Unga wa kwenye bomba la kutolea moshi wa gari una kazi gani?

Unga wa kwenye bomba la kutolea moshi wa gari una kazi gani?

Sijui mimi ni mshamba au vipi! Lakini ukweli ni kuwa inaonesha unga huo umekuwa dili, unatolewa sana.

Sasa je, hakuna madhara kwenye gari lililotolewa huo unga?
Ule unga ni akiba yako endapo utakwama porini bila msaada, weka kwenye kikombe changanya na majimoto toka kwenye rejeta utapata uji.
Unga ule ni kwa ajili ya kuchuja sumu ya lead itokanayo na uunguaji wa mafuta.
 
Una umuhimu mkubwa sana kuwepo kwenye mafla ya exhaust...

Husaidi kupunguza hewa au gesi chafu zinazozalishwa na engine...

Hii pia husaidia kupunguza uchavuzi wa mazingira...

Gari likiwa vizuri, kwenye exhaust litatoa mvuke msafi ulio transparent au matone ya maji, hiyo ni kazi ya huo unga, bila huo unga ni moshi mkubwa mweusi na majivu... hupelekea gari kukosa nguvu na hatimae engine kuchoka mapema...

Cc: mahondaw
Kibaya zaidi baadhi ya wamiliki wa magari hawajui kabisa kuhusu hii ishu. Kwa madhara hayo uliyotaja inabidi kuwa makini sana.
 
Siku hizi unga ni kama bikra. Unavyonunua gari angalia bikra ipo? kama hamna mnaanza kuongea biashara upya hata kama gari ni DYY
 
The organization blames the under-vehicle crime wave on much higher prices for the valuable metals inside catalytic converters. One metal, rhodium, has skyrocketed to about $28,000 an ounce, though only a tiny fraction of that quantity — perhaps worth a few hundred dollars — goes inside each converter.

F22DD112-A461-43FB-AB5B-44D1345378A7.jpeg
 
Kama gari ni yako ikitolewa huo unga lazima tu utajuwa kwa sababu mlio wa gari unabadilika unakuwa mkubwa kuliko kawaida, gari inapoteza nguvu na gari inaanza kula mafuta kuliko kawaida. Kuna gari wanakata kwa gesi wanatoa halafu wanachomea tena. Na kuna gari nyingine wanafungua "exhaust" halafu wanauchokonoa huo unga unatoka.

Waathirika wakubwa ni wale:-
1. Wamiliki wa "uber". Madereva wengi wa "uber" ndio wanauza sana huo unga. Wamiliki fanyeni utafiti kuanzia leo muone kinachofantywa na madereva wenu.
2. Wamiliki wa magari wanaoacha magari yao kwa mafundi kwa muda mrefu.
4. Wamiliki wa magari wanaoacha magari yao muda mrefu kwa waosha magari. Sasa hivi kumezuka mtindo wahusika wanakaa karibu/jirani kabisa na "car wash"/gereji na vifaa vyao vya kazi tayari tayari ukiacha gari ukaondoka nusu saa tu jamaa wanamaliza shughuli fasta.
5. Wamiliki wa magari wanaowapa madalali wakawauzie magari. Wanachofanya madalali wanakuja kuchukua gari wanakwambia kuna mteja anataka aone gari. Wakipewa tu nusu saa nyingi wanarudisha gari wanakwambia mteja kaghairi kumbe wameshaweka mfukoni kati ya TSHS. 150,000 mpaka 800,000/= (kutegemeana na na aina ya gari).

Jinsi ya kudhibiti
1. Usiache gari lako "car wash"/gereji muda mrefu bila sababu za msingi. Watengeneze au waoshe wakati mwenyewe ukiwepo wakimaliza ondoka nalo. Ikiwa lazima kuliacha wapige mkwara kabisa kuwa unajua kuna wizi wa huo unga unaendelea ili wasijaribu kukuibia.
2.Kama unauza gari usiwape madalali waondoke nalo wenyewe. Tafuta mtu mwaminifu afuatane nao.
3. Jitahidi sana kuwa na fundi mmoja mwaminifu kwa ajili ya matengenezo ya gari yako. Ikitoke umewaachia mafundi wengine iwe ni ubovu wa dharura lakini nao wapige mkwara kuwa unafahamu kinachoendelea kuhusiana na wizi wa huo unga.

Tahadhari
Wengine wakishaiba wanakuwekea mle ndani vibati viwili (kimoja kila upande) na "steel wire" hii ya kuoshe vyombo katikati. Gari itaendelea kuwa na mlio wa kawaida. Kwa hiyo hutaweza kujua kwa haraka labda mpaka mwezi uishe. "Steel wire" ni suluhisho la muda kwani ni laini sana na kwenye "exhaust" kuna moto mkali sana kwa hiyo gari inaweza pata madhara muda wowote kadiri ile "steel wire" inavyoungua na kupunga.
 
Na rafiki yangu iko hivyohivyo. Ni sehemu gani wanatoa ili aweze kureplace?
Kureplace inabidi uende ukanunua kipande cha "exhaust" (lakini hakikisha kwanza hilo sega lipo ndani) kwenye maduka ya "used" utoe kilichopo ukauze kama chuma chakavu au wape tu zawadi mafundi hapo gereji.
 
Asante kwa taarifa. Kwa wastani ni bei gani?

Huwezi pata replacement ya huo unga. Nenda kwa fundi wa gari atoe kipande cha "exhaust" kinachohifadhi huo unga kinaitwa kibuyu ndivyo kinavyojulikana kwenye magereji mengi. Nenda kwenye maduka yanayouza "used" ununue kipande kingine waje wafunge/wakichomee. Ni kama unavyonunua "spare used" nyingine tu.
 
Asante sana.
 
Huu unga huwa unachanganywa na kinyesi cha mnyama flani (naomba nisimtaje hapa) kisha wanachukua mchanganyiko wanauza kilo moja shs laki 8 kwa ajili ya matumizi (naomba nisitaje matumizi)
Naona umemis kufatwa inbox
 
Back
Top Bottom