- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu,
Kuna ujumbe huu umekuwa ukisambaa sana kwenye magroup za Whatsapp na nyingine zikitumwa na watu unaowafahamu.
Kuna mtu nimemwambia huu ni utapeli anabisha anaona kama namnyime fursa. Naomba mtusaidie kuhakiki hii, kama nitakuwa nimekosea nisiwakoseshe watu na fursa, kama ni habari ya uongo kama nnavyodhani basi tuokoe wengi wasipigwe.
Kuna ujumbe huu umekuwa ukisambaa sana kwenye magroup za Whatsapp na nyingine zikitumwa na watu unaowafahamu.
Kuna mtu nimemwambia huu ni utapeli anabisha anaona kama namnyime fursa. Naomba mtusaidie kuhakiki hii, kama nitakuwa nimekosea nisiwakoseshe watu na fursa, kama ni habari ya uongo kama nnavyodhani basi tuokoe wengi wasipigwe.
- Tunachokijua
- UNICEF ni shirika la umoja wa mataifa linalijihusuisha na masuala ya watoto liloanzishwa mwaka 1946 baada ya vita kuu ya pili ya dunia ikiwa na malengo ya kusaidia watoto na vijana wadogo ambao wapo katika mazingira magumu na kulinda haki zao. Kwa hivi sasa UNICEF inafanya kazi katika nchi zaidi ya 190 ulimwenguni kote.
Kumekuwepo na taarifa ambazo zinasambazwa katika makundi sogozi ya WhatsApp kuwa UNICEF wana mradi wa kutoa pesa kwa watu ambapo ili upate pesa hizo unapaswa kutoa kiwango cha pesa kilichopangwa ili upate zaidi, huku wengine wakionesha Screeshots za miamala waliyopata baada ya kujiunga na huduma hiyo.
Ukweli upoje kuhusu suala hilo?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa taarifa hizo si za kweli na wanaofanya hivyo wanfanya kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa watu na wakati mwingine kudukua akauntizao na kuzitumia kufanya matangazo yao ulaghai.
Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia kiungo (link) kilichoambatanishwa na taarifa hiyo ambacho ni cha mtandao wa WhatsApp, tumebaini kuwa kiungo hiko ni cha WhatsApp business ambayo inawezesha kuweka autoreply inayoleta majibu kadri ya ilivyoelekezwa na hapo baadaye inachukua taarifa zako na kufanya utapeli walioukusudia, ikiwa utaenda tofauti na vile inavyokueleza basi hautojibiwa tena kama inavyoonekana hapa chini.
Vilevile Picha za Screenshots zinazotumika kuonesha watu wameshinda fedha hizo ni za kutengenezwa na si halisi huku nyingi zikiwa na makosa na utofauti mkubwa ukilinganisha na jumbe halisia kutoka kwenye mitandao ya simu inayotoa huduma za kifedha.
Mathalani picha hapo juu ambayo wamekuwa wakitumia kuonesha kuwa muamala umepokelewa, wameweka muda ‘31/10/2024 Saa 6:08 PM’ ambapo neno ‘saa’ kwenye jumbe halisi za miamala huwa haliandikwi na badala yake ingekuwa ‘31/10/2024 6:08’ hali inayothibitisha kuwa ujumbe huo siyo halisi.
JamiiCheck pia imepitia mitandao ya kijamii ya UNICEF na kubaini kuwa hakuna ofa iliyotangazwa, lakini pia kupitia tovuti yao wamewatahadharisha watu kuhusu utapeli ambao unafanyika na baadhi ya watu kwa kutumia jina la shirika lao (UNICEF);
“Inawezekana kwamba umepokea au kuona ujumbe kwenye mitandao ya kijamii au WhatsApp ukiahidi zawadi za pesa taslimu au ukiomba maelezo yako ya kibinafsi kwa jina la UNICEF. Madai haya ni UONGO kabisa.
UNICEF haitoi aina yoyote ya zawadi ya pesa kupitia chaneli yoyote, iwe mtandaoni au kawaida. Hili ni jaribio la ulaghai la kuchukua fursa ya uaminifu wa watu”. UNICEF wameandika.