Ungependa kiongozi gani aje Jukwaani kutoa majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini?

Kutokana na hali ya umeme kwasasa,

Nafikiri mkurugenzi wa Tanesco anapaswa kuanza.

Sababu umeme umekuwa kero kubwa.

Fikiria unasimu yako lakini huamini kama ndani ya dk 10 zijazo kama umeme utakuwepo,
Muda wote ni bora uwe kwenye charge.

Wenye biashara zinazotegemea umeme hawawezi ulipa kodi tena kutokaana na hela itokanayo na biashara hiyo.

Kwasasa natambua ukosefu wa umeme ni kama janga la kitaifa.

"juzi nlikuwa nasafiri kwa basi, simu yangu ilikuwa 20% lakini nliendelea na athari za saikolojia huenda hata umeme kwenye basi ungeweza kukatika"
 
Aje mama hangaya mwenyewe atuambie kwanini asitupishe
 
Mimi naomba aje Tundu Lisu na Mbowe huwa ni wasema ukweli kwa vitu vikivyojificha maana serikali yetu sikivu haina majibu ina propaganda tu.
 
Nakubaliana nawe changamoto za hasa Wizara ya Ardhi. Huko mbeleni changamoto kubwa inakuja kuwa migogoro ya ardhi, hivyo ni vyema wahusika wakatujuza mikakati ya kupambana na janga hili lijalo.
Kabisa
Ni janga kubwa ni mimi nshakuwa muhanga wa hiyo migogoro ya ardhi
 
Doh! hv ngosha si ndo iliosemekana ameharibu mzunguko wa pesa, vyuma vilikaza, leo tena ni mama! ameshaacha kuupiga mwingi na kuifungua nchi?
 
Naomba angekuja Mama mwenyewe maana hao wengine nao wakija kwa maswali yangu watampelekea Mama ni vizuri aje Mama Mwenyenyumba ili aone sehemu zinazovuja..
 
Kadri watakavyopatikana. Mambo mengi ni shida.
Mimi nataka waziri wa afya na kamishna wa uhamiaji.
 
Kuna mmoja akija nitamwambia tu hana akili basi. Sitakuwa na zaidi ya kuhojiana naye.
 
Kwangu nisingependakiongozi yeyote majibu na ufafunuzi wa jambo lolote. Nasema hivyo kwa sababu kwa miaka zaidi ya 20 kila mwaka tunapewa majibu yaleyale na ufafanuzi wa kero kubwa zinazotukabili.

Instead ningependa mawaziri watueleze wanatekelza nini kutatua kero zetu kubwa kisector na lini wanatarajia hizi kero zitaisha. Mh Raisi nametegema yeye atupatie ni hatua zipi zinatekeleza kututoa kwenye umasikini na kuboresha elimu yetu.
 
Nishati
Fedha
Usafirishaji
 
Mleteni Mh. Rais Samia.
 
Doh! hv ngosha si ndo iliosemekana ameharibu mzunguko wa pesa, vyuma vilikaza, leo tena ni mama! ameshaacha kuupiga mwingi na kuifungua nchi?
Watawala wa ccm wote ni 🚮. Usifikiri mimi ni mtu wa kusifia ujinga na upuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…