Smotor
JF-Expert Member
- Jan 3, 2021
- 2,461
- 2,058
Kutokana na hali ya umeme kwasasa,Habari wadau,
Jamiiforums imekuwa sehemu ya wanachama kushiriki kutoa maoni yao, kuelezea kero zao na kupata ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali nchini, nafasi inayowawezesha kufanya maamuzi mkiwa na taarifa sahihi na zenye ubora. Wapo viongozi wachache kama Dkt. Gwajima D ambao wamekuwa wakitoa ufafanuzi mara zote wanapohitajika.
Kama mkipata nafasi ya upendeleo ya kuletewa viongozi kwa siku maalum kwa lengo la kuwahoji na kutolea ufafanuzi wa kero mbalimbali hapa Jukwaani ungependa kiongozi gani awe wa kwanza na kwasababu gani?
View attachment 2910067
Nafikiri mkurugenzi wa Tanesco anapaswa kuanza.
Sababu umeme umekuwa kero kubwa.
Fikiria unasimu yako lakini huamini kama ndani ya dk 10 zijazo kama umeme utakuwepo,
Muda wote ni bora uwe kwenye charge.
Wenye biashara zinazotegemea umeme hawawezi ulipa kodi tena kutokaana na hela itokanayo na biashara hiyo.
Kwasasa natambua ukosefu wa umeme ni kama janga la kitaifa.
"juzi nlikuwa nasafiri kwa basi, simu yangu ilikuwa 20% lakini nliendelea na athari za saikolojia huenda hata umeme kwenye basi ungeweza kukatika"