Wanaweza kumaanisha unlimited speed au unlimited download volume.
Hebu tuandikie hilo tangazo lao tuone.
Kwenye hizi taaluma mimi mgeni kidogo, lakini nina wasiwasi hapo kwenye red, hivi technically inawezekana?
....inaweza kuwa kwamba device uliyonayo (Blackberry kwa mfano) ambayo maximum speed yake ya ku-download ni 1Mbps, halafu ISP anatoa 2Mbps.
Jamani mimi natumia Zantel kwenye huduma ya internate,cha ajabu kwenye package zao ziwe za saa 24,siku 7 au siku 30 wanatangaza kuwa ni Unlimited ilihali ni UONGO,ukishusha vitu vingi inaisha kabla ya muda wake na unatakiwa uongeza hela sasa hiyo UNLIMITED ina maana gani,tafadhali wajuzi naomba mtutoe matongotongo ya hizi huduma.Kwenye speed sina tatizo nako ,Zantel ni nambare wani.
Tanzania hakuna advertising standards, unaweza ukaandika chochote kile. Nilikumbana na tatizo hili hili Zain baada ya kununua Unlimited Data package yao.
Sehemu zengine utakuta kuna kinyota baada ya Unlimited* ujue kuna fair usage policy ambayo inadai unlimited means 200Mb/month, wizi mtupu.
Kwenye wireless internet kuwa na Unlimited ni ngumu sana, kwa sababu bandwidth ni limited resource.
Hakuna kitu kama unlimited speed, haileti maana yoyote.
Tatizo ni LUGHA YA BIASHARA!
Katika miaka ya hivi karibuni tangu watanzania wajifunze lugha za 'kibishara' kila kitu kimeharibika! Sio kwenye mashirika ya umma wala binafsi! Hebu angalia kwa ufupi magazeti yetu yanavyotumia lugha za biashara! Unakuta bonge la kichwa cha habari kwa lugha ya 'kibiashara' ili hali ukisoma ndani unakuta havishabihiani na kichwa cha habari!
"MWALIMU NYERERE ALIMPAPASA AMINA CHIFUPA"! Mara "WANTED"! Mara "VIONGOZI WA DECI MATATANI"
Yani kunakila aina ya lugha ya 'kibiashara' siku hizi inatumika kuficha ukweli wa huduma unavyotolewa. Angalia matangazo ya promotions nyingi za kampuni za simu ni feki. Wanakwambia ukijiunga na XTREME unaongea BURE! Zain nao ni vivyo hivyo! Kwa hiyo ndugu zangu kuna kila udanganyifu katika matangazo ya Taasisi hizi. Mara nyingi sana nakuwa makini kwa kiwango kikubwa katika matangazo ya vyakula na madawa ya binadamu aidha katika taasisi zilizo na mamlaka au za kienyeji! Huku ndo watanzania wengi tunaumia.
Sasatel wanazo Bundle za Unlimited ya kweli (hamna quota)
Kuna
Bundle za 250,000/- per month for 5 computers
Bundle za 500,000/- per month for 6-10 computers
Bundle za 840,000/- per month for 11-30 computers
Kuna pia za prepaid za 600mb , 3gb up to 10gb pia
B.P - 2009