Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
16,717
Reaction score
13,176
Habari zenu wakuu,najua watu mko katika hali ya hatari na msongo wa mawazo kwa kuiona hii kitu ikitokea leo hii katika dunia Benetton retira foto do Papa beijando um imã no Cairo - Yahoo!.

sasa twendeni kwenye swali langu,
Wewe ni dereva wa malori na umeoa,kwahiyo unaposafiri unamuacha my wife wako peke yake nyumbani,lakini tabia ya mkeo sio nzuri kwa kweli,ukitoka huwa anaingiza bwana wake nyumbani kwako hapo,kitendo hicho kinawaudhi baadhi ya majirani na kukusubiri urudi ili wakuambie.
Basi uliporudi majirani wakakuambia yote yanayotendeka na wewe kuamua kufanya uchunguzi kwa kumuaga mkeo ya kuwa utasafiri siku hiyo, lakini ukweli ni kwamba hutosafiri bali utajificha katika nyumba moja ya majirani zako ili kijana huyo akija basi wakutaarifu ili ufumanie.

kweli ukamuaga mkeo kuwa utafasiri na kwenda Lubumbashi kwahiyo utakaa kama week hivi katika safari yako hiyo.

Usiku ulipowadia ,majirani wakamuona kijana akiingia katika nyumba yako wakaja kukutaarifu kuwa huyo mume mwenzio ameshafika,mzee bila kuchelewesha muda unatoka kwa ghadhabu ili ukafumanie

ulipofika mlangoni na kubisha hodi mara akatokea simba na kukuvamia na kutaka kukula lakini yule mume mwenzio akapata ujasiri akatoka na mchi na kumpiga nao Simba,Simba akakimbia na yeye akakuchukua akakuingiza ndani akaufunga na mlango,ukimuangalia jamaa amevaa khanga ya mkeo.

Je? utamfanyaje huyo mume mwenzio.Nalog off
 
Ni kweli atakuwa amekuokoa na unapaswa kushukuru, lakini hiyo huruma yake siyo ndo tiketi ya kuruka na mywife wangu aiseeee! Nitawachukulia hatua stahili ili kudhibiti hiyo hali isiendelee!

Siwezi kuendelea kudhalilika kwa sababu tu ni nimeokolewa, hata kidogo, sikubali! Ni bora wangeniacha nife.
 
piga jamaa mchi wa kichwa unakaulia mbali.Nalog off
 
nyumba gani iyo unagonga anatokea simba................yani izi ni story zingine loh! ila nimependa tu kua amejua wamepata mulizi wa house yao mana ingekua ni majambazi pia angewasaidia kupambana nao na wasingeibiwa au sio.........na log in
 
hapo hata mimi hamna mswalie mtume ni kumalizana tu na mke wangu aondoke na mwokozi wangu
 
nyumba gani iyo unagonga anatokea simba................yani izi ni story zingine loh! ila nimependa tu kua amejua wamepata mulizi wa house yao mana ingekua ni majambazi pia angewasaidia kupambana nao na wasingeibiwa au sio.........na log in
ni kwenye nyumba ya huyu dereva.Nalog off
 
Na-Apply kanuni ya FIFO (First In, First Out).

Bidhaa ya kwanza kuingia akili ilikuwa ni kufumania na kugawa kipondo, so nachofanya Nafumania, Mke nampa Talaka, jamaa nampiga mangumi mbaya halafu baada ya hapo namshukuru kwa wema wake kuniokoa.
 
Huko Kufikirika Kwangu huwa hainipi shida ya kutafakari maana ni kama stori ya kusadikika vile hakuna ukweli wowote.
 
sasa jamaa akikudunda?Nalog off
 
Huko Kufikirika Kwangu huwa hainipi shida ya kutafakari maana ni kama stori ya kusadikika vile hakuna ukweli wowote.
hii ni stori mkuu sio kisa kilichonitokea.Nalog off
 
Baada ya kuniokoa lazima turudi kwenye lengo lililonifanya nirudi, kwani ni yeye ndiye aliyenifanya nirudi mpaka nitake kuliwa na simba. Atakuwa na makosa mawili, kwanza ni la kuimba mke na la pili ni kusababisha mimi kutaka kuliwa na simba. Nalog off!
 
Back
Top Bottom