Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
Amekua muda mrefu akihisi mke wake anamuibia kwa kutembea nje yandoa. Akaamua aandae safari feki na kurudi ghafla bila mkewe kutarajia. Akarudi na Taxi usiku wa manane na aliamua dreva Taxi aweshahidi, akamlipa 100,000 ili waende wote kufumania. Akanyanyua Bastola, wakanyatia ndani mpaka chumba chakulala, akaingia yeye na dereva taxi kwa kupanda kwa kamba,akawasha taa na dreva akafunua blanketi alilojifunikia mke wake....wapo wawili!Mke wa jamaa yu kitandani na mwanaume mwingine!!!Jamaa akaweka bastola kichwani kwa yule mwanaume mgoni wake, ghafla mke wake akapaza sauti, Usimuue!Huyu bwana ametusaidia sana! Nlikudanganya niliposema nimerithi fedha. Ni yeye alinunua lile LandCruiser VX niliyokununulia, alilipia hii nyumba tunayomiliki sasa, alinipa zile pesa tulikuwa tunadaiwa na benki na analipia tiketi zetu zotetunavyoendaga maonyesho. Ndiye pia anayelipia ada za watoto wetu, hata hiyo suti uliyovaa na nyingine. Pia analipa kodi zetu za kilamwezi!Huku akiyumbayumba kwa kutoamini, MME AKASHUSHA BASTOLACHINI, akamtazama dereva, akamuuliza, UNGEFANYA NINI UNGEKUWA NI WEWE? Dreva Taxi akamwambia; Mfunike bwana, mfunike na hilo blanketi kabla hajasikia baridi