SI KWELI UNICEF wanagawa pesa ukiwatumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba yao ya simu

SI KWELI UNICEF wanagawa pesa ukiwatumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba yao ya simu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu,

Kuna ujumbe huu umekuwa ukisambaa sana kwenye magroup za Whatsapp na nyingine zikitumwa na watu unaowafahamu.

Kuna mtu nimemwambia huu ni utapeli anabisha anaona kama namnyime fursa. Naomba mtusaidie kuhakiki hii, kama nitakuwa nimekosea nisiwakoseshe watu na fursa, kama ni habari ya uongo kama nnavyodhani basi tuokoe wengi wasipigwe.

Unicef funds.jpg
 
Tunachokijua
UNICEF ni shirika la umoja wa mataifa linalijihusuisha na masuala ya watoto liloanzishwa mwaka 1946 baada ya vita kuu ya pili ya dunia ikiwa na malengo ya kusaidia watoto na vijana wadogo ambao wapo katika mazingira magumu na kulinda haki zao. Kwa hivi sasa UNICEF inafanya kazi katika nchi zaidi ya 190 ulimwenguni kote.

Kumekuwepo na taarifa ambazo zinasambazwa katika makundi sogozi ya WhatsApp kuwa UNICEF wana mradi wa kutoa pesa kwa watu ambapo ili upate pesa hizo unapaswa kutoa kiwango cha pesa kilichopangwa ili upate zaidi, huku wengine wakionesha Screeshots za miamala waliyopata baada ya kujiunga na huduma hiyo.

picture1-png.3146181

Ukweli upoje kuhusu suala hilo?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa taarifa hizo si za kweli na wanaofanya hivyo wanfanya kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa watu na wakati mwingine kudukua akauntizao na kuzitumia kufanya matangazo yao ulaghai.

Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia kiungo (link) kilichoambatanishwa na taarifa hiyo ambacho ni cha mtandao wa WhatsApp, tumebaini kuwa kiungo hiko ni cha WhatsApp business ambayo inawezesha kuweka autoreply inayoleta majibu kadri ya ilivyoelekezwa na hapo baadaye inachukua taarifa zako na kufanya utapeli walioukusudia, ikiwa utaenda tofauti na vile inavyokueleza basi hautojibiwa tena kama inavyoonekana hapa chini.

picture2-png.3146185
Vilevile Picha za Screenshots zinazotumika kuonesha watu wameshinda fedha hizo ni za kutengenezwa na si halisi huku nyingi zikiwa na makosa na utofauti mkubwa ukilinganisha na jumbe halisia kutoka kwenye mitandao ya simu inayotoa huduma za kifedha.

picture3-jpg.3146186
Mathalani picha hapo juu ambayo wamekuwa wakitumia kuonesha kuwa muamala umepokelewa, wameweka muda ‘31/10/2024 Saa 6:08 PM’ ambapo neno ‘saa’ kwenye jumbe halisi za miamala huwa haliandikwi na badala yake ingekuwa ‘31/10/2024 6:08’ hali inayothibitisha kuwa ujumbe huo siyo halisi.

JamiiCheck pia imepitia mitandao ya kijamii ya UNICEF na kubaini kuwa hakuna ofa iliyotangazwa, lakini pia kupitia tovuti yao wamewatahadharisha watu kuhusu utapeli ambao unafanyika na baadhi ya watu kwa kutumia jina la shirika lao (UNICEF);

“Inawezekana kwamba umepokea au kuona ujumbe kwenye mitandao ya kijamii au WhatsApp ukiahidi zawadi za pesa taslimu au ukiomba maelezo yako ya kibinafsi kwa jina la UNICEF. Madai haya ni UONGO kabisa.

UNICEF haitoi aina yoyote ya zawadi ya pesa kupitia chaneli yoyote, iwe mtandaoni au kawaida. Hili ni jaribio la ulaghai la kuchukua fursa ya uaminifu wa watu”.
UNICEF wameandika.
Utawapata wengi sanaaa......maana wadanganyika kwa bure utashangaaa
....watakimbiliaa weee hao Unicef wenyewe hata hiyo budget ha2ana wala hawajuii kazi sanaaa
 
Watakuambia utume 50 kwanza ya malipo ya fomu, ukishatuma hutokaa uwaskie tena😅
 
Ila wabongo ni manyumbu... Yani utume pesa kwenda namba ya Kenya (+254) alafu UNICEF wakutumie hela 😂

Hapo utakuta huyo mkenya ashajipigia manyumbu wengi sana
 
IMG-20241107-WA0007.jpg


Hiyo namba ya World Humanitarian finance imesajiliwa kwa jina la Grace Maiko, anajitumia na hela kabisa ionekane muamala umetiki 😁.....nilichat nae akanikaribisha kwa swali nimejuaje shirika lao, nkamwambia nimesikia kwa mtu, akaniambia nijaze taarifa jina, nida, acc namba nikamwambia Grace una akili utafika mbali aakaacha na kujibu msg zangu
 
Utapeli huo. Atakayejaribu ndiyo basi tena. Ahesabie maumivu. Njia pekee nzuri ya kupata pesa ni ile ya kuzitafuta kihalali. Nje ya hapo, ni mateso tu na laana.
 
In magufuli voice hakuna cha bure vijana chapen kaziiiii
 
Kwamba ishu kama hii nayo unahitaji Jamiicheck
 
Wakuu,

Kuna ujumbe huu umekuwa ukisambaa sana kwenye magroup za Whatsapp na nyingine zikitumwa na watu unaowafahamu.

Kuna mtu nimemwambia huu ni utapeli anabisha anaona kama namnyime fursa. Naomba mtusaidie kuhakiki hii, kama nitakuwa nimekosea nisiwakoseshe watu na fursa, kama ni habari ya uongo kama nnavyodhani basi tuokoe wengi wasipigwe.


UNICEF haiwezi kufanya biashara za kijinga namna hiyo. Hao ni matapeli wakubwa wa Tanzania.
 
Duniani mijinga haiishi, hapa tunaitahadharisha huu ni UTAPELI, ila utashangaa kuna mipumbavu itatuma pesa na kuja kulia lia hapa.
 
Si kweli toka zamani. Jumbe hizo ni za kitambo, wanaopigwa ni wale ambao hawajasanuliwa.
 
Wakuu,

Kuna ujumbe huu umekuwa ukisambaa sana kwenye magroup za Whatsapp na nyingine zikitumwa na watu unaowafahamu.

Kuna mtu nimemwambia huu ni utapeli anabisha anaona kama namnyime fursa. Naomba mtusaidie kuhakiki hii, kama nitakuwa nimekosea nisiwakoseshe watu na fursa, kama ni habari ya uongo kama nnavyodhani basi tuokoe wengi wasipigwe.

Utapigwa huo ujumbe uko muda mrefu mtandaoni hao ni matapeli wa kenya na kuna jamaa wameishalizwa sana don't try.
 
Back
Top Bottom