wa siku akiwa ni mtu mzima mwenye akili timamu, na ameshapata maelezo ana uhuru wa kuchagua juu ya maisha yake (power of autonomy). Huweza kumlazimisha kama hataki.
 
Ila mkeo kiboko au anapepo mkuu ebu tafuta watu wenye hekima wamshauri.. Unene yaan sio dili afu mbona wanawake wenzie wamegutuka wanafanya mazoez tena ye unamsapot bado mbishi chaaaaaa
 
Exactly!
Na huo ukali kuhusu unene wake ni kwa sababu issue ya msingi inayompa stress haijafanyiwa kazi. Anajiskia kuonewa kuangaliwa matokeo badala ya chanzo.

Mtoa mada, hii ni jf. Tutaremba hapa Na kukuonea huruma Na kumshangaa mkeo. Mwisho wa siku wewe unajua jinsi ya kutatua shida alizo nazo mkeo kabla wasamaria wema Na washauri wa mjini hawajamsaidia kwa mbinu m'badala.
Mkeo ana stress...
 
Ni unene wa kula, kilo 2 za kitimoto kila siku si mchezo, mwambie afanye mazoezi aache ubishi, apunguze kula sana.
 
Mtengenezee mazingira akachukue mkope Access bank,mkopo ambao atashindwa kuulipa,then uone kama hatakonda,au apate kipindu pindu
 
Huyo talaka tu ndo solusheni lasivo atakuja kukufia ndani,inawezekanaje mke awe na uwezo wa kukataa maelekezo yako?
 
Pole sana Mkuu, kuna wengine wanaweza kuwa na masters au Phd lakini hawajaelimika. Nimeshangaa sana hapo ulipondika kwamba alimjia juu Doctor baada ya kumpa recommendations zake za kupambana na unene.

Solution ya kupambana na tatizo hili kubwa ni kwenda pamoja gym na yeye kuacha kufakamia mavyakula hovyo hovyo tena kupita kiasi. Umeandika kwamba unaweza kumpoteza mkeo, hilo ni kweli kabisa mwambie anajichimbia kaburi mwenyewe na jaribu kuwa mkali at the same time umuonyeshe kwamba unampenda na kumuhitaji kwenye maisha yako wewe na watoto.

Hajitambui huyu, kila la heri na Baraka katika juhudi zako. Usisahau kuleta mrejesho uwe hasi au chanya.

Nilifanikiwa kupata mwenza wa maisha (kuoa) mnamo mwaka 2006 kipindi ninaoa mimi nilikua na uzani wa kilo 50 na wife alikua na kilo 42 maisha yalisonga tukapata mtoto wakwanza. Wife alijifungua normal kabisa na tukalea mtoto wetu wa kwanza wife alikua na kilo 44 mpaka mwanetu anafikisha umri wa miaka mitatu mwaka 2009. Tukafanikiwa kupata mtoto wa pili ambae Mungu si athumani wife alijofungua salama pia na mpaka mwanetu anafikisha miaka mitatu wife alikua na kilo zile zile 44.

Hatujawahi kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ila mnamo mwaka 2014 wife alianza kunenepa katika kipindi cha mwaka mmoja alitoka kilo 44 mpaka 76. Nilijitahidi kumshawishi japo kwa njia ambayo isinge mkwaza kua tuwe tunakimbia kimbia jioni wife akisikia swala la mazoezi anakua mkali nitanuniwa hata wiki tatu haongei yeye ni ku deal na watoto tu.

Ilipofika mwaka jana mwishoni wife alifikia kilo 95 kuna kipindi alikuwa anappata dalili za pressure tukaenda hospitali daktari alimshauri apunguze weight lakini alimgombeza daktari kama mtoto mdogo kua amuache yeye ni mtu mzima kama kumtibu ameshindwa aseme. Sikuwa na jinsi zaidi ya kua mpole na kupewa baadhi ya vidonge na kurudi nyumbani.

Mwezi uliopita wife amefika kilo 110 ambazo zinazidi kumuweka katika hatari yakupata magonjwa mengine ya hatari zaidi. Ameanza kukoroma kwa sauti kubwa sana usiku na akilala hataki umuamshe hata kama kuna kitu chochote kile amekua mkali sana na hata haki ya ndoa anasema anachoka sana skuizi ananipiga kalenda. Unene wa wife umekua ukinipa uoga na kumuonea mke wangu huruma sana hasa nikiona anapokua akilalamika miguu inamuuma.

Kuna siku nilijaribu kumwambia miguu inakuuma kwasababu ameongezeka uzito katika kipindi kifupi mno, hili lilizua ugomvi mpaka tukaenda kusuluhisha kwa wazazi baada ya miezi miwili ya kuvutiwa mdomo na kukosa amani ndani ya nyumba kwa kumshauri wife jambo la busara tu.

Kwa sasa nina kilo 54 wife anachezea 110 ninaomba ushauri nifanyeje wife anielewe na aweze japo kufanya mazoezi amekua kibonge sana na anapata matatizo ambayo yananiogopesha naweza kumpoteza mama watoto. Nilishawahi kujaribu kumshauri tujiunge kwa pamoja gym hilo ndilo lilizua maneno kuwa ninafuata wanawake huko gym namshangaa wife japo ni msomi ana masters yake ila haoni umuhimu wa afya yake.

Kitu kinachomfanya wife awe hivi ni kula kupita kiasi na kupenda sana vitu vya wanga kuna siku kulikua na birthday ya mwanetu alikula keki ya kilo tatu na ile sukari ya juu yote baada yakuwakatia watoto. Anaweza kutoka kazini akapita mahali akala hata kilo mbili za kitimoto, kuna siku nilimfuma anakula kitimoto bar kwa makadirio kilikua kama kilo 2 nikajaribu kudadisi nikagundua huwa ana desturi yakupita pale kila siku na ameweka oda kabisa na akifika nyumbani pia anafanya majukumu yake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapikia watoto na hula tena mara yapili na kulala akimaliza tu kula.

Ninaombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kunusuru afya ya mke wangu.
 
Back
Top Bottom