Unga wa kwenye bomba la kutolea moshi wa gari una kazi gani?

Shin Lim

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
7,837
Reaction score
14,198
Sijui mimi ni mshamba au vipi! Lakini ukweli ni kuwa inaonesha unga huo umekuwa dili, unatolewa sana.

Sasa je, hakuna madhara kwenye gari lililotolewa huo unga?
 
Unga gani huo au ni masizi, ule mweusi unaosababishwa na moshi? Wanaufanyia nini wakiutoa hata useme imekuwa dili?
Sina uhakika ila ninachofikiri ni kuwa unatolewa ili usizibe mfumo wa kutoa moshi na kusababisha matatizo mengine.
 
Mimi pia nasubiri kujua ule unga unafanyiwa kazi gani... naona mtu anakuja anataka kununua kile ki bafla kwa hela ndefu.

Kuhusu kaz yake katika exhaust ni kupunguza kuchafua hali ya hewa
 
Mkuu, naona hauja fahamu kinacho zungumziwa...😂😂😂
Usije tu ukadhania ni unga wa Dona ndio unajadiliwa hapa...🤣🤣
 
Mimi pia nasubiri kujua ule unga unafanyiwa kazi gani... naona mtu anakuja anataka kununua kile ki bafla kwa hela ndefu.

Kuhusu kaz yake katika exhaust ni kupunguza kuchafua hali ya hewa
Inasemekana ilekitu huwa inachukuliwa na kusagwa Hadiikuwe laini kama poda, Kisha inachanganywa na kitu ingine (naomba nisiitaje), alafu inawekwa kwenye vifungashio vidogo tayari kwa kuingia sokoni kwaajili ya kunusa/kulamba kama brauni shuga
 
Unga gani huo au ni masizi, ule mweusi unaosababishwa na moshi? Wanaufanyia nini wakiutoa hata useme imekuwa dili?
Sina uhakika ila ninachofikiri ni kuwa unatolewa ili usizibe mfumo wa kutoa moshi na kusababisha matatizo mengine.
Itoshe tu kusema kuna unga kule nyuma ni hela ile. Hebu tuwasubiri mafundi waje.
 
Mimi pia nasubiri kujua ule unga unafanyiwa kazi gani... naona mtu anakuja anataka kununua kile ki bafla kwa hela ndefu.

Mimi pia nasubiri kujua ule unga unafanyiwa kazi gani... naona mtu anakuja anataka kununua kile ki bafla kwa hela ndefu.

Kuhusu kaz yake katika exhaust ni kupunguza kuchafua hali ya hewa k
Ni mgodi unao tembea, kwenye catalytic converter Kuna madini ya thamani kama platinum (Pt) palladium (Pd), na rhodium (Rh).
 
Kiufupi huo unga ni biashara kubwa, sehemu kama zimbabwe kuna makpuni kabisa yanatangaza yananunua.

Kwa hapa bongo nashangaa watu wanauza kwa elf 80 na ikienda sana ni laki.

kwa zimbabwe kuna watu wanakifata kabisa uwauzie tena kwa kupimo cha uzito, Kilo moja ni dola 150 (zaidi ya laki 3) na ikiwa yenye ubora wa juu basi unaweza kupewa hata dola 200 (zaidi ya laki 4)

Sasa inavyoonekana hapa bongo wanaozonunua kwa bei chee nao wanaenda kuziuza zimbabwe au afrika kusini.

Unga huu ni biashara kubwa kw anchi za china, uingereza, marekani, n.k....Huko ni kawaida sana kupewa milioni 2 au zaidi kwa unga huu huu ambao mafundi wa bongo wanatuibia wanaenda kuuza elf 80.

Sasa sijajua unatumika wapi ila nachojua ni biashara halali kabisa
 
Back
Top Bottom