Ungekuwa ujinga kumtaka kocha Nabi abaki Yanga milele

Ungekuwa ujinga kumtaka kocha Nabi abaki Yanga milele

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kila mtu hapendi aibu na kushuka. Hata Nabi na wachezaji wanaoondoka Yanga baada ya kuipa Yanga Mataji mengi na kucheza finali ya CAF wangependa kuondoka na sifa Yao hiyo kama ikiwezekana.

Ukiona kocha, mchezaji au mfanyakazi yeyote anaendelea kubaki kwenye kituo chake Cha kazi kwa muda mrefu ni ama Hana kitu Cha ziada, ameboreshewa maslahi kuliko anakotakiwa au ana shida za kiafya.

Uwezo wa Nabi na wachezaji wetu ndio umeishia pale, Sasa ni wakati wa kusonga mbele zaidi kwa kutafuta kocha mpya zaidi ya Nabi na wachezaji wapya zaidi ya wanaoondoka badala ya kukunja shingo.

Hata CCM hakuna Rais ambae anataka Chama kimfie mikono mwake hata kama anajuwa kuwa umaarufu wa Chama umepungua sana.

Nabi kuacha kumpa namba Dumbia ni ushahidi kuwa hakuhusishwa wakati wa usajili wake. Lakini hakuna kocha mwenye akili timamu atapenda kushiriki mashindano ya mapinduzi cup.
 
Umeandika vitu vingi havina logic, mchezaji ukimsajiri ni lazima umpange? Miqsone alisajiliwa na Pisto Misomane alikua ana mpanga? Chama Rs Berkane Ibenge alikua anampanga?
 
Umeandika vitu vingi havina logic, mchezaji ukimsajiri ni lazima umpange? Miqsone alisajiliwa na Pisto Misomane alikua ana mpanga? Chama Rs Berkane Ibenge alikua anampanga?
Kwahiyo unataka kutuaminisha kuwa Nabi ndiye alimtaka Dumbia ila Dumbia ndiye hakutimiza mashariti ya Nabi?
 
Mpira ni kununua na kuuza, using'ang'anie mchezaji yeyote ambae mkataba ukiisha anaondoka bure. Namna Yanga ilivyoumaliza mgogoro wake na Fei Toto utaisumbua sana Yanga kubakiza wachezaji wake. Timu inaendeshwa kisiasa kuliko kitaaluma. Hivyo hakuna kocha na mchezaji makini anaweza kubakia Yanga. Namna Yanga ilivyoumaliza mgogoro wake na Fei Toto umewavunja moyo wachezaji wenzake ambao walikuwa wakimshauri Fei afuate taratibu sahihi za kuondoka. Sasa hizi Fei amewaproove wrong wote waliokuwa wakimshauri kufuata kanuni za mpira
 
Back
Top Bottom