reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,203
- 28,789
Kuumbe Ndo maaana hakuna daladala za KikuyuKuna route Dom ya Town - Kikuyu kulikuwa kuna mgogoro wa hivyo,baadae wenye bajaji waliomba route hiyo,kwa sasa hakuna tena daladala ktk route hiyo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuumbe Ndo maaana hakuna daladala za KikuyuKuna route Dom ya Town - Kikuyu kulikuwa kuna mgogoro wa hivyo,baadae wenye bajaji waliomba route hiyo,kwa sasa hakuna tena daladala ktk route hiyo.
Tension inazidi kuwa kubwa kati ya bajaj na daladala. Na mara nyingi hii huwa inaleta vurugu na mahasi baina ya wahusika wa bajaj na daladala, ila pia migomo ambayo inapelekea tabu kwa wasafiri.
Currently, huko Arusha kuna mgomo wa daladala. Jamaa wa daladala wanalalamika bajaj wanawaharibia biashara kwa kuchukua wateja wao katika njia zao.
Bila kupendelea upande wowote, ni hatua gani ungependa zichukuliwe ili amani na utulivu udumishwe milele bila ya yoyote kuwa mhanga wa mgogoro wa dala dala na bajaj?
Karibuni.
Hii ni biashara huria. Daladala wanapaswa kuelewa wananchi kwanza hawapenzi huduma zao kwani ni duni sana. Hawana kauli nzuri na wengi wanakuwa wachafu.Tension inazidi kuwa kubwa kati ya bajaj na daladala. Na mara nyingi hii huwa inaleta vurugu na mahasi baina ya wahusika wa bajaj na daladala, ila pia migomo ambayo inapelekea tabu kwa wasafiri.
Currently, huko Arusha kuna mgomo wa daladala. Jamaa wa daladala wanalalamika bajaj wanawaharibia biashara kwa kuchukua wateja wao katika njia zao.
Bila kupendelea upande wowote, ni hatua gani ungependa zichukuliwe ili amani na utulivu udumishwe milele bila ya yoyote kuwa mhanga wa mgogoro wa dala dala na bajaj?
Karibuni.
Ahsante mtaaalaamSolution ni kuondoa bajaj kubeba abiria wa kuchangiana kwenye route ndefu kuanzia 7 kilometres hii itasababisha daladala waendelee kuchukua abiria wa route ndefu.
Nashauri hivi kwa kuangalia pia suala zima la usalama wa abiria wanaopanda bajaj kwenye route ndefu inakuwa changamoto kiasi lakini pia kufanya mgawanyo wa riziki ili kila mmoja apate kiasi.
Bajaj hatumii mafuta mengi kwenye route fupi hivyo huwalipa na daladala hapati hela nzuri kwenye route fupi sababu atalazimika kuchaji nauli ndogo na haitamlipa kwenye mafuta sababu atalazimika kukaa vituo vingi kwa nauli ndogo hivyo kukamua mafuta zaidi.
Hili suala lilishafanyika sana hata Arusha hapohapo coaster waliona hawawezi kushindana na hiache kwenye town trips ndio maana wakaamua kupiga route ndefu ambazo nauli yake ni ndefu kiasi.
Hizi ishu hata bajaj kwenye routefupi hulalamika pale bodaboda wakija maana wao kwenye foute ambayo bajaj atachaji 3000 boda anachukua 2000 na unafika fasta maana ni route fupi.
So binafsi nashauri wangetumia busara kuallocate hizi route na kuweka vituo rasmi vya bajaj maeneo ambayo sio stand za hiace za route ndefu ili mtu akitaka route ya kilometer tatu ataamua apande basi au bajaj.
Lakini pia kama bajaj wataamua kubeba abiria basi wawekewe special rate za kulipa TRA na Vibali vingine kama LATRA nk.
Ahsante mtaalamHii ni biashara huria. Daladala wanapaswa kuelewa wananchi kwanza hawapenzi huduma zao kwani ni duni sana. Hawana kauli nzuri na wengi wanakuwa wachafu.
Wananchi wanapanda daladala kwa sababu tu hawana mbadala na laiti wakipata mbadala hawatapanda hizo dala dala zao. Mfano nauli ya daladala na bajaji ikiwa sawa wengi watapanda bajaj na kuacha daladala.
Pia daladala waelewe muda na tekinilojia havisubiri. Leo wanaona kama biashara ya ni ya muhimu. Je kesho serikali ikijenga mwendokasi Arusha watafanyaje? Wajifunze kwa taxi na uber na waishi na bajaji in harmony.
Mwisho mimi nashauri mamlaka zisiwalegezee hizo daladala. Kama wanagoma wagome milele ila walazimishe bajaj zinaxokusanya abaria wachaji bei ile ile ya dala dala. Hakuna muda wa kubembeleza hizo dala dala. Na pia serikali ifikirie kujenga mwendokasi kwenye majiji ili kukomesha kiburi cha dala dala