Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kwanza ningehakikisha raslimali zote za nchi mfano madini, gesi, mbuga za wanyama, mito, maziwa, ardhi yenye rutuba, nk. Zinakuwa na manufaa kwa nchi, badala ya mabeberu!
Nitahakikisha matajiri waubwa kama akina Ahmed Shabiby wanaotaka kila mwananchi kukatwa 2000 kila mwezi kwenye simu kwa ajili ya kufanyia ujinga gani sijui! Wanalipa kodi ipasavyo!
Maana hawa wafanyabiashara wakubwa ndiyo wakwepa kodi wakuu duniani kote huku wakishirikiana na watendaji wasio waaminifu serikalini.
Ningehakikisha nchi inakuwa na sheria kali za kuwabana wala rushwa, wabadhirifu, na wezi wa mali za umma. Yaani ukibainika umeiba, basi suala la kufilisiwa na kufungwa lile ni jambo la kawaida kabisa.
Nitajenga mifumo imara ya kisheria, kiuchumi, kijasusi, kisiasa, nk. ili kuondoa ule utegemezi wa mtu mmoja tu katika nchi. Yaani nitahakikisha kila mwananchi anatimiza wajibu wake.